GET /api/v0.1/hansard/entries/242565/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 242565,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/242565/?format=api",
"text_counter": 236,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Shakombo",
"speaker_title": "The Minister of State for National Heritage",
"speaker": {
"id": 244,
"legal_name": "Rashid Suleiman Shakombo",
"slug": "rashid-shakombo"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, mimi nilikuwa Mkuu wa Wilaya katika wilaya anayotoka mhe. Kipchumba. I will refer tothe road later on. Jambo ambalo ningependa kumkumbusha Waziri na maofisa wake ni kwamba katika Mkoa wa Pwani biashara ya utalii ni takriban asilimia 60 ya biashara zote zinazofanywa huko. Watalii hutalii eneo la pwani sana ijapokuwa zile barabara muhimu ambazo wanatumia hawa watalii zimesahauliwa. Hazikutajwa kabisa katika bajeti ya Wizara hii. Barabara muhimu iliyotajwa peke yake ni ile inayotoka Maji ya Chumvi kuelekea Miritini. Kule Mombasa, kuna barabara inayotoka Likoni Ferry kuelekea Kombani. Utashangaa sana kusikia kwamba kukinyesha mvua kidogo tu, hata matatu haziwezi kuitumia barabara hii. Lazima pawe na watu wa kuzisukuma ndipo ziende. Hii ni barabara inayotumiwa na watalii sana. Aidha inaunganisha Kenya na Tanzania. Sijui ni kwa nini imesahaulika. Barabara nyingine ni ile inayoitwa Dongokundu Bypass. Hii barabara ikitengenezwa, itafanya usafiri kutoka Mombasa hadi Tanzania kuwa rahisi mno. Vile vile itawawezesha wenye viwanda kutoka sehemu ya kisiwani kwenda huko eneo la kusini ya pwani. Wao wanaogopa kwenda kule kwa sababu ya kucheleweshwa na kwa kuwa ni ghali kusafiria feri. Barabara hii itaweza kupunguza msongamano wa magari katika mji wa Mombasa. Sijui ni kwa nini barabara hii imesahaulika. Isitoshe, Bw. Naibu Spika wa Muda, tumekuwa tukizungumza jinsi tutakavyoifanya bandari yetu kuwa huru. Huko katika Bandari ya Mombasa kuna zaidi ya ekari 3,000 za KPA ambazo huenda zikafanywa bandari huru. Hili ni jambo ambalo huenda lisifanyike kwa sababu 2150 PARLIAMENTARY DEBATES July 18, 2006 Dongokundu Bypass imesahaulika. Katika sehemu hiyo ya Dongokundu, tunatarajia kujenga makao makuu ya wilaya mpya inayoitwa Kilindini. Makao haya makuu yatakuwa yanatoa huduma kwa watu wa Likoni na Changamwe. Bila ya barabara hii, hatutaweza kuwasaidia watu wa sehemu hii. Barabara nyingine muhimu katika utalii ni hiyo inayotoka Mariakani kupitia Kaloleni hadi Malindi. Aidha, ile barabara ya Mombasa-Malindi hutumiwa sana na watalii wanaozuru Mkoa wa Pwani. Tunafahamu kuwa, Malindi, katika pwani ya kaskazini, ndiyo sehemu iliyo na hoteli kubwa za kisasa duniani. Hoteli hizo ndizo zinatembelewa sana na watalii. Sijui ni kwa nini Wizara inayohusika na barabara imeisahau barabara hii. Barabara ya Mariakani-Kinango husaidia sana katika usafirishaji wa matunda kama vile machungwa na ndizi. Barabara nyingine ambazo zimesahauliwa ni Kwale-Kakuneni-Mamba- Ramisi na Kwale-Kinango-Lungalunga. Barabara hizi nilizotaja zisipotengenezwa, hatutakuwa tumesaidia watu wa Mkoa wa Pwani vilivyo. Hatutaweza kamwe kuvutia hii biashara ya utalii ambayo tunasema ni muhimu kwa nchi yetu. Sehemu zile ambazo zinakuza michungwa pia zimesahaulika. Si ukweli kwamba barabara zinazoelekea kwa maboma ya Mawaziri ndizo zimetengenezwa. Barabara ya Mariakani-Kaloleni- Malindi inapatikana katika eneo analowakilisha mhe. Dzoro. Ile nyingine ya Likoni Feri-Kombani- Lungalunga inapatikana katika mawakilisho yao waheshimiwa Shakombo na Mwakwere. Ingawa hivyo, barabara hii bado haijatengenezwa. Tusiseme kwamba Mawaziri wanapendeleana. Ni muhimu tuzitaje zile shida ambazo tuko nazo. Nina hakika kwamba Waziri na maofisa wake watatusikiliza kwa sababu kughafilika ni hali ya binadamu. Ikiwa mtu amesahau kufanya hili ama lile basi tukumbushane; hakuna haja ya vita. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, ningependa kuunga mkono Hoja hii."
}