HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 241348,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/241348/?format=api",
"text_counter": 194,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kuhusu kuufufua na kuuimarisha uchumi, lakini jambo muhimu kwanza kwa kila Mkenya ni kuipenda nchi hii. Sisi Wakenya ni kana kwamba tunaichukia nchi yetu. Tunapotembelea nchi za ng'ambo na kukutana na wageni, tunaitusi nchi yetu kwa sababu mtu mmoja au wawili wamekosea kwa njia moja au nyingine. Inafaa mtu akiyatembelea mataifa yaliyostawi ajigambe na nchi yake. Serikali imeanzisha sera nzuri ambazo zinatarajiwa kutuwezesha kuufufua uchumi wa nchi hii. Waziri wa Biashara na Viwanda ametembelea nchi nyingi ulimwenguni. Amezungumza mambo mazuri katika mkutano wa WTO na kwingineko. Tumerahisisha sana utaratibu wa kufunguliwa kwa kampuni nyingi na wageni wanaotaka kuleta raslimali zao humu nchini. Lakini, jiulize: Ni nani anayefaidika? Utaona kwamba nchi hii inafaidika kwa kiasi kidogo tu kutokana na kuajiriwa kwa wafanyakazi katika kampuni hizo. Wanaofaidika sana ni wageni wenye raslimali. Bw. Naibu Spika, wakati umefika wa kubadili fikira zetu na kuiga mifano kutoka nchi zilozostawi. Nchini Afrika Kusini, utajiri ulikuwa umethibitiwa na wageni. Nchini Saudi Arabia, hali ilikuwa hivyo hapo awali. Lakini, Serikali za nchi hizo zilikata shauri kutajirisha watu wao. Wakasema: \"Njooni, tumetengeneza mazingira bora ya kuweka raslimali, lakini, mkija, ni lazima mtafute mzalendo ambaye atakuwa mshirika wenu.\" Pili, serikali za nchi hizo zilizitambua sekta fulani za chumi zao ambazo zilihitaji ushirikiano wa kibiashara na nchi jirani. Barani Afrika kuna biashara nyingi sana tunazoweza kuzifanya na tufaidike. Kwa nini bado tunaenda Ulaya na kwingineko, na kuziacha nchi kama Nigeria, Rwanda na nchi nyinginezo barani Afrika? Ningetaka kumwomba Waziri, ambaye amefanya juhudi kubwa ili kuufufua uchumi wa nchi, aanze kuyazuru mataifa barani Afrika. Kwa sababu, ukiangalia, utaona kwamba nafasi nyingi zinazohusiana na nchi hii kiuchumi zinapatikana katika bara hili. Hii ni kama ajali tu. Siyo kwamba tumeweka harakati nyingi za kufanya biashara na Waafrika wenzetu. Ni kweli kwamba barabara na reli zetu haziko sawa. Lakini, tusitarajie Waziri wa Biashara na Viwanda kuzirekebisha kwa sababu hiyo siyo kazi ya Wizara hii; ni kazi ya Wizara nyingine. Kuanzia sasa, inafaa tukipeleka mabalozi katika mataifa ya Kiafrika, wasiwe mabalozi ambao kazi yao ni kunywa mtindi na kupiga gumzo. Inafaa tupeleke mabolozi kamili ambao ni wafanyibiashara. Trade Attaches' watakuwa wakiwasaidia mabalozi hao katika kazi zao. Miaka 2322 PARLIAMENTARY DEBATES July 25, 2006 iliyopita, mabalozi kutoka nchi zilizostawi walikuwa na majukumu ya kuzitafutia nchi zao nafasi za biashara ugenini. Hivyo ndivyo tunavyostahili kufanya ili tuweze kuziendeleza nchi zetu Barani Afrika. Bw. Naibu Spika, nilizungumza hapa juu ya sekta ya Jua Kali. Ukizitembelea ofisi za Serikali, utaona viti kutoka Dubai na kwingineko. Sasa, tunataka tujenge maabara ya Jua Kali katika sehemu zote nchini ili tuwafundishe maseremala na mafundi wengine jinsi ya kuboresha bidhaa zao ili tuanze kuviuza katika nchi za ugenini. Kila tunapowahitaji wageni walete raslimali zao humu nchini, Serikali huwapa motisha. Lakini hatufanyi hivyo kwa Wakenya. Wahenga walisema kwamba ukarimu huanzia nyumbani kwako. Inafaa tuanze kufanya hivyo na tuzipende bidhaa zetu. Mapema miaka ya 1970, katika sehemu ya Viwandani kulikuweko na viwanda vingi sana vilivyokuwa vikisimamiwa na Wakenya. Lakini, Wakenya hawakuwa wakizinunua bidhaa hizo zilozokuwa zikitengenezwa na Wakenya wenzetu. Walikuwa wakinunua bidhaa kutoka kwa viwanda vya wageni. Hiyo ni kwa sababu tunajidharau. Hatufikiri kwamba Mwafrika anaweza kufaulu. Siyo kwamba tunataka kuipatia Wizara pesa nyingi au cho chote kile. Tunachotaka ni kuwepo kwa sera ambazo zitatuwezesha sisi Waafrika wenyewe kuufufua uchumi wetu. Kulikuweko na sera moja ambayo ilizitaka Wizara za Serikali kuwapendelea Wafrika zinapotoa kandarasi, hata kama bei za bidhaa zao ziko juu kwa kiasi kidogo ya bidhaa za wageni. Bw. Naibu Spika, tulipoanzisha Kenya Industrial Estates (KIE), tulinuia kuwapendelea Wakenya. Kwa hivyo, ningependa Waziri afanye juhudi ya kuleta pamoja KIE na Export Processing Zones (EPZs). Waziri alikwenda Amerika akapata AGOA lakini ni nani anayefaidika na AGOA? Ninamwona mkubwa wa EPZs ambaye yuko hapa, na anasikiliza ninayoyasema. Ningependa tuziweke maanani shughuli za EPZs na KIE, ili tuweze kuendeleza uuzaji wa bidhaa zinazotengenezwa na mashirika hayo. Vile vile, tungependa Wizara hii ishirikiane na Wizara ya Kilimo kuona kwamba kilimo pia kinaimarishwa kwa sababu kilimo na biashara huenda sambamba. Tunataka kilimo kiimarishwe ndiyo tuendeleze ukuzaji wa pamba ambayo itatuwezesha kuviendeleza viwanda vya EPZ ili tupate faida. Kwa sasa, viwanda vya EPZ vinapeana ajira tu kwa Wakenya. Kila mara, tunasikia kwamba watu wetu wananyanyaswa. Bw. Naibu Spika, mwisho kabisa, ningependa kusema kwamba, tunapaswa kufahamu kwamba bila ya teknolojia hatutaweza kuendelea. Kwa hivyo, ningependa kuwashauri wafanyakazi katika mashamba makubwa ya majani chai nchini, ambao wanapinga matumizi ya vyombo vya kuvunia majani chai, wasilitilie mkazo jambo hilo. Tukilitilia jambo hili maanani sana, tutapoteza pesa nyingi sana tunazopata kutoka kwa mataifa yanayoipenda chai yetu. Kwa hayo machache, ninaiunga Hoja hii mkono."
}