GET /api/v0.1/hansard/entries/242937/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 242937,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/242937/?format=api",
"text_counter": 21,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, ukweli wa mambo ni kwamba wageni wa kila aina wameingilia idhaa zetu za utangazaji. Wamarekani wamefanya hivyo. Vipindi vingi vinatoka Marekani na Uingereza. Nao Wachina wameingilia soko hili. Nadhani tatizo lililoko ni kwamba bado hatujafanya mabadiliko ya kutuwezesha kuwa na vipindi vyetu wenyewe ambavyo vitatetea utamaduni wetu na kuwatolea watu wetu elimu ambayo tumeipanga sisi wenyewe. Ni kweli kuwa katika upande wa runinga, Wachina wanatumia idhaa ya Serikali, lakini wamepewa masafa katika redio. Nadhani kuwa jawabu la swali hili lingekuwa ni kusahihisha kutoka upande wetu kuliko kutaka kupewa nafasi hiyo huko Beijing. Lakini iwapo Wachina watasema wako tayari kutupatia nafasi ya kutumia idhaa yao ya Serikali ya runinga, tutasema \"Hewala\". Natumai kuwa watasikiza mambo yaliyozungumziwa hapa Bungeni leo."
}