GET /api/v0.1/hansard/entries/239720/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 239720,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/239720/?format=api",
    "text_counter": 255,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. M.Y. Haji",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 26,
        "legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
        "slug": "yusuf-haji"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaunga mkono Hoja hii. Ningetaka kusema Prof. Oniang'o juu, juu, juu sana, kwa sababu sehemu anakotoka kule Butere ni sehemu ambayo Mungu amewabariki kwa maji na ardhi nzuri. Ameleta Hoja hii kwa sababu anajali maslahi ya ndugu zake ambao wanakufa kila siku kwa njaa. Badala ya Serikali kuunda tume ambazo zinatumia Kshs258 milioni, ni kwa nini Serikali isichukue wataalam wa nchi hii ili waende wakasome na kutafuta njia ya kupambana na ukosefu wa chakula? Hatuwezi kupambana na njaa kwa kutoa chakula cha misaada. Tunapotoa chakula tunawafanya watu wawe wanyonge na wasiweze kufikiria kujisaidia wenyewe. Tunataka wataalam wetu waangalie njia za kuanzisha miradi ya kunyunyizia mashamba maji. Utapata kwamba mvua ikinyesha barabara zote katika sehemu za ukame hubadilika kuwa mito na maji haya yote hutiririka mpaka baharini. Tukitafuta njia ya kuyakusanya maji hayo na kuleta utaalam wa kupanda mimea ambayo inaweza kukua haraka, tutaweza kupambana na janga la njaa. Inaonekana kwamba Waziri wa Miradi Maalumu anashughulika na mambo ya njaa peke yake. Hiyo inaonyesha kwamba Serikali inataka kufanya biashara na maisha ya wananchi wa Kenya. Tunataka Wizara ambayo itasimamia kwa jumla, mambo ya utekelezaji wa maendeleo katika sehemu zetu kame. Kwa hayo machache, ningependa kusema: Prof. Oniang'o, juu, juu, juu sana! Asante!"
}