GET /api/v0.1/hansard/entries/238514/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 238514,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/238514/?format=api",
    "text_counter": 195,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, Hoja hii ni muhimu sana. Hatuwezi tukashinda vita vya kupigana na ufisadi bila uhuru wa habari. Ufisadi ni kufichua wizi na huwezi kufichua wizi, bila habari. Sheria hii itatusaidia kupigana na uongo tunaosoma katika vyombo vya habari. Uhuru huu ukiwepo, na kama watu wataweza kupewa habari zilizo sahihi, basi mtu akipatikana anasema uongo itakuwa ni haki mtu huyo kuchukuliwa hatua. Kwa hivyo, naamini sheria hii itatusaidia kuondoa uongo wakati wa kupatia watu wetu habari, yaani upotoshaji wa habari. Unakwenda kwa mkutano na unasema moja, lakini ukiangalia magazeti keshoye, habari ni tofauti kabisa hata huwezi kutambua yale yaliyomo kwa magazeti kama ndio uliyosema mkutanoni."
}