GET /api/v0.1/hansard/entries/238987/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 238987,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/238987/?format=api",
"text_counter": 147,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 246,
"legal_name": "Joseph Matano Khamisi",
"slug": "joseph-khamisi"
},
"content": "Ningependa wakati mambo haya yanapofanywa, tushirikiane na Serikali ili tuwaelimishe wananchi ili wajue kwamba masingaombwe ni ndoto tu za kiutamaduni. Hili si jambo ambalo linatokea katika ulimwengu wa sasa. October 17, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 2947 Bw. Naibu Spika, kumekuwa na mazungumzo mengi kuhusu ukosefu wa madaktari. Hivi majuzi nilizuru Indianapolis, Marekani, kuwatembelea watoto wangu. Mtoto wangu mmoja anafanya kazi huko kama daktari. Niliwaona madaktari saba kutoka Kenya ambao wanafanya kazi katika hospitali za kigeni. Malalamiko yao makubwa ni kwamba Serikali hailipi mishahara mizuri ya kuweza kuwahifadhi katika hospitali zetu. Ningeiomba Serikali mara kwa mara iwe ikiangalia mambo ya mishahara ya wafanyakazi ili tuwahifadhi madaktari wetu. Badala yao kwenda nchi za kigeni wanaweza kufanya kazi hapa. Tunaona kwamba wauguzi wengi wanakimbilia nchi za kigeni kufanya kazi huko kwa sababu kuna mishahara na marupurupu mazuri. Hilo linaweza kuwa ni jambo zuri lakini kwa upande wa Kenya si jambo nzuri kwa sababu pesa ambazo tunazitumia kuwaelimisha watu hawa ni nyingi. Ikiwa tutawaacha watu hawa kufanya kazi katika hospitali za kigeni, basi tunawanyima Wakenya huduma ambazo wangeweza kuzipata kutoka kwao. Bw. Naibu Spika, jambo lingine ni kuhusu madaktari wa kienyeji. Najua Serikali imejaribu kuwaleta karibu na kuwaunganisha madakatari hawa wa kienyeji ili waweze kuungana na madaktari wa kisasa katika kutibu magonjwa. Hata hivyo, Serikali haijawapa nafasi ya kutosha ya kuweza kujumuika pamoja na madaktari wa kisasa. Ingekuwa bora zaidi, kama tungelipata ripoti kutoka kwa Serikali kuhusu jambo hili. Bw. Naibu Spika, ningependa kupata ufafanuzi kutoka kwa Serikali kuhusu wenyeji ambao wanajiita madaktari. Sielewi kama madaktari wa kienyeji wamehitimu kuweza kuitwa madaktari. Jambo hili linawapotosha wananchi. Wakisikia ni daktari wanadhani ni daktari kamili. Lakini mtu huyu hajapata masomo yoyote ya uuguzi. Mara nyingi ukienda Mkoa wa Kati, utapata vibao vya hawa madaktari vimepachikwa kwenye kuta za nyumba. Vinasema hivi: \"Daktari kutoka Tanzania au Pwani\". Hii ni kuonyesha kwamba madaktari wa kienyeji kutoka Pwani na Tanzania ndio waganga maarufu kushinda madaktari kutoka sehemu nyingine. Bw. Naibu Spika, ningependa kuzungumza kuhusu zile kandarasi zilizotolewa kwa wauguzi waliokuwa wakifanya kazi ya dharura au ya kujitolea wakati wauguzi wa Serikali walipogoma. Wengi wao baada ya mgomo, walitimuliwa kutoka kazi mwao. Walijitolea kimhanga kuweza kuisaidia Serikali wakati wa dharura lakini baada ya mgomo kumalizika, wakasahauliwa. Nafahamishwa kwamba ni asilimia 40 ya wao ambao waliajiriwa na Serikali. Waliosalia wanatukera maofisini mwetu wakiuliza Serikali itawajiri lini na ilhali walifanya kazi kwa muda wa miezi sita. Najua kwamba kuna kazi ambazo hivi majuzi zilitangazwa. Ni matumaini yangu kuwa wao watapewa nafasi za kwanza na kuajiriwa kwa sababu walijitoa mhanga wakati wa mgomo. Baadaye, tunaweza kuwaajiri watu wengine. Bw. Naibu Spika, ningependa kuzungumza kuhusu swala la madawa. Hivi leo tumesoma katika vyombo vya habari kwamba hospitali nyingi, hasa katika mikoa ya Nyanza na Bonde la Ufa, hazina dawa na vifaa vingine muhimu. Tunaambiwa ya kwamba hospitali nyingi katika mikoa hiyo zitasimamisha huduma kwa wananchi kwa sababu ya ukosefu huo."
}