HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 243935,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/243935/?format=api",
"text_counter": 261,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Karume",
"speaker_title": "The Minister of State for Defence",
"speaker": {
"id": 234,
"legal_name": "Njenga Karume",
"slug": "njenga-karume"
},
"content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nitoe maoni yangu. Naunga mkono mambo haya yote kwa sababu nikiangalia kazi inayofanywa na Wizara hiyo, pengine wamepewa pesa kidogo kwa sababu tunajua kuwa kuna upungufu wa pesa katika Serikali yetu. La sivyo, tunajua kuwa wangepewa pesa nyingi zaidi kuliko hizo walizopewa. Bw. Naibu Spika wa Muda, ukiangalia kwa makini, utaona kwamba ile kazi inayofanywa na Wizara hii ni ya maana sana. Kuanzia vijijini wanakoishi wananchi wa kawaida, hapo mbeleni, kulikuweko na malalamishi mengi sana. Unywaji chang'aa ulikuwa umeenea kila mahali. Watu walikufa kwa kunywa chang'aa kupindukia, na kwa njia zingine nyingi kwa sababu machifu hawakuwa na nidhamu. Hawakuwa wakizingatia mambo hayo. Shughuli waliyokuwa wakifanya zaidi ilikuwa kunywa pombe na kupokea hongo. Hivi sasa, ukiwauliza akina mama hali ilivyo kule vijijini, watakwambia kwamba Serikali imewasaidia sana. Hata wale mabwana ambao hawakuwa wakirudi makwao kwa sababu ya kunywa chang'aa kupindukia, wakati huu hufika nyumbani mapema. Wanaweza hata kula chakula kwa sababu hawanywi chang'aa kupindukia. Huo ndio ukweli. Viongozi wanafanya mikutano mara kwa mara katika sehemu wanazowakilisha Bungeni. Zamani, hata mikutano haingeweza kufanyika vizuri kwa sababu ya ulevi wa chang'aa . Bw. Naibu Spika wa Muda, kufuatia juhudi ya Serikali ya kuleta nidhamu miongoni mwa machifu na polisi, hali ya usalama nchini imeimarika. Ni vigumu kumaliza uhalifu kabisa, lakini ukilinganisha hali ya usalama wakati huu na wakati uliopita, utaona kwamba hali hiyo imeimarika kwa kiasi kikubwa. Tunafahamu kwamba bado watu wanauawa na kuibiwa. Hata hivyo, ukiwauliza wananchi kuhusu hali ya usalama nchini kwa jumla, watakwambia kwamba, ingawaje hali hiyo haijaimarika kikamilifu, visa vya uhalifu nchini vimepungua maradufu. Kwa hivyo, ni bora tuseme ukweli, kama kazi nzuri imefanywa. Hivyo basi, ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeza Waziri mwenzangu anayehusika na maswala ya usalama kwa kazi nzuri aliyofanya, akishirikiana na maafisa wake. Ninawaomba Wabunge wenzangu waangalie kwa makini ili waweze kuona maendeleo yaliyopatikana katika sekta ya usalama. Ukilinganisha hali ilivyokuwa hapo awali na hali ilivyo sasa katika Utawala wa Mikoani, utaona kwamba kuna madiliko makubwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, hata wananchi wanafurahia jinsi Serikali ya NARC July 11, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 1963 inavyofanya kazi. Wakulima katika sekta zote hulipwa marupurupu yao kwa wakati unaofaa. Shughuli katika sekta ya utalii pia zimeimarika. Kama mnavyojua, sekta ya utalii ilikuwa imesambaratika. Wageni kutoka nchi za nje hawakuwa wakiitembelea nchi hii kwa sababu hali ya usalama ilikuwa mbaya sana. Wabunge wenzangu watakumbuka kwamba hoteli nyingi katika sehemu za pwani za nchi hii zilikuwa zimefungwa. Wafanyikazi katika hoteli hizo walifutwa. Lakini wakati huu, hoteli zimejaa wageni. Hoteli zingine zimepanuliwa. Hoteli mpya zimejengwa nchini na watu wanapata ajira. Hilo ni thibitisho kwamba hali ya usalama nchini imeimarika. Kama hali ya usalama ingekuwa mbaya kama zamani, hakungekuwepo na maendeleo kama hayo. Wageni hawangefurahia kuizuru nchi hii. Kwa hivyo, ni bora tufurahie hatua tuliyopiga katika kuimarisha hali ya usalama humu nchini. Bw. Naibu Spika wa Muda, wale Wabunge wanaosema kwamba hawataiunga mkono bajeti ya Wizara hii wanakosea, kwa sababu, pesa hizi zitatumiwa kutoa huduma kwa wananchi. Waziri na maafisa wake hawatazitumia pesa hizi kwa mahitaji yao ya kibinafsi. Kama tunavyojua, Serikali ya NARC haijali ni mfuasi wa chama gani au mtu kutoka jamii gani atakayefaidika na pesa hizi. Wanaofaidika na mpango wa elimu ya bure nchini ni watoto wote wa Kenya. Serikali haiwabagui watoto kwa misingi ya kikabila au kisiasa. Sisi hatusemi eti eneo fulani la uwakilishi Bungeni lisifaidike na hazina ya CDF kwa sababu wakazi katika sehemu hiyo wanaipinga Serikali. Hiyo inaonyesha kwamba Serikali hii inatoa huduma nchini kote bila mapendeleo. Bw. Naibu Spika wa Muda, hapo zamani, hata mtu angejua kwamba kijana fulani mtaani alikuwa mwizi, hakuthubutu kwenda kupiga ripoti katika kituo cha polisi. Wale waliothubutu kufanya hivyo walikuwa wakihangaishwa na wahalifu. Nyakati hizo, ungetoa ripoti juu ya mhalifu fulani kwa polisi, siku ya pili ungeulizwa na mhalifu huyo: \"Jana ulienda kufanya nini katika kituo cha polisi?\" Hiyo ni kwa sababu wakati huo, hapakuwa na nidhamu miongoni mwa maafisa wa polisi. Sasa kuna urafiki na ushirikiano kati ya polisi na wananchi. Hata idara zingine katika Afisi ya Rais zimeimarisha hali ya uwajibikaji katika utoaji wa huduma kwa umma. Zamani watu walikuwa wakifikiri kwamba wanajeshi wetu hulinda mipaka ya nchi yetu peke yake. Lakini wakati huu ukiangalia, utaona kwamba wanajeshi wetu pia hufanya shughuli za ujenzi wa taifa. Kwa mfano, kufikia sasa, katika Wilaya ya Pokot Magharibi, wanajeshi wamechimba visima 14 na mabwawa 13 ya maji. Idara ya Ulinzi pia imewajengea wakazi wa wilaya hiyo zaidi ya shule 60. Tunafanya hivyo kwa sababu tunawatambua wakazi wa sehemu hiyo kuwa Wakenya. Bw. Naibu Spika wa Muda, Idara ya Ulinzi inataka kuongeza idadi ya vifaa vya kuchimbia visima katika Mkoa wa Kaskazini Mashariki na pia kutengeneza barabara, licha ya kuweko kwa Wizara ya Maji na Unyunyizaji Mashamba na Wizara ya Barabara na Ujenzi. Kwa hivyo, utaona kwamba Serikali inafanya kazi ya maana sana kwa wakati huu. Kwa hivyo, ningependa kuwaomba ndugu zangu katika Bunge hili waache kuibinafsisha bajeti hii, na badala yake wazingatie shughuli za maendeleo zitakazofanywa kutumia pesa hizi. Kwa hivyo, ningependa kuiunga mkono Hoja hii na kuwaomba Wabunge wenzangu wafanye hivyo ili tuweze kujadili bajeti za wizara zingine, ili wananchi waweze kupata huduma. Bw. Naibu Spika wa Muda, nikitamatisha mchango wangu kwa Hoja hii, ningependa kumkumbusha Waziri wa Haki na Sheria, ambaye anasimamia vita dhidi ya ufisadi, jambo fulani: Uchochezi na kunyakua mali ya watu wengine kwa mabavu husababisha vita na mauaji. Kuna watu fulani katika nchi hii ambao wamezoea kulisha mifugo yao katika mashamba ya watu wengine bila ya ruhusa ya wenye mashamba hayo. Watu hao huwa hawataki kuulizwa ni kwa nini wao hufanya hivyo. Kama tunavyojua, katika nchi hii, kila mtu ana mali yake. Kwa hivyo, ningependa Waziri alizingatie jambo hilo. Ukienda katika sehemu ya Naivasha, ukielekea Nakuru na Gilgil, utaona ng'ombe wanalishwa katika mashamba ya watu binafsi. Inafaa kila mtu akae kwake. Katika nchi hii, hakuna mtu ambaye ana nguvu zaidi ya sheria ya nchi. 1964 PARLIAMENTARY DEBATES July 11, 2006 Ukivunja sheria, haijalishi kama wewe ni Mbunge au Waziri; inafaa uchukuliwe hatua ya kisheria. Kwa hivyo, mtu akiwachochea wananchi waanzishe vita ili wauane, inafaa achukuliwe hatua ya kisheria, kwa sababu Katiba ya nchi hii inawahudumia Wakenya wote bila ya ubaguzi. Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii."
}