GET /api/v0.1/hansard/entries/243446/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 243446,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/243446/?format=api",
    "text_counter": 278,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kingi",
    "speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
    "speaker": {
        "id": 27,
        "legal_name": "Amason Jeffah Kingi",
        "slug": "amason-kingi"
    },
    "content": " Asanti Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii, ili nizungumze machache kuhusu Hoja iliyo mbele yetu. Kabla sijafanya hivyo, nataka kuomba radhi kwa sababu asubuhi ya leo, hatungeweza kuyajibu Maswali yetu ya Bunge. Hii ni kwa sababu tulikuwa katika mkutano ambao tuliuitisha ili tujadili ripoti iliyosema kwamba Ofisi ya Raisi imekumbwa na ufisadi. Tulipokuwa katika mkutano huo, tulijichunguza. Ningependa kuhakikishia Bunge kwamba tutafanya jambo ambalo linafaa kufanywa ili kuiondoa sura hiyo mbaya ambayo ilitangazwa. Tutafanya jambo lolote tuwezalo katika Ofisi yetu, ili kuhakikisha kwamba tunatoa huduma kwa wananchi vile inavyopaswa. Jambo moja ambalo limezungumziwa sana ni lile la ufisadi. Nataka kulizungumzia, pengine nikiangalia upande mwingine. Ufisadi tunaouzungumzia wahusu utumiaji mbaya wa fedha na mali ya Serikali. Lakini pia, kuna ufisadi mwingine ambao ni mbaya zaidi, pengine kuliko ule wa kutumia fedha za umma vibaya. Tunapokuja kwa Bunge hili na kuzungumzia maswala muhimu kama vile Urekebishaji wa Katiba, tunatoa maoni yetu kuhusu swala kama vile utawala wa mikoa. Wengine wetu tumeshasema kwamba mfumo wa utawala wa mikoa ni mbaya sana na haufai. Inafaa tufuatilie jambo hilo zaidi mpaka tutakapoandika Katiba mpya, ili tuondoe utawala wa mikoa. Wengine wetu ambao tulisema utawala huo ni mbaya, tulitoka nje na kuwaambia wananchi na maofisa wa utawala wa mikoa kwamba wakatae Katiba Kielelezo kwa sababu wakiikubali wataachishwa kazi. Kama huo si ufisadi mbaya, nahitaji kuelezwa ufisadi ni nini. Tumezungumzia mambo ya Wilaya. Tunachofanya katika Ofisi yetu leo ni kuhalalisha wilaya zilizoundwa wakati wa Serikali iliyopita. Pia, wakati huo huo, tulikuwa tukiwapa wananchi ambao hawakupata, wilaya mpya na wanazihitaji ili tuhakikishe kwamba wanapata huduma karibu nao. Tunapokaa katika Ofisi yetu, tunapata maoni kutoka kwa wananchi kila siku, na ripoti kutoka watawala wetu wa mikoa na maoni mengi kutokana na mikutano mingi ambayo wananchi wanahudhuria. Katika ripoti hizo zote, tunaona ya kwamba wananchi wanataka wilaya mpya ili wapate wakuu wa wilaya na huduma ziwe karibu nao. Hatujapata ripoti yoyote kutoka sehemu yoyote ambapo wananchi wanakataa Wilaya yao na kusema ivunjwe ili iwe pamoja na nyingine, lakini tunapata ripoti za kuunda wilaya mpya ili huduma ziwe karibu na wananchi. Tunapokuja katika Bunge hili, tunawakilisha wananchi. Ikiwa wananchi hao ndio wanaosema wanataka wilaya mpya halafu tukija hapa tunasema hatutaki wilaya mpya, siwezi kujua tunawakilisha nani kwa sababu wananchi wanataka wilaya mpaya. Uhalifu ni kutu kibaya na adui mkubwa na usalama. Hiyo ndio sababu tunafaa kuunga mkono Hoja hii ili Serikali ipate pesa za kuimarisha usalama katika Taifa hili. Tunafaa kuimarisha usalama ili shule zetu ziendeleze kazi zao vizuri na watu wetu wapate huduma bila shida. Ukiangalia kiwango cha askari sambamba na idadi ya wananchi, utaona yakwamba askari mmoja hulinda watu 1,150. Askari mmoja anawezaje kulinda idadi kubwa hivyo ya wananchi? Itawezekanaje afisa mmoja atoe usalama kwa Wakenya wengi namna hiyo? Tunataka tuongeze idadi ya maafisa wa polisi, tuwape elimu bora ili tuhakikishe wanafanya kazi yao vizuri. Kufanya hivyo kunahitaji pesa ili tupanue vyuo vinavyotumiwa kuwapa mafunzo askari wetu. Tutaweza pia kuwapatia nyumba nzuri ili waache kulala watu wanne au watano katika nyumba moja. Hao pia ni maafisa wanaotaka kuheshimiwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, hivi juzi, tulianza mfumo wa community policing . Pale wananchi wamezingatia mfumo huo, hasa upande wa Magharibi mwa Kenya, matokeo yake ni mazuri. Uhalifu umepungua sana. Kwa hivyo, tunataka kuwauliza wale ambao hawajazingatia 2054 PARLIAMENTARY DEBATES July 12, 2006 mfumo huo, wafanye hivyo ili tuweze kuimarisha usalama katika sehemu tunazotoka. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii."
}