GET /api/v0.1/hansard/entries/242559/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 242559,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/242559/?format=api",
    "text_counter": 230,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Ahsante Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa hii fursa kuzungumzia Hoja hii kuhusu Wizara ya Barabara na Ujenzi. Ningependa kusema kwamba wakati aliposoma Bajeti, mhe. Kimunya alitaja kuwa barabara ya Voi-Mwatate-Taveta ingeangaliwa. Ninashanga sana kwa sababu alitaja hayo siku ya Bajeti, lakini makadirio ya Serikali yana pesa haba sana kwa barabara hii. Katika barabara za kiwango cha \"A\" nchini mwote barabara hii ndiyo \"imeonewa\" zaidi. Itakuaje barabara ya kiwango \"A\" itengewe Kshs4 million pekee. Je, tutatumiaje shs4 million kujenga barabara hiyo? Nasikitika sana kwa sababu, mwaka jana tulipatiwa Kshs68 million kuifanyia barabara hii usorovea na utafiti, lakini pesa hizo hizikutumika. Wakati huu, Mhe. Kimunya ameamua kuwa barabara hiyo haistahili kutengewa pesa za kuifanyia usorovea. Jambo la ajabu ni kwamba katika Mkoa wa Pwani mzima Wilaya ya Taita-Taveta ndio \"imeonewa\" katika Bajeti ya Wizara ya Barabara na Ujenzi. Wilaya ya Malindi pia \"imeonewa\" kwa kupewa Kshs7 million pekee. Ajabu ni kuwa Wilaya ya Taita-Taveta, ninakotoka mimi, kuna ukuzaji wa chakula kingi. Tunalisha Mkoa wa Pwani wote, lakini Serikali ya NARC inaona kuwa watu wa Taita- Taveta hawafai kusadiwa. Jambo lingine la kustaajabisha ni kuwa Mawaziri wamejigawia pesa za Serikali wanavyotaka. Mhe. Kimunya alisafiri kwa barabara hadi Wilaya ya Taita-Taveta na alishuhudia vile barabara zetu zilivyo mbaya. Nilipomwona afisini mwake aliniambia: \"Mhe. Shaban ninakumbuka vile barabara za Taita-Taveta zilivyo mbaya\". Ajabu ni kuwa sijui kama Kshs4 million zinaonyesha kuikumbuka Taita-Taveta au kuidharau. Labda Mhe. Nyachae hajakanyanga Wilaya ya Taita-Taveta na hajui vile barabara zilivyo huko, na kuwa zinahitaji pesa. Ningependa kutaja kuwa barabara zilizopendelewa ni zilizo sehemu zinazowakilishwa na mawaziri. Masikini mhe, Konchella hakufikiriwa; hakupewa chochote. Ningependa kutaja barabara zilizopendelewa. Kiasi cha Kshs515 million zimetengewa Wilaya ya Maragua, anakotoka naibu wa Waziri, Bw. Toro. Kiasi cha Kshs264 million zimetengewa Kangema, anakotoka mhe. Michuki, hali Kshs956 million zimetengewa Nyandarua, anakotoka mhe. Kimunya. Pia Kshs845 zimetengewa eneo la Kisii, anakotoka mhe. Nyachae. Nasikitika sana kuwa Kshs369 million zimetengewa Gatanga, anakotoka mhe. Kenneth. Vile vile, Kshs415 million zimetengewa Rarieda kwa mhe Tuju. Pia shs265 million zimetegewa July 18, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 2149 Busia, anakotoka Makamu wa Rais, Bw. Awori. Pia Kshs785 million zimetengewa Wilaya ya Nyeri. Ni lazima uwe waziri ndipo upewe pesa. Nasikitika kuwa watu wa Taita-Taveta wanateseka ingawa hulisha Mkoa mzima wa Pwani. Kwa nini hii Serikali \"inatuonea\" hivyo? Kwa nini tumeonewa tangu Uhuru hadi sasa? Nimesimama hapa kwa uchungu na masikitiko makubwa. Kumbe tunahitaji kuwa Serikalini ndipo tukumbukwe! Bunge hili sisi husikia katika Mawaziri wakidai kuwa Serikali yao ni tofauti na ili ilikuwa ya KANU. Lakini ninawauliza: Tofauti iko wapi? Ninasikitika sana kuhusu jambo hili. Hata nilimuuliza mhe. Kimunya ni kwa nini aliizungumza juu ya barabara za Voi-Taveta-Mwatate katika Bajeti na huku akaondoa Kshs68 zilizokuwa zimetengewa mwaka jana. Maskini watu wa Taita-Taveta, nani atawahurumia? Ninapendekeza makadirio ya pesa za Serikali yafanywe upya ili watu wote wafanyiwe usawa. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}