GET /api/v0.1/hansard/entries/241380/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 241380,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/241380/?format=api",
    "text_counter": 226,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika, shukrani kwa kunipa nafasi hii nami nichangie kidogo Hoja hii juu ya Wizara ya Biashara na Viwanda. Kwanza, wacha nianze kwa kusema ya kwamba biashara haihusu tu wafanyabiashara July 25, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 2327 wakubwa, bali inahusu pia wafanyabiashara wadogo sana kama vile wachuuzi ambao naamini ya kwamba wana haki ya kuishi na kujitafutia mapato, lakini hawapewi nafasi hiyo na Wizara ya Serikali za Mitaa. Katika jiji hili la Nairobi na katika miji mingine mikubwa ya nchi yetu, kila baada ya siku chache utakuta kuna vita vikali kati ya askari wa mji, wakipambana na wachuuzi wakijaribu kuwakomesha wasifanye kile wanachofanya ndio waweze kuishi. Bw. Naibu Spika, sijui ni nani ambaye ana wajibu wa kutetea wafanyabiashara hawa wadogo. Sijui kama ni Waziri ambaye tunajadili bajeti ya Wizara yake au ni mhe. Kombo, lakini kwa kweli, huyo Mheshimiwa Mbunge amevuruga sana wafanyabiashara hawa wadogo. Amewavuruga sana na amewanyima usalama, na unashindwa hakuna pahali ambapo utakwenda na usikutane na hawa wachuuzi. Hakuna! Na unashindwa wachuuzi hawa tunataka kufanya nini nao? Tunataka kuwaua? Tunataka wafanye nini ndio tukubali ya kwamba wana haki ya kufanya hiyo biashara yao ndogo? Naamini ya kwamba hili ni swala nyeti, lakini muhimu na ambalo linastahili kushughulikiwa na Wizara hii ikishikiriana na ile Wizara ya Serikali za Mitaa. Sio haki kila siku tuwe tunalia shida hiyo hiyo bila ya kuitafutia utatuzi. Bw. Naibu Spika, pia ningetaka kusema ya kwamba tunaelewa ya kwamba biashara katika wakati huu inatawaliwa na moyo wa soko huria na kile kinachotajwa siku hizi kama utandawazi, lakini wengine wanasema ni \"utandawizi\". Ninaongea juu ya uwekezaji kutoka nje, na majuzi tu nilikuwa naongea na ujumbe mmoja kutoka Uchina na tukaingia katika mazungumzo juu ya utandawazi na namna tunavyoweza kujilinda kutokana na utandawazi ambao umegeuka na kuwa \"utandawizi\". Nilishangaa Wachina wakiniambia kwamba wamekubali kuwa na utandawazi katika uwanja wa biashara na soko huru. Hata hivyo, walisema hakuwezekani kuwa na soko huru katika siasa na utamaduni. Ukiangalia namna utamaduni wetu umeathiriwa na wageni kutoka nchi za magharibi, utashindwa ni biashara gani tunayofanya nao. Ikiwa leo wasichana watatembea uchi wa mnyama kule New York, kesho wanawake wetu watavua nguo na kutembea uchi. Ni huzuni tunaambiwa kwamba huu ndio utandawazi na biashara. Ni lazima Wizara hii itufafanulie kama biashara ni kuathiri utamaduni au siasa zetu. Kama Wachina, ni lazima tuhakikishe ya kwamba wakati tunakubali utandawazi katika uwanja wa biashara, tusiukubali katika tamaduni na siasa zetu. Tusipofanya hivyo, tutaingiliwa na ubeberu mpya na tunaweza hata tukatawaliwa tena na wakoloni. Bw. Naibu Spika, katika kukubali tuwe na wawekezaji kutoka nje, ni lazima tufahamu kuwa hawa si miungu. Tusiwaabudu wageni mradi tu wamekuja na pesa. Kama unadhani ninalitia jambo hili chumvi, kumbuka juzi watu wawili waliingia hapa nchini kwa kisingizio cha wawekezaji wa kigeni. Utashangaa ni akina nani waliowasujudia na kuwapigia magoti. Hii ni kwa sababu walikuwa na pesa. Hata shetani akaja hapa kesho akiwa na bunda la dola, utashangaa namna tutakavyomkimbilia na kumpigia magoti, tukimwambia tufanye biashara pamoja. Ni lazima tuwe waangalifu. Kuna wawekezaji na \"wawekezaji\". Wengine ni bandia, \"wawekezaji hewa\" na kadhalika. Sidhani tumesahau vile tulivyoathirika kutokana na \"uwekezaji hewa\" wa makampuni kama yale ya Anglo Leasing na Goldenberg. Hawa wote walikuwa ni \"wawekezaji hewa\", watu ambao wanaendeleza ufisadi badala ya kuwekeza rasilmali kutoka nje. Ni lazima Wizara hii iwe angalifu sana, kuchunguza ni akina nani wanaokuja nchini na jina hilo la uwekezaji. Ni lazima wawekezaji wote wapigwe darubini kwa sababu wengine ni wakora na wahuni. Lakini kwa sababu wana ngozi nyeupe na wanaongea Kiingereza, hatuwachunguzi hata kidogo, na wanaweza wakafanya chochote katika nchi hii. Hivi majuzi, mamluki wawilli tunaozungumza juu yao karibu wachukue nchi hii. Tulikuwa tunakutana nao barabarani na wanatusongeza kando wakisema: \"Kaeni kando, sisi ni wawekezaji.\" Lakini walikuwa ni mamluki! Kwa hivyo, Wizara hii ni lazima ifuatilie na ishikilie kwa dhati jukumu lake la kuhakikisha kwamba kila anayekuja kuwekeza hapa, amepigwa darubini na imehakikishwa ya kwamba ni mwekezaji halisi wala sio bandia. 2328 PARLIAMENTARY DEBATES July 25, 2006 Bw. Naibu Spika, jambo lingine ningetaka kusema ni kwamba kukubali uwekezaji kutoka nje hakumaanishi tusimiliki viwanda vyetu. Kuna watu ambao wanaamini kuwekeza ni kuwapa wageni uchumi wetu. Hakuna nchi ambayo inaweza kuhifadhi uhuru na uhai wake, ikiwa haitamiliki viwanda vyake. Ni lazima wananchi wawe na nafasi ya kumiliki viwanda vyao. Hatuwezi kuwapa wageni uchumi wetu wote ulivyo kwa jumla kwa sababu tupate ajira na tuukuze uchumi wetu. Hakuna nchi nyingine ambayo inaweza kufanya hivyo. Kuna viwanda vingine ambavyo tunaweza kuwaachia wageni kwa sababu hatuna uwezo wa kuviendesha. Lakini kiwanda chochote kile ambacho tuna uwezo wa kukiendesha, tusimpatie mgeni akimiliki au akisimamie. Bw. Naibu Spika, jambo lingine ningetaka kusema ni kwamba uwekezaji kutoka nje sio kufuga utumwa. Ninasema hivyo kwa sababu utakuta katika mashamba au viwanda vingine ambavyo vinashikiliwa na wageni, wageni wamekuwa watundu sana na wanawafanyia wafanyakazi wetu dhuluma ya aina yoyote ile, na hawana ulinzi. Wizara ya Leba ililala zamani na wafanyakazi hawana mtu wa kuwatetea viwandani na katika mashamba. Sasa, Wizara hii haiwezi kulala kama mwenziwe wa Leba, au sivyo wafanyakazi watakufa. Ni lazima ichukue jukumu, hata kama si jukumu lake, la kutetea wafanyakazi na kuhakikisha ya kwamba wanatendewa haki. Katika mashamba ya maua, ukienda pale na utazame mfanyakazi aliyeajiriwa kazi na umlinganishe na mwingine aliyeko mlangoni akitatufuta kazi, utakuta kuwa sura ya yule ambaye anatafuta kazi ni bora kuliko ile ya yule ambaye ameajiriwa. Unashindwa hii ni kazi ya aina gani? Watu wanafanywa watumwa! Wanapewa mishahara midogo. Wakiumia kwa madawa, hawalipwi chochote au kupewa madawa. Hili ni jambo la kushughulikiwa. Ukienda kwa mashamba ya maua na mikonge, utaaibika kama Mkenya. Hapa ningetaka kutofautiana na mhe. Makamu wa Rais kuhusu swala la mashamba ya majani chai. Mimi naamini, kama kuna watu 80,000 ambao watakosa kazi kwa sababu ya kutumia mashine hizo kuchuna majani chai, mashine hizo haziwezi kutufaa. Ni lazima, kabla ya kuziweka, tutafute---"
}