GET /api/v0.1/hansard/entries/239761/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 239761,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/239761/?format=api",
    "text_counter": 296,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika wa Muda. Ninachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia fursa hii ili niweze kuchangia Hoja iliyo mbele yetu. Ninamuunga mkono na kumpongeza mhe. ole Metito kwa kuileta Hoja hii. Hoja hii inazungumza juu ya watoto yatima na elimu yao. Maswala haya mawili ni muhimu na yangeshughulikiwa jana wala si leo. Korani Tukufu inatwaambia: \" Kullu nafsin dhaaikatul maut \", inayomaanisha kila kiumbe siku moja kitakufa. Wanaotunga sera, na Serikali kwa jumla, ni kama roho zao zimetengenezwa na chuma na ni kama kamwe, hawatakufa siku moja. Hivyo basi, wamesahau kuwapangia watoto yatima. Ingawa kifo ni lazima kwa kila mwanadamu, kifo cha jana, cha zamani na cha leo ni tofauti. Leo kuna ugonjwa unaowaua watu katika nchi hii kutoka kila pembe ya nchi na kila sekta ya uchumi wetu. Licha ya Serikali kutangaza Ukimwi kama jangwa la kitaifa, imesahau kutenga pesa maalum za kupigana na ugonjwa huu. Inategemea wafadhili na michango kutoka nje. Ulimwengu unaamini kuwa Kenya si nchi maskini bali ufisadi umetanda. Tusipokuwa na sera, sheria na pesa za kuwasaidia watoto yatima, tegemeo lao litakuwa ni nini? Ndio maana nimesema mara nyingi katika Bunge hili kuwa tuko na watunzi sera bubu, tuko na viziwi ambao hawasikii, hawasemi wala kuona haki za watoto yatima. Bw. Naibu Spika wa Muda, Serikali inajigamba kwamba imeanzisha elimu ya msingi ya bure. Kila siku, kuna doa linalotokea kwa elimu ya bure. Kwanza, idadi ya watoto waliojiandikisha shuleni ni wengi kuliko wale waliokuweko zamani. Idadi ya walimu waliopo haimudu kusomesha watoto wale. Leo, mwalimu mmoja anasomesha kati ya watoto 120 hadi 200 katika darasa moja. Hapo awali, kila mwalimu alikuwa akisomesha watoto 40. Kwa hivyo, idadi ya walimu haitoshi kuendesha shughuli za elimu ya msingi ya bure. Kuna ukosefu wa karakana. Watoto wanakaa chini ya miti. Serikali imepiga hatua nyingine mbele na kutoa bursary kwa watoto yatima kupitia kwa CDF. Sheria inatuambia kuwa CDF inategemea pendekezo ambalo linatoka katika lokesheni. Lokesheni inasema kuwa CDF haiwezi kutoa bursary. Kwa nini Serikali isiwe na sera maalum ya kuwezesha sera ya elimu ya msingi ya bure kuendelea mbele. Wanakula huku wakitumia majina ya watoto mayatima. Bw. Naibu Sika wa Muda, vile mwenzangu alivyosema ni kweli. Hii imeathiri sehemu nyingi za nchi hii. Mashirikia yasiyo ya Serikali yanaleta pesa kutoka nje, yanachukua picha za watoto na kamwe hawatoi msaada wowote kwa watoto hao. Wanadhulumu watoto mayatima, lakini Mwenyezi Mungu anawaona. Kwa nini Serikali isichukue hatua kwa watu kama hao? Bw. Naibu Spika wa Muda, iwapo Kshs350 milioni iliyopewa tume ya Goldenberg hivi majuzi ingetumiwa kwa kusaidia watoto mayatima, hizo pesa zingefanya kazi ya maana sana. Watoto wetu wanahangaika na hawana mwelekeo wala tegemeo, na Serikali inalipa Jaji Kshs350 milioni. Sasa sisi, nini kipa umbele chetu kama Serikali? Pesa za Goldenberg \"zimeliwa\" miaka hiyo na wewe leo unaacha watoto mayatima wanaangamia! Bw. Naibu Spika wa Muda, nasikitika Makamu wa Rais hayuko hapa. Afisi yake inayohusika na watoto wamekwenda wakafunga Africa Muslim Agency iliyokuwa na zaidi ya mashule ishirini katika nchi ya Kenya. Pia walifunga Almuntha Dalislami. Shirika hili lilikuwa linasaidia watoto mayatima. Wanadai kwamba wanahusiana na Al-Qaeda. Kwa nini wasishtakiwe na shirika lisaidie watoto? Badala ya kuwalinda watoto mayatima unawanyanyasa. Baada ya Africa August 2, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 2549 Muslim Agency kufungwa, zaidi ya watoto 2,000 mayatima wamerudi nyumbani bila kuwa na tegemeo. Wakati Serikali inapochukuwa sera kama hii, kwa nini isiangalie athari ya uwamuzi wao? Ni kwa nini kuwadhulumu watoto mayatima? Bw. Naibu Spika wa Muda, katika mazungumzo yake, Waziri anasema umaskini unadhaniwa kuwa wa kiwango cha juu katika nchi ya Kenya. Lakini ningependa kumweleza kwamba umaskini haudhaniwi, umetanda na sura yake mbaya inaonekana kila mahali katika nchi ya Kenya. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}