GET /api/v0.1/hansard/entries/243389/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 243389,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/243389/?format=api",
    "text_counter": 221,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Awori",
    "speaker_title": "The Vice-President and Minister for Home Affairs",
    "speaker": {
        "id": 290,
        "legal_name": "Moody Arthur Awori",
        "slug": "moody-awori"
    },
    "content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Bunge lina majukumu makubwa. Jukumu lake la kwanza ni kutunga sheria ambazo zitaiwezesha Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi. Jukumu lake la pili ni kutoa mwongozo utakaotumiwa na viongozi ili nchi hii iweze kupata manufaa. Jukumu la tatu ni kujadiliana jinsi mapato ya Serikali yatakavyotumiwa. Bunge huhakikisha kwamba kila mwananchi anapata huduma kutoka kwa Serikali. Bunge hili sharti lielezwe jinsi pesa hizo zinavyotumika. Waziri akiwasilisha maombi yake ya pesa humu Bungeni, yeye huwa anawakilisha Serikali kupitia Wizara yake. Wakati Waziri alipoomba apewe Kshs29 bilioni, hakufanya hivyo eti kwa sababu yeye binafsi anataka kuzitumia pesa hizo. Yeye analiomba Bunge limpe idhini ya kutumia hizi pesa kuendesha shughuli za Serikali. Kwa hivyo, jukumu la Wabunge ni kuhakikisha kwamba pesa hizo zimepeanwa ndiposa Serikali iweze kuendeleza kazi yake. Tunapopewa nafasi kujadili Hoja hii, haimaanishi eti tumepewa nafasi kuwajadili watu binafsi. Tukifanya hivyo, tutakuwa tumepotea njia. Jana nilihuzunishwa sana na hotuba za Wabunge fulani hapa Bungeni. Wabunge kadhaa hawakutaka hata kumwona Waziri alipokuwa akitoa Hoja hii. Sheria za Bunge hili zilipuuzwa hata ikakulazimu wewe, Bw. Naibu Spika wa Muda, kuingilia kati swala hilo ndiposa wakampa Waziri nafasi ya kutoa maoni yake. Kulikuwa na jaribio la kuangamiza hotuba yake. Kelele zilipigwa humu ndani na Waziri akatupiwa matusi. HANSARD inaonyesha wazi matusi hayo. Kwa nini tunaleta chuki ndani ya Bunge hili? Hili ni Bunge la heshima na ndio sababu sisi tunaitwa waheshimiwa. Inampasa mheshimiwa Mbunge yeyote kusikiliza maoni ya wenzake. Waziri hakuwa anatoa maoni yake; alikuwa anawakilisha Wizara yake alipokuwa akitoa Hoja kwamba anahitaji pesa za kumwezesha kufanya kazi yake. Haya yote yakitendeka jana, watoto wa shule walikuwa humu ndani wakishuhudia. Kwa nini watoto hutoka shuleni kwao kuja hapa Bungeni kusikiliza hotuba zetu? Ni kwa sababu wanajua kuwa sisi ni Wabunge waheshimiwa na wangependa sana kuiga mfano wetu. Je, ni mfano gani ambao sisi tulionyesha jana? Hata kulikuwa na Mbunge mmoja ambaye alisema kuwa Bunge litakataa kuidhinisha hilo ombi la Kshs29 bilioni. Ikiwa ombi hili litakataliwa, na Wabunge wanatarajia hali ya usalama iimarishwe, je, usalama huo utatoka wapi? Ni muhimu tutupilie mbali fikira zetu za kibinafsi juu ya Mawaziri wa Serikali. Ni kweli kwamba Serikali yetu imejaribu kufanya mambo mengi na hii Wizara imekuwa ikifanya kazi vema. Usalama unadumishwa humu nchini. Hakuna nchi yoyote katika dunia ambayo inaweza kudai kuwa imedumisha usalama kote. Mara nyingi tunasikia habari za ufisadi. Mimi ningependa kujua tuna malaika wangapi humu Bungeni ambao hawana dhambi. Hili ni jambo ambalo inatupasa tulichunguze ili tujue ukweli wake. Ni lazima tuheshimiane. Wakati huu tunahitaji pesa sana ili polisi wetu waweze 2044 PARLIAMENTARY DEBATES July 12, 2006 kufanya kazi yao vema. Tunataka kuangalia maslahi yao; kwa mfano, tunataka kuwajengea nyumba na kuwapa vifaa vya kazi kama vile motokaa, redio na kadhalika. Bw. Naibu Spika wa Muda, wakati huu magereza yetu yamesongamana sana. Sisi tunataka kutumia hizi pesa kuwafundisha polisi sheria ili waelewe kwamba hawawezi kuwashika watu kiholela na kuwatupa korokoroni. Tunahitaji pesa ili vituo vya polisi viweze kuwa na korokoro. Magereza yote nchini yana watu takribani 52,000. Kati ya hawa, wafungwa ni 20,000 peke yake. Waliobakia ni watuhumiwa tu. Hawa watuhumiwa, ikiwa polisi wangekuwa wamefundishwa kazi yao vilivyo, wangepatiwa dhamana. Tukifanya hivyo, tutaweza kupunguza idadi ya wafungwa magerezani. Kwa nini basi hatuwezi kuondoa hisia za kibinafsi katika haya mambo yanayotukabili? Bw. Naibu Spika wa Muda ile dhana ya jamii kushirikiana na polisi katika kuangamiza uhalifu imesaidia sana katika kupunguza uhalifu nchini. Sasa tunataka kuzipa jamii zetu vifaa ambavyo vitawezesha udumishaji wa amani humu nchini. Tunataka pesa za kuwanunulia vifaa kama vile pikipiki ambazo zitawawezesha kushika doria vilivyo. Ofisi ya Rais ndio inasimamia idara ya uchapishaji wa makala ya Serikali. Ingekuwa bora ikiwa idara hii ingefanywa kuwa shirika la Serikali ili iweze kutenda kazi yake bila kuingiliwa na idara nyingine. Mambo mengi ambayo yanagusiwa katika magazeti yetu hakika si mambo ya kuleta maendeleo. Ni mambo ambayo yanalenga kuwafurahisha watu fulani. Wakati umewadia sasa wa Serikali kutumia pesa zake katika shughuli za kunufaisha magazeti ya Serikali, likiwemo gazeti rasmi la Serikali. Ni maoni yangu kuwa tunaweza sasa kuiondoa idara inayohusika na uthibiti wa matumizi ya madawa ya kulevya (NACADA) katika Ofisi ya Rais na kuipeleka katika Wizara ya Jinsia, Michezo, Tamaduni na Maswala ya Kijamii. Matumizi ya madawa ya kulevya na unywaji pombe ni maswala ya kijamii na inatupasa sisi katika jamii kupunguza tabia hizi. Tunatarajia kubadilisha mambo ili maadili yetu ya zamani ya kuheshimu maisha yaweze kutiliwa maanani. Bw. Naibu Spika wa Muda, tunatakikana kuongeza pesa ambazo Wizara hii inahitaji. Kuna idara nyingi katika Ofisi ya Rais na Kshs29 bilioni hazitoshi. Kule mashinani kuna machifu wasaidizi. Tunataka kuwapanulia barabara kule mashinani ili waweze kuzuru kila sehemu kuwasaidia wananchi. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, naomba kuunga mkono Hoja hii."
}