GET /api/v0.1/hansard/entries/243947/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 243947,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/243947/?format=api",
    "text_counter": 273,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ninachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyeniwezesha kusimama hapa kuchangia Hoja iliyo mbele yetu. Sehemu ninayowakilisha hapa Bungeni ya Bura iko na kata 12, kata dogo 25 na tarafa tatu. Kati ya kata 12, inne ambazo ziko karibu na barabara ziko na kambi ya chifu, Mkuu wa Tarafa (DO) na zinaendelea vizuri. Kata nane hazina hata askari mmoja. Chifu peke yake ndiyo yuko huko. Niliuliza Swali katika Bunge hili na nikamjulisha Waziri anayehusika kwamba kata nane za Bura hazina hata bendera ya taifa. Hivyo basi, mtoto ambaye alizaliwa 1991 hajawahi kuona bendera ya Kenya. Ukimuuliza yule mtoto ni mwananchi wa kutoka wapi na akwambie yeye ni wa kutoka Somalia, atakuwa na hatia yoyote? Sisi tuko na matatizo mengi. Bw. Naibu Spika wa Muda, zamani, Bunge, Utawala na Mahakama zilikuwa zinashirikiana kuendesha shughuli ya ujenzi wa taifa. Leo, tunasikitika! Utasema maneno ndani ya hili Bunge, uadhini na upige filimbi, lakini mambo yatabaki vile vile. Kusema nitasema kwa sababu huu ni wajibu wangu. Nikisikilizwa au nisiposikilizwa, wajibu wangu nikutekeleza mambo kwa kusema. Kata za Balabala, Bua, Saka, Sala, Nanigi, Chewele na Hilimani hazina hata bendera ya taifa. Iwapo Serikali imefilisika, Waziri anafaa kutuambia. Ukienda Tarafa ya Madogo, utaona kuwa ofisi ya DO iko hospitalini. Akina mama kwetu wanaona haya sana kujifungua kwa sababu DO anakaa na baraza lake la wananchi karibu na chumba chao cha kujifungulia. Hii ni dhuluma! DO hana nyumba ya kulala wala ofisi. Mr. Naibu Spika wa Muda, niliongea kuhusu jambo hili hapa Bungeni miaka minne iliyopita na nikauliza Swali kuhusu swala hili lakini hakuna kitu ambacho kimefanyika. Bw. Naibu Spika wa Muda, angalia Kamati ya Wilaya ya Usalama na utapata kwamba sehemu ninapotoka ni sehemu ya usalama ama utata. Leo shifta wametuvamia na kesho balaa fulani imezuka. Kisha angalia wanakamati wa Kamati ya Wilaya ya Usalama na utapata kwamba Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Polisi na Ofisa wa upelelezi wanatoka sehemu zingine. Wote katika orodha hii ni watu waliokuja kufanya kazi ya mshahara. Baada ya mwaka mmoja au miaka miwili wanaenda zao. Sisi ni wazaliwa. Nikisema hivi sio lazima mimi Ali Wario Mbunge niwe katika kamati hii. Viongozi wa mashinani na sehemu hiyo wanapaswa kuhusishwa kwa sababu wanajua ni sehemu gani ina tisho na ni sehemu gani nzuri ambayo Serikali ijulishwe mapema waweze kuingilia. Lakini ukimwambia Mkuu wa Wilaya kwangu kumevamiwa atakuuliza njia yake iko wapi. Ni lini maswala hayo yatajibiwa? Wakati umefikia ambapo ulimwengu umetoka katika ule utawala wa kuteremsha maswala kutoka juu hadi mashinani. Maswala ni kutoka mashinani yaende juu, hivyo, basi ni vizuri watu wahusishwe. Viongozi na wananchi wahusishwe ili watoe maoni yao kwa kamati hii. Ni kweli hatuhusishwi katika maswala ya usalama lakini katika sakata ya Anglo Leasing licha ya maswala 1970 PARLIAMENTARY DEBATES July 11, 2006 ya usalama mabilioni ya pesa zimeibiwa na sisi Wabunge maskini tukienda tunaambiwa haya ni maswali ya usalama na basi bahati mbaya wewe hutakuwa hapa. Mimi ndiye naiongoza sehemu hii. Mimi ni mwananchi na tangu kuzaliwa ninaishi hapa. Nani anajua usalama wa sehemu hii kushinda mimi? Ni Mkuu wa Wilaya ama Mkuu wa Tarafa aliyekuja juzi? Ni wakati wa Serikali kuangalia maswala haya na ikiwezekana wabadilishe sera hiyo. Bw. Naibu Spika wa Muda, majuzi tulipoenda katika kura ya maoni, chifu wetu waliahidiwa ahadi kubwa kwamba wataongezewa mishahara. Hata mimi niliuliza ndani ya hii Bunge juu ya hii ahadi. Marehemu Mhe. Mirugi hayuko na sisi leo lakini alisimama na akanijibu hapa. Leo bahati mbaya baada ya heka heka za kampeini ya kura hiyo kuenda, mpaka leo hakuna mabadiliko yoyote. Hata leo haiko katika hii bajeti. Ni lini mishahara ya machifu itaboreshwa kwa sababu hiki ni kiungo muhimu? Nilisimama na nikasema haya wakati nilikuwa katika kura ya maoni. Katika kura ya maoni nilisema kwamba kama kuna mtu ambaye ana fikira za kuondoa machifu fikira zile ni bovu. Bahati nzuri au mbaya, kura ya maoni imekwisha na machifu wetu bado wako. Ni lini mishahara yao itaboreshwa? Ni lini hali yao ya kazi itaangaliwa? Bw. Naibu Spika wa Muda, tunatatizwa na Serikali kushughulikia maswala ya dharura. Miaka mitatu iliyopita kamati ya dharura ya Nairobi imejulishwa kwamba mto wa Tana utaharibu Garsen karibuni. Waliambiwa hii itakuwa dharura kubwa. Naomba unilinde kwa sababu nasikia mazungumzo kando yangu sana. Miaka mitatu iliyopita ripoti ilitolewa kwa kamati ya dharura kwamba mto wa Tana usipoangaliwa utafagia mji wote wa Garsen. Leo ni miaka minne tangu kwambiwa hivyo na juzi ofisi ya maji imebomolewa. Kamati yetu ya dharura iko Nairobi na kwa mwaka wa nne Serikali inafaa ishughulikie maswala ya dharura. Wakati inapoletewa ripoti kutoka mashinani ni vizuri wale wanaohusika wachukue hatua ya dharura. Ofisi ya maji imekwenda. Mashamba zaidi ya 12 imekwenda. Sasa mji wa Garsen huenda ukaenda wakati wowote. Bado tunangojea \"manna\" kutoka huko juu. Bw. Naibu Spika wa Muda, tatizo kubwa ni kwamba watunzi wa sera hawaelewi mbinu za ufugaji. Matatizo mengi na mizozo ya vita inayotoka katika jamii ya wafugaji yanasababishwa na malisho au maji. Wewe utashangaa kwa nini twapigana juu ya jangwa hili? Jangwa hili ndilo kahawa na majani chai ya sehemu hizo. Kwa nini? Kwa sababu ndilo tegemeo la mifugo. Hii nyasi na maji. Kisha maisha yote ya mfugaji kama ni elimu, afya na kadhalika, yamefungamana na ng'ombe au mbuzi huyo.Ili ng'ombe wetu wapate malisho na maji ya kutosha ni lazima tutenge sehemu za malisho na maji. Kuna wafugaji wengi wanaotumia pesa wanazozipata kutokana na ufugaji wa mifugo kulipa karo ya watoto wao. Tunajua kuwa wafugaji wengi huhama ili wapate malisho bora ya wanyama wao. Ningependa Serikali itenge sehemu za malisho na maji kwa sababu mzazi akihama kutafuta malisho bora, watoto wake huathirika sana. Iwapotutatenga sehemu hizo, basi wafugaji watafaidika na hawatahama kutafuta malisho ya mifugo yao. Tunataka watoto wetu waendelee na masomo yao. Hata hivyo, imekuwa ni vigumu kwa Utawala wa Mikoa kuelewa maswala haya. Maswala haya ni wazi kabisa. Wakati umefika wa mimi kuchukua panga ili nilinde malisho yangu. Je, wabuni sera za nchi hii watachukua miaka mingapi kuelewa shida za wananchi wetu? Bw. Naibu Spika wa Muda, Chifu ana mamlaka na uwezo anaoweza kutumia kulinda mazingira yetu. Uchimbaji wa mawe aina ya Gypsum, kwa mfano, umekuwa wa kutisha. Kila mwenye pesa anachimba mawe haya na kuharibu mazingira yetu. Mambo haya yote yanafanyika machoni mwa chifu, DO na DC. Hakuna anayeshughulika na mambo haya. Bw. Naibu Spika wa Muda, mazingira yana lugha ya ajabu na tunahitaji kuyalinda kwa lolote lile. Tusipofanya hivyo, yatatuathiri vibaya siku za usoni. Inafaa machifu wachukue hatua dhidi ya watu wanaokata miti na kuchimba mawe kiholelaholela. Sheria ya---"
}