GET /api/v0.1/hansard/entries/244541/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 244541,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/244541/?format=api",
    "text_counter": 112,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Rai",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 203,
        "legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
        "slug": "samuel-rai"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ya kuichangia Hoja hii. Kwanza, ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeze Bw. Khamisi kwa kuileta Hoja hii Bungeni. Kwa miaka zaidi ya 40, wakazi wa pwani tumekuwa tukiishi katika hali ambayo Mwenyezi Mungu ndiye anayeijua. Miaka 40 iliyopita, wakazi wa pwani walikuwa wakijetegemea. Walikuwa na matumaini kwa sababu ya shughuli fulani za kiuchumi zilizokuwa zikiendelea katika Mkoa wa Pwani. Zao la korosho lilikuwa tumaini kubwa la kiuchumi kwa wakazi wa Pwani. Mazao ya bixa, miwa, nazi na pamba yalikuwa tumaini kubwa kwa wakazi wa Pwani, lakini miaka 40 baadaye, haijulikani iwapo kilimo cha bidhaa hizo kinaweza kufufuliwa tena. Kwa hivyo, ninaiomba Serikali ifikirie itakavyofanya kuwawezesha wakazi wa pwani kuufurahia uraia wao katika nchi hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, hali ilivyo Mkoani Pwani inaweza kufananishwa na ile hadithi ya mama aliyekosa chakula cha kuwapikia watoto wake. Katika hadithi hiyo, mama huyo aliweka mawe kwenya sufuria na kuibandika jikoni. Mama huyo aliijaza maji sufuria hiyo halafu akaifunika. Mama huyo akawaambia watoto wake kwamba chakula kilikuwa kikitokota jikoni, na hali alijua kwamba alikuwa akichemsha mawe. Watoto walingojea chakula kiive hadi wakashikwa na usingizi na wakalala, mmoja baada ya mwingine. Wapwani wamevumilia kwa muda mrefu. Mawe hayo hayajaiva, na haijulikani yataiva lini. Kwa hivyo, Serikali inapaswa kufahamu kwamba sasa Mpwani anajua haki zake za uraia katika taifa hili. Mkorosho unafaida nyingi. Zao la korosho lilimfaidi Mpwani kwa njia nyingi, jinsi mazao ya bixa, miwa na nazi yalivyomfaidi mkazi wa eneo hilo. Jambo la kushangaza ni kwamba, uzalishaji wa mazao hayo ulipuuziliwa mbali na shughuli katika sekta hizo zikasambaratika. Licha ya kwamba mimea hiyo hustahimili ukame, na hivyo basi kuweza kustawi katika mazingira July 5, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 1819 magumu, haijatiliwa maanani. Ni kama kwamba Serikali imeziba masikio ili isiweze kusikia kilio cha watu wa pwani, na ndio sababu uchumi wa eneo hilo umesambaratika. Huu ndio wakati wa kuibadilisha hali hiyo. Bw. Naibu Spika wa Muda, wakati nilipozaliwa, zaidi ya miaka 40 iliyopita, zao la pamba lilikuwa likifanya vizuri sana katika Mkoa wa Pwani. Mapato kutokana na zao la pamba yalikuwa yakiwasaidia wakulima katika sehemu hiyo. Kufikia sasa, shughuli za uzalishaji wa hiyo mimea yote mitano zimekuwa historia. Tumekuwa tukiambiwa kwamba tuendelee kukaa vile tulivyo. Hatujui tutategemea kitu gani. Bw. Naibu Spika wa Muda, bahari \"imezaliwa\" kule pwani lakini sasa Serikali inanuia kuyahamisha makao makuu ya Bandari nchini, kutoka Mombasa hadi Nairobi. Mambo kama haya yatakoma mwaka gani? Wakati umefika watu kuambiana ukweli na kujua tulikotoka na tunakoelekea. Kila mwananchi anastahili kiasi fulani cha matunda ya Uhuru. Mambo kama hayo ya kutegemea chakula cha msaada yatakoma siku gani? Tumelima na kupanda vizuri na pia nafikiri kumeanza kuwa na unawiri wa mahindi. Hata hivyo, janga lingine ambalo limeanza kutukumba ni lile la kuona kwamba ndovu wa Kenya Wildlife Service (KWS) wamefunguliwa milango yote. Ndovu hao wameanza kuingia mashambani mwetu na kuharibu mimea. Kila wakati tunapopiga kelele, tunaambiwa tunyamaze, eti Serikali inajua. Ikiwa kuna sumu ya ndovu, na niipate ikiuzwa mahali, ndovu hao hamtawasikia tena kwa sababu hatutaruhusu wala kukubali watu wetu waendelee kuwa maskini na kupewa chakula cha msaada. Umaskini huo waweza kupunguzwa kwa sababu wananchi wenyewe wanajitahidi katika kazi zao. Ofisi ya KWS imefunga maskio na haitaki kujua shida zetu. Inafanya kama vile ndovu hufanya anapotembea kama amefunga maskio yake na kusema hakuna mtu anayemweza duniani hii. Watu wa KWS yafaa wakate shauri na wajue kwamba sisi tumetoa ilani: Kuanzia sasa hivi, ni sisi na wanyama! Mimea yetu imepata taabu na uchumi wetu kuharibika. Maisha yetu yamekuwa duni kwa sababu ya mambo kama hayo. Mkorosho ulikuwa ukimsaidia Mpwani, lakini ukafika wakati ambapo soko la korosho liliharibiwa. Kiwanda cha korosho kilisimamiwa vibaya na mashine zikauzwa; pengine zikapelekwa Tanzania. Baada ya Serikali hii kuingia mamlakani, ahadi na nadhiri tulipewa. Tuliambiwa viwanda tofauti vitafunguliwa lakini sasa, hayo yote ni ndoto. Kama Serikali yenyewe yaweza kuota mchana, je, mwananchi atafanyaje? Tunaiomba Serikali, kupitia Wizara inayohusika na mambo kama hayo, ijue kwamba kama mkorosho hauonekani kama mmea dhahiri ili uchumi wa watu wa Pwani uwe na mabadiliko, tutakuwa na nia mbili katika safari hii yakuelekea kule Kaanani, kwa sababu wengine wetu ambao si Waisraeli, afadhali turudi tulikotoka. Hatuwezi kusafiri pamoja na wenzetu ambao wanakula mikate, ila sisi tunakula mchanga. Haiwezekani! Utafika wakati wa kusema tumetosheka, na tutakuwa tumetosheka, lakini kwa sasa, tunataka jawabu la kutusaidia na kujua kama soko la korosho litafunguliwa au vipi, ili tupate kuwa na ustawi katika sehemu zetu. Bw. Naibu Spika wa Muda, hakuna jamii katika ulimwengu huu ambayo hutarajia kuwa maskini. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba hadi wakati huu, nchi hii inatambulika kuwa na matajiri wengi sana na maskini waliopita kiasi. Utajiri huo ulitoka wapi kama si mashine zetu za korosho na thamani za raslimali zetu kufanyiwa vibaya na Serikali na viongozi? Kufikia wakati huu, tumekuwa tukihimiza watu hao wachukuliwe hatua, ili kesi iwasilishwe katika Ofisi ya Mkuu wa Sheria. Sasa hivi, Mkuu wa Sheria yuko nje ya nchi, na Ripoti ya Bunge hili haijamfikia ili achukue hatua dhidi ya watu walioharibu soko la korosho huko Pwani. Wakati umefika ambapo tunahitaji vitendo na ishara ya kujua kwamba kwa kweli, tunaanza kutambuliwa, lakini si ahadi na nadhiri ambazo hazitambuliki. Mkorosho umefanyiwa utafiti wa kutosha na inajulikana kwamba unaweza kumuokoa Mpwani mahali popote alipo. Kwanda na soko la korosho vilifanyiwa ufisadi ili korosho zetu ziweze kukosa bei nzuri. Pamba tulipoteza, viwanda vya bixa na miwa tulifunga, na sasa ni mkorosho uliobaki tuukate ili tusubiri neema ya Mwenyezi Mungu. Sisi si Waisraeli 1820 PARLIAMENTARY DEBATES July 5, 2006 huko Pwani ili tuishi kwa kutegemea Mana. Tunategemea jitihada zetu. Tunalima ili tupate. Hatusubiri chakula kutoka mbinguni. Ni wakati kama huu ambapo viongozi wanapokaa yafaa tuambiwe ukweli kwamba mipango kama hiyo inaendelea. Naomba ndugu zangu tuipitishe Hoja hii. Tunapoipitisha, isiwe kama ile sheria ya mnazi ambayo baada ya kupitishwa iliwekwa katika sanduku la sahau. Masanduku hayo, funguo zake zitakapopatikana, watu wengine watakuwa mashakani. Ni lazima tusaidiane na kushirikiana ili tujue wananchi wanaweza kuokolewa kwa njia gani. Kama tutakuwa tukiwanyanyasa wananchi tunaowategemea na ambao wamejitolea kufanya kazi ngumu ili wainue hali yao ya maisha, itakuwa jambo la kusikitisha sana. Ni matumaini yangu kwamba, baada ya Hoja hii kupitishwa katika Bunge hili, yale mambo ambayo tumeomba yatimizwe yatafuatiliwa na ihakikishwe kwamba sheria mwafaka italetwa, ili iimarishe zao la korosho. Tumevumilia mengi lakini umefika wakati ambao sisi--- Sisemi tuonewe huruma, lakini nasema tunafaa kutambulika kama watu wengine katika Jamhuri hii. Twahitaji viwanda vya korosho, miwa, nazi na pamba virudishwe. Mchanga wetu ni ule ule ambao unafaa sana kwa kilimo. Mambo hayo yanafaa kutiliwa maanani ili mkorosho uweze kumfaidi Mpwani. Kwa hayo machache, nashukuru na ninamuomba Mwenyezi Mungu aibariki Hoja hii."
}