GET /api/v0.1/hansard/entries/245427/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 245427,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/245427/?format=api",
    "text_counter": 99,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa nafasi hii nami nichangie Hoja hii kuhusu Bajeti. Bajeti ya mwaka huu imepewa sifa nyingi. Inalenga kuondoa umaskini, ina shabaha ya kubadilisha maisha ya vijana na kadhalika. Lakini mimi nasema kwamba sifa ya Bajeti hii itajitokeza wakati itakapotekelezwa. Ndipo tutajua ikiwa Bajeti hii imeleta mabadiliko mapya katika hii nchi. Katika historia ya nchi yetu, tunatengeneza Bajeti miaka nenda, miaka rudi, lakini maisha ya wananchi hayabadiliki. Maana ya maendeleo ni kuboreka kwa maisha. Maisha yakibadilika kuwa mazuri zaidi, umaskini ukipungua, watu wakipata ajira zaidi, watu wakiwa na nyumba bora zaidi na ufukara ukipungua katika nchi, ndipo tutasema kwamba tumeona maendeleo. Lakini tukichunguza nchi yetu kwa ujumla, tunatengeneza Bajeti kila mwaka. Lakini mitaa ya mabanda inazidi kuenea kila siku. Umaskini upo katika miji. Watu wengi wanateseka. Kuna watu maskini ambao hawana ardhi. Lakini kila mwaka, tunatengeneza Bajeti. Lakini wale maskwota wanabaki vile vile. Waliotolewa katika mashamba yao kutokana na vita vya kikabila bado wanaendelea kuteseka. Hali yao haibadiliki kabisa! Kazi haziongezeki, viwanda haviongezeki--- Hata vinafungwa zaidi! Bw. Naibu wa Spika, tutakapokuwa na Bajeti kamili inayoambatana na mipango halisi ya kiuchumi ambayo inalenga kuboresha maisha katika nchi yetu, tutasema kwamba Bajeti hiyo ni bora. Kupata Bajeti kama hiyo, lazima tuwe na nia halisi ya kuangalia vile tunavyomiliki rasilmali zetu za asili. Katika Bajeti ya sasa, kumekuwa na juhudi za kutotegemea pesa za wafadhili. Hilo ni jambo zuri kabisa kwa sababu tukiendelea kutegemea wafadhili, tutakuwa chini ya makucha ya ubeberu. Tunajua kwamba hatujakuwa na faida kubwa kutokana na misaada kutoka nje. Inafaulu kutuparaganya na kutupotezea njia ya mipango ya maendeleo. Kwa hivyo, hiyo nia ya kutengeneza Bajeti ambayo haitegemei pesa za wafadhili ni nzuri sana. Lakini, lazima iambatane na mipango halisi ya umilikaji wa rasilmali zetu. Katika kufanya hivyo, sikubaliani na nia ambayo imejitokeza katika hii Bajeti kwamba, suluhisho la kiuchumi la nchi kama yetu ni kubinafsisha mashirika ya umma. Tunaelewa kwamba kubinafsisha mashirika ya umma sio suluhisho peke yake. Maduka ya Uchumi yalikuwa yakimilikiwa na watu binafsi. Lakini umeona vile yameangaia! Kwa hivyo, dhana kwamba suluhisho la kiuchumi ni ubinafsishaji wa mashirika ya umma peke yake, haifai. Katika nchi hii, lazima tuzingatie sekta zote za kiuchumi. Sekta zote tatu lazima zifanye kazi pamoja - sekta ya ubinafsi, ya dola na ya vyama vya ushirika. Tukiwa na suluhisho la kiuchumi kama hilo, tutaendelea mbele. Kama taifa, ni lazima tumiliki mambo muhimu katika uchumi letu. Mfano mzuri ni nchi za Latin Amerika. Zimekuwa na mpango wa ubinafsishaji kwa zaidi ya miaka 200, na hazijafaulu. Lakini sasa, zimeondoa ubinafsishaji na kuchukua uongozi wa makampuni kutoka watu wa nje. Mabadiliko yameanza kuonekana. Nchi ya Venezuela imeanza kusimamia mafuta yake. Bolivia imeanza kusimamia gesi yao. Peru na Mexico June 28, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 1643 pia zimefuata mtindo huo. Nafikiri nchi hizo zitaendelea mbele na kutuwacha nyuma sisi Waafrika. Nchi hizo zimeamka ilhali sisi tunaendelea kudanganywa kwamba barabara ya kujiendelesha ni ubinafsishaji tu. Mataifa mengi yamejaribu ubinafsishaji, lakini za yameanza kuendelea wakati yameanza kusimamia uchumi wao. Bw. Naibu Spika, ili kuwe na utekelezaji wa mambo ambao tunapitisha hapa, lazima tuwe na tarakimu sawa sawa. Kwa hivyo, Wizara ya Mipango na Maendeleo ya Kitaifa lazima ifanye kazi. Hakuna utafiti wa kutosha. Kwa mfano, katika Mkoa wa Pwani, Wilaya za Voi na Mwatate zinapewa basari. Lakini huwezi kuelewa ni kwa nini waalimu wa Wundanyi hawapati pesa hizo, na hali mazingira ya Wundanyi ni sawa na yale ya Voi na Mwatate. Hali hiyo inaletwa na kutokuwa na tarakimu za ukweli. Inaonekana kwamba Wizara ya Mipango na Maendeleo ya Kitaifa haifanyi kazi. Wakati tunapozungumzia habari ya Constituencies Development Fund (CDF)--- Kama vile Bw. Mwenje amesema, katika sehemu za mijini, kuna umaskini sana. Ni kana kwamba hakuna utafiti umefanywa kujua hali halisi ya umaskini. Ili kuwe na utekelezaji wa Bajeti kikamilifu, lazima kuwe na tarakimu za ukweli na lazima Wizara ya Mipango na Maendeleo ya Kitaifa ifanye kazi. Isitoshe, katika mambo haya yote tunayoyazungumzia, lazima tuzingatie sheria. Katika nchi yetu, tunatunga sheria lakini hatuzifuati. Kwa mfano, miji yetu inaendelea kuwa mitaa ya mabanda. Miji yote katika nchi yetu inakuwa mitaa ya mabanda! Tuko na sheria zinazowaongoza watu kujenga nyumba. Lazima wazingatie uhandisi fulani na kanuni zilizowekwa na Serikali za Mitaa. Lakini, hakuna mtu anafuata sheria. Ikiwa hatufuati sheria, hata tukiandika Bajeti nzuri namna gani, itakuwa kazi ya bure! Bw. Naibu Spika, pesa za CDF kwa kweli zinafanya kazi. Lakini hatujui asili mia 97.5 ya pesa zinazobaki katika mikono ya Serikali zinafanya kazi gani. Kwa mfano, tukienda Wundanyi na kuuliza Wizara ya Maji na Unyunyizaji Maji Mashamba ilifanya mradi gani tangu niingie Bungeni, hakuna hata mmoja. Tunaweza kuzungumzia Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Samaki. Lakini Wizara ya Elimu inajaribu. Kuna pesa kidogo ambazo zinafika kwa watu mashinani. Lakini kwa ujumla, ni lazima tuangalie kwamba hizi pesa--- Hali ya kuachia Serikali asili mia 97.2 na hatuoni maendeleo ni dhibitisho kwamba sera hiyo haifanyi kazi. Hizo pesa hazifikii wananchi. Nisikitika kwamba mwaka huu, CDF haijaongezwa mara dufu. Tungefanya hivyo, umaskini ungekwisha. Bw. Naibu Spika, tunasema kwamba Bajeti imelenga vijana. Lakini hizo ni siasa zinazoitwa kwa Kizungu \" populist politics\" . Ni siasa za kufurahisha tu. Matatizo ya vijana - kama ya kitaifa - yatasuluhishwa kama kutaboresha uchumi halisi katika nchi yetu. Lazima tutengeneze kilimo, viwanda vyetu na kuweka mikakati halisi ya kuondoa umasikini. Vijana wenyewe pia wamegawanyika kitabaka. Kuna tabaka la vijana wachache ambao ni matajiri. Hao ndio wanashikilia mamlaka. Ukiangalia watu wote ambao wanashikilia mamlaka katika nchi yetu, ni vijana. Kwa hayo machache, naomba kuunga mkono."
}