GET /api/v0.1/hansard/entries/244538/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 244538,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/244538/?format=api",
"text_counter": 109,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Raila",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 195,
"legal_name": "Raila Amolo Odinga",
"slug": "raila-odinga"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ninazungumza juu ya uchumi kwa jumla. Ninasema kwamba Serikali ina jukumu la kusimamia uchumi wa nchi hii na kuhakisha kwamba umestawi. Nimesema kwamba badala ya kuzingatia mambo ambayo hayana manufaa kwa nchi hii, Serikali inapaswa kuweka juhudi zaidi katika sekta ya kilimo. Hivyo ndivyo nilivyoiambia Serikali, na ninafahamu kwamba ukweli huuma. Bw. Naibu Spika wa Muda, mimi ningependea kuiambia Serikali kwamba, mkulima mdogo ameathirika zaidi. Wakulima hao hufanya kazi mashambani mwao kwa muda wa miezi tisa lakini hawapati cho chote. Watoto wao hufukuzwa shuleni kwa kukosa kulipa karo. Watu kama hao huona uchungu sana wanapoiona Serikali ikiwapuuza na badala yake kufanya mambo ya kujipatia faida ya haraka haraka na kutuletea mamluki kutoka nchi za nje, ambao hatuwahitaji. Hivyo ndivyo nilikuwa nikisema."
}