GET /api/v0.1/hansard/entries/242532/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 242532,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/242532/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Achuka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 353,
        "legal_name": "Francis Achuka Ewoton",
        "slug": "francis-ewoton"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Hoja hii ya Wizara ya Barabara na Ujenzi ni muhimu sana. Barabara ni maendeleo. Nataka kuongea juu ya barabara kutoka Kapenguria hadi Lodwar. Hali ya barabara hiyo ni ya kusikitisha sana. Barabara yenyewe ni ya kilomita 300. Wakati ilipojengwa, ungeweza kutumia masaa matatu kwa gari kutoka Lodwar hadi Kitale. Lakini sasa, unatumia masaa saba kutoka Lodwar hadi Kitale! Hali ya barabara hiyo ni mbaya sana. Watu wanatatizika sana. Sijui ikiwa Serikali inajua hali hiyo. Mimi mwenyewe nimelalamika juu ya barabara hiyo hapa Bungeni. Hata nilimtembelea Waziri wa Ujenzi na Barabara wakati huo, Bw. Raila. Yeye mwenyewe alikuja kwa helikopta mpaka Kainuk. Tulimwomba atoke kwa helikopta tutumie gari kusafiri. Tulitumia gari kutoka Kainuk hadi Lokichar! Yeye mwenyewe aliamua kuitisha helikopta kutoka Lodwar kuja kumchukua. Hangeweza kuendelea na safari hiyo kutokana na hali mbaya ya barabara. Bw. Naibu Spika wa Muda, hali hiyo ni kama janga kwa watu wa Turkana na Kitale. Ni tatizo kwa usalama pia. Wakati unasafiri, unataka uende kasi kidogo ili uhepe majambazi. Lakini kwa sababu barabara hiyo ni mbaya kuliko mtaro, huwezi kuendesha gari kwa mwendo wa kasi. Mara nyingi, tunasikia magari yamesimamishwa na watu kuibiwa mali yao! Hata wengine hupigwa risasi. Barabara hiyo imeharibika kabisa. Bw. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono ujenzi wa barabara. Tangu Serikali ya NARC ilipochukua uongozi, kinachoniridhisha mimi na pia Wakenya wenzangu ni Constituencies Development Fund (CDF). Ikiwa ujenzi wa barabara ungekuwa na mpangilio kama wa kama CDF, barabara nyingi zingejengwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, nimejaribu juu chini kuwashawishi watu wa Idara ya Ujenzi wa Barabara huko Lodwar kutengeneza barabara ndogo ndogo zinazopitia katika maeneo mengi huko vijijini, lakini wanasema ile tinga yao inayoitwa \" caterpillar \" imeharibika. Hakuna tinga katika kila wilaya. Kwa hivyo, naomba Bunge hili lihimize Serikali ipeleke maendeleo katika sehemu hizo. Wakati wa kura, Serikali iliahidi maendeleo katika sehemu zote za Kenya. Hata ikiwa pesa zimetengwa kwa miradi mingine, tunataka zitumiwe na kutumiwa kurekebisha barabara. Hata hapa Nairobi, wakati wa mvua, barabara nyingi zinakuwa lagha. Zinageuka kuwa 2140 PARLIAMENTARY DEBATES July 18, 2006 mito mikubwa. Hata wakati mwingine, maji husomba magari. Ikiwa tunataka kuendelea, lazima tuwe na mipango. Bw. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii kuhusu barabara. Nimetoa mawazo yangu mbele ya Serikali na Bunge hili. Lazima tufanye juu chini kuona kwamba barabara katika nchi hii zimerekebishwa. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}