GET /api/v0.1/hansard/entries/244536/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 244536,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/244536/?format=api",
    "text_counter": 107,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Raila",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 195,
        "legal_name": "Raila Amolo Odinga",
        "slug": "raila-odinga"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi ili nichangie Hoja hii muhimu sana. Kama nilivyosema hapo awali, ufukara katika nchi yetu utamalizwa iwapo Serikali itaangalia maslahi ya wakulima wadogo. Nimesema awali, na ninataka kurudia tena, kwamba haitoshi Serikali kutuambia kila mara kuwa uchumi wetu umekua kwa asilimia 5.8 kama mwananchi wa kawaida aliye mashinani hatahisi mabadiliko yoyote na ufukara unazidi kuenea nchini. Bw. Naibu Spika wa Muda, ukulima wa njugu kwa jumla ni muhimu. Kwa mfano, uchumi wa Senegal hutegemea ukulima wa njugu nyasa peke yake. Kwa hivyo, ikiwa nchi yetu itaweza kuimarisha ukulima wa njugu zote, sio tu ukulima wa korosho, uchumi wetu utaweza kuimarika. Ningependa Hoja hii ibadilishwe ili izungumzie njugu zote kwa jumla: njugu nyasa, korosho na makadamia. Pia, ni muhimu kuwa na halmashauri ya kusimamia sekta hii ya uchumi wetu ili wakulima waweze kuwa na njia ya kuuza bidhaa zao wenyewe bila ya kutegemea mawakala. Mawakala hawa huwanyonya sana wakulima na wavuvi. Wakulima wa njugu na wavuvi hawapati manufaa yoyote kutokana na jasho lao katika ukulima na uvuvi kwa sababu wale wanaofaidika zaidi ni mawakala wanaonunua bidhaa zao kwa bei ya chini na kuuza kwa bei ya juu. Wafanya July 5, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 1817 biashara hawa wanazidi kutajirika hali wakulima wanazidi kufukarika. Kwa hivyo, Bw. Naibu Spika wa Muda, ni jukumu la Serikali kuwa katika mstari wa mbele katika kutetea haki za wakulima na wavuvi. Kila mara Waziri anapokuja hapa kusoma Bajeti, yeye hutuelieza vile Serikali inataka kupigana na umaskini na vile uchumi unavyoendelea kuimarika. Kwa mfano, tumeelezwa kuwa uchumi wetu sasa umepanuka. Lakini iwapo mwananchi wa kawaida hatahisi faida za kupanuka kwa uchumi, ni kazi bure kutuambia kwa ishara tu na kutupatia idadi ya kukua kwa uchumi ili kuwapumbaza watu. Ni watu wachache tu kule juu wanaohisi kupanuka kwa uchumi wetu. Kwa mfano, kila mwaka tunasikia kuwa benki na kampuni za mafuta zinazidi kupata faida zaidi. Lakini kwa upande mwingine, kule chini, bei za bidhaa muhimu kama vile unga, sukari na mafuta taa zinazidi kuongezeka. Kwa hivyo, mwananchi wa kawaida anazidi kupata shida zaidi. Ninaunga mkono kwa dhati kuletwa kwa Hoja hii ili wakulima waweze kupata manufaa zaidi. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa muda mrefu, nimekuwa na uhusiano na wakulima wa korosho. Kwa mfano, unajua kuwa kile kiwanda cha korosho cha Kilifi kilikuwa kimefungwa na wakulima wa korosho wamekuwa na shida zaidi. Lakini ikiwa kiwanda hiki kinafanya kazi, vile vile viwanda vingine vinaweza kujengwa kwa sababu korosho inaweza kukuzwa kwa wingi kwa sababu hali ya anga kule pwani ni nzuri zaidi kwa ukulima wa korosho. Lakini wakulima sasa hawana haja kulima korosho kama watakuwa wanavuna korosho na hawaoni manufaa yake. Hii ndio sababu wakulima wa korosho wanakata mikorosho. Unajua kuwa kupanda mikorosho hadi ikomae na kuzaa korosho kunachukua muda mrefu. Kwa hivyo, jambo hili ni la dharura na wakati umewadia kwa Serikali kufanya kazi haraka zaidi ili tuwaokoe wananchi wetu wanaopata shida. Bw. Naibu Spika wa Muda, nilipokuwa mtoto, kulikuweko na mafuta yaliyokuwa yanaitwa Uto. Mafuta hayo yalikuwa yakitengenezwa kutoka kwa njugu nyasa. Njugu nyasa zilikuwa zikikuzwa kwa wingi katika sehemu ya Ziwa Victoria. Hali ya anga na ardhi katika sehemu hiyo ni nzuri sana kwa ukuzaji wa njugu nyasa. Wakati huo, wakulima walikuwa wakipeleka njugu sokoni na wanunuzi walikuwa wakilipa pesa taslim. Wakulima walitumia pesa hizo kununua vyakula na kulipia karo za shule. Kwa hivyo, watu hawakuwa maskini. Wakati huu Mkoa wa Nyanza unaongoza kwa ufukara humu nchini kwa sababu kilimo cha njugu nyasa na ufuta kimekufa. Kilimo cha njugu kinaweza kufufuliwa. Nimewahi kuitembelea Senegal na kujionea jinsi nchi hiyo inavyokuza njugu nyasa. Kama nilivyosema hapo awali, uchumi wa Senegal unategemea kilimo cha njugu nyasa peke yake. Mapato ya zao hilo yanaiwezesha nchi hiyo kununua bidhaa nyingine kutoka ng'ambo. Kwa hivyo, tuko na utajari ambao hatujautambua. Tumekuwa kama fisi anayeishi katika shamba la miwa, lakini hajui utamu wa miwa. Fisi huyo, hutoka katika shamba hilo la miwa na kwenda kutafuta chakula kwingineko. Bw. Naibu Spika wa Muda, nchi hii ina utajiri mkubwa. Mmea wa macadamia unaweza kukuzwa katika maeneo ya Taita na kwingineko. Korosho, njugu karanga na ufuta ni mazao yanayoweza kukuzwa katika sehemu nyingi nchini. Tunaweza kutengeneza siagi maalum inayoitwa \"peanut butter\" kutoka kwa njugu. Siagi hiyo inahitajika sana katika nchi za ng'ambo. Bidhaa hizo zinaweza kuiletea nchi hii fedha nyingi za kigeni. Tunachohitajika kufanya ni kutayarisha mpango muafaka wa kuimarisha uchumi wetu. Kwa hivyo, nikitamatisha mchango wangu, ningependa kuiomba Serikali hii iamke na kuzingatia maslahi ya wananchi. Serikali hutumia pesa nyingi kwa Bajeti ya Ulinzi. Pesa hizo hutumika kununua vifaa vya kijeshi na silaha ambazo hazihitajiki hapa nchini. Inafaa Serikali izingatie maslahi ya wakulima badala ya kuleta humu nchini watu kama Artur Margaryan. Watu hao hawana kazi ya kufanya katika nchi hii. Sisi sio maadui kiwango cha kupigana kwa silaha. Sisi hupigana kwa mdomo. Tumestaarabika. Hakuna haja ya kuleta mamluki kutoka nje. Mamluki wanaletwa hapa nchini kufanya kazi gani? Bw. Naibu Spika wa Muda, niliposema kwamba kulikuweko na mamluki humu nchini, 1818 PARLIAMENTARY DEBATES July 5, 2006 watu fulani walisema eti nilikuwa nikisema uongo. Walidai eti nilikuwa nikidaiwa pesa na mamluki hao, na kwamba eti madai yangu yalikuwa njama ya kukwepa kulipa deni hilo. Kila mtu anapaswa kufahamu kwamba, yale mambo anayoyafanya usiku hujitokeza mchana. Sasa, ukweli umekithiri. Watu fulani walisema: \"Wale watu walikutana na Bw. Musyoka na alikuwa anataka pesa kutoka kwao.\" Pesa za kufanyia nini? Huwezi kuomba pesa kutoka kwa mtu ambaye unakutana naye kwa mara ya kwanza. Hayo yote---"
}