GET /api/v0.1/hansard/entries/239684/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 239684,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/239684/?format=api",
"text_counter": 219,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwenje",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Co-operative Development and Marketing",
"speaker": {
"id": 257,
"legal_name": "David S. Kamau Mwenje",
"slug": "david-mwenje"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, niko ndani ya Serikali hii na nasema mahindi hulipwa. Bw. Rotino amesema kwamba silimi mahindi, lakini mimi ni mkulima wa mahindi. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna msemo wa Kiswahili husema: \"Usinipe samaki kutoka 2530 PARLIAMENTARY DEBATES August 2, 2006 kwa refrigerator ! Nionyeshe jinsi ya kuvua samaki kutoka kwa maji.\" Kitakachookoa nchi hii ni kuwasaidia wanaokumbwa na baa la njaa - kama huko Mwingi na Kitui - kupata maji ili waweza kulima. Hakuna wakati hatutalia njaa ikiwa hatutawapatia watu maji ya kulima. Kutegemea kupewa chakula kila wakati ni jambo la umaskini kabisa. Tutaishi na umasikini miaka yote ikiwa hatutaanza miradi ya kunyunyisha mashamba maji. Bw. Musila na Bw. Kalonzo walizungumzia mambo ya kwao. Taabu hiyo inatokana na ukosefu wa maji. Tunatakiwa kusuluhisha shida hizo. Tunaweza kutumia pesa ya Constituency Development Fund (CDF) kujenga visima ili kuwasaidia watu. Bw. Naibu Spika wa Muda, pia inatakiwa watu wapande miti. Ni kwa nini kuna sehemu ambazo mito imekauka? Ni kwa sababu hakuna miti. Watu wetu lazima waambiwe wapande miti. Hatuwezi kuwa na mito bila miti. Bei ya mashine za kupiga maji iko juu sana. Lazima tupunguze bei ya mashine za kupiga maji, ili watu waweze kuzitumia kulima. Hata mahali kuna maji, watu wanaweza kushindwa kulima kwa sababu hawawezi kununua mashine hizo. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaunga mkono Hoja hii ili tuweze kuleta Mswada kuhusu jambo hili hapa Bungeni. Kuna haja ya kuunda Kamati ya kuangalia modalities za kutayarisha Mswada huu. Hivi sasa---"
}