GET /api/v0.1/hansard/entries/239432/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 239432,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/239432/?format=api",
"text_counter": 284,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kingi",
"speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
"speaker": {
"id": 27,
"legal_name": "Amason Jeffah Kingi",
"slug": "amason-kingi"
},
"content": " Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii ili nizungumzie Hoja iliyo mbele yetu. Nataka kuunga mkono Hoja hii ambayo inanuia kutupatia nafasi ya kwenda nyumbani ili tuweze kushirikiana na wananchi katika mipango mingine mingi ya maendeleo. Ningetaka kuchukua fursa hii kuishukuru Serikali kwa miradi mingi ya maendeleo ambayo imeanzishwa kila mahali katika taifa letu. Hii ni miradi ya elimu, barabara, afya, kilimo na kadhalika. Tunajionea miradi hii tunapoenda katika mawakilisho yetu. Hata hivyo kuna mambo fulani ambayo tunahitaji kuzingatia ili maisha yetu yazidi kuboreka. Mojawapo ya mambo hayo ni usalama wa wananchi na mali yao katika taifa letu. Jambo hili la usalama ni la umuhimu sana. Tunapoelekea nyumbani, kuna miradi tumeanzisha, kama mradi wa kushirikiana kati ya wananchi na polisi kupambana na wahalifu, yaaani, community policing . Ningetaka kuwauliza Wabunge, wakati tutakapokuwa katika mawakilisho yetu tukijumuika na wananchi, tuweze kusisitiza umuhimu wa mfumo huu wa community policing ili tupunguze uhalifu katika sehemu tunazowakilisha. Bw. Naibu Spika, maisha ya vijana wengi yako hatarini kwa sababu ya utumiaji wa madawa ya kulevya. Kila siku tunasoma habari kwamba maisha ya vijana wengi yanaangamia kwa sababu ya madawa haya. Ni jukumu letu kama Wajumbe tuzungumze na vijana na wananchi wote kwa jumla ili utumiaji wa madawa haya ya kulevya umalizike katika taifa letu. Ikiwa tunafahamu watu ambao wanauza madawa haya kwa vijana wetu, tuweze kushughulika na kuripoti watu hawa ili wachukuliwe hatua. Hii ni pamoja na vinywaji vingine ambavyo havijahalalishwa na vinaangamiza wananchi. Bw. Naibu Spika, kwa muda mchache uliopita tuliona Wizara ya Elimu ikiajiri walimu. Pia tumeona Wizara ya Afya ikiajiri wauguzi, lakini kuna Wizara nyingine ambazo ni muhimu sana kwa maisha yetu, kwa mfano, Wizara ya Kilimo. Tungetaka kuuliza kwamba Wizara hii pia iajiri August 3, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 2629 maofisa zaidi ili waweze kutembea kwenye mashamba ya wananchi na kuwapa maarifa ya kukuza mimea ili tabia hii ya kuombaomba chakula kila wakati imalizike. Bw. Naibu Spika, kwa upande wa misaada ya elimu yaani, bursaries tunashukuru Serikali kwa sababu imekuja na mfumo wa kupeana pesa za masomo. Tatizo lililoko ni kwamba sehemu kame na maskini ambapo wazazi hawawezi kupeleka watoto shule kwa sababu wazazi ni maskini ndizo zinaendelea kuumia wakati wa kugawanya fedha hizi. Utapata Eneo Bunge kama langu linapata Kshs500,000 na kuna mawakilisho mengine katika jamhuri hili ambayo yanapatiwa milioni kumi au milioni nane. Mawakilisho ambayo yanapatiwa pesa nyingi ni yale ambayo labda maisha ya wananchi wao ni mazuri kwa sababu wana rasilmali mbali mbali na wanaweza kupeleka watoto wao shuleni. Wakati wakuhesabiwa vijana hawa, unapata kwamba wale wa sehemu hizo ni wengi kuliko sehemu hizi ambazo watu hawana pesa. Vijana wanaoenda shule ni wachache na kwa hivyo wanaendelea kuumia. Tungeomba mfumo huu ubadilishwe ili sehemu zile kame na zile ambazo haziwezi kujimudu ziweze kupata pesa zaidi kuliko vile mpango unavyoendela kwa wakati huu. Bw. Naibu Spika, tatizo lingine tulilo nalo katika taifa letu linahusiana na wizi wa mifugo. Tunataka kuwaomba wananchi waache tabia hii mbaya; tabia ambayo imeleta maafa, vifo, chuki na matatizo makubwa katika taifa letu. Siku hizi wafugaji wote wanaweza kwenda kutafuta mikopo na kufuga mifugo wao badala ya kuiba ya wenzao. Kwa hivyo, tunataka tabia hii ikomeshwe! Kwa hayo machache, naomba kuunga mkono."
}