GET /api/v0.1/hansard/entries/245435/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 245435,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/245435/?format=api",
    "text_counter": 107,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Twaha",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 145,
        "legal_name": "Yasin Fahim Twaha",
        "slug": "yasin-twaha"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, asante sana kwa kunipatia fursa hii kuchangia Hoja hii ya Bajeti, yaani makadirio ya pesa za Serikali na matumizi yake. Wakenya kwa hakika walifurahishwa sana na Bajeti hii ya juzi kwa sababu iliangalia mambo mengi kama hayo ya akina mama, vijana, wakulima na waliostaafu. Yote yalikuwa ni mambo mazuri na ya maana na naunga mkono Bajeti hiyo. Bw. Naibu Spika wa Muda, lakini kuna maswali mawili au matatu ambayo wananchi wanauliza kule nyumbani. Swali la kwanza ambalo wanauliza ni: \"Tumesikia kwamba wakulima wa kahawa, maziwa na sukari walisamehewa madeni. Kwa nini Serikali haijafikiria katika Bajeti hii kutenga pesa za kusamehe madeni ya wakulima kule kwetu Lamu ambao wanapanda mazao ya pamba, bixa na korosho na wote ni wakulima wa Kenya?\" Kama Waziri angeangalia swala hilo, nafikiri pia sisi kule Lamu tungekuwa na furaha kama wale Wakenya wengine waliosamehewa madeni. Bw. Naibu Spika wa Muda, deni sio tu la wakulima bali liko katika mambo ya ardhi. Unajua swala la ardhi kule Pwani ni swala tata na nyeti sana. Tatizo la Lamu ni tofauti na yale matatizo ya sehemu zingine katika Pwani kwa sababu, kule Mombasa, Kwale na kwingineko kuna sehemu tatu ambazo zinavutana kwenye mambo ya ardhi. Kuna Serikali, wananchi wanaokaa katika ardhi na wale wenye ardhi ambao wanaitwa absentee landlords kwa Kimombo. Swala hilo linakuwa ngumu lakini kule Lamu ni baina ya wananchi na Serikali pekee yake. Kwa hivyo, Serikali ikifanya uamuzi inaweza kutatua shida za ardhi mara moja na wananchi wapate vyeti vyao vya kumiliki ardhi na wafanye maendeleo mengine wakichukua mikopo na kufanya biashara nyingine kwa sababu ukulima peke yake haiwezi kumudu idadi ya watu ambao wanazaliwa kila siku. Bw. Naibu Spika wa Muda, tumependekeza kwa Wizara, hata kama Serikali haitaki kutuhurumia jinsi iliwahurumia wananchi wa sehemu zingine za nchi hii kwa kuwasamehea madeni, tuko tayari kutumia pesa zetu za hazina inayojulikana kama, Constituency Development Fund (CDF) kulipia mashamba yetu. Watu wengine wanasema hatuwezi kutumia pesa za Serikali kulipa madeni ya kibinafsi. Ikiwa wakulima wote wanalipiwa mashamba, hilo si deni la kibinafsi, bali ni deni la jamii. Hazina ya CDF hasa, ni ya kuondoa umaskini. Njia moja ya kuondoa umaskini ni kuturuhusu tuzitumie pesa za CDF kulipia madeni ya mashamba yetu kwenye makao yetu ya mashambani katika Eneo Bunge la Lamu. Bw. Naibu Spika wa Muda, Hotuba ya Waziri ilikuwa nzuri lakini alisahau kutuambia ni pesa ngapi ametenga kulipa fidia kwa wananchi ambao wameathiriwa na wanyama pori. Wanyama pori wametusumbua sana. Wanyama hao wanaharibu mimea, wanawaumiza watu na wakati mwingine, hata kuwaua wananchi. La kustaajabisha ni kuwa wananchi hawalipwi fidia kwa kupoteza mimea, vyombo na hata maisha yao. Tungefurahi kusikia ni pesa ngapi Waziri ametenga na ni utaratibu upi utafwatwa ili watu ambao wameathiriwa na wanyama wa pori wapate kulipwa fidia. Wanyama hao ni miliki ya Serikali. Ni lazima Serikali iwahifadhi vizuri, ili wasiwaathiri wananchi. Ikiwa Serikali haiwezi kulipa fidia, basi inafaa iwasamehe watu wa Eneo Bunge la Lamu madeni mengine. Shida moja inayotufanya tusilipe madeni yetu ya mashamba ni kwa sababu mimea inaharibiwa na wanyama wa pori kama ndovu, viboko na kadhalika. Wakulima wanapata hasara na hawawezi kupata pesa za kujibuni kimaisha na kulipa madeni hayo. Bw. Naibu Spika wa Muda, Waziri pia hakuzungumzia ni vipi atawasaidia wakulima wa pamba na korosho kwa njia ya kuwapatia vifaa kwa bei ya chini, kwa mfano, mbolea, madawa ya kuwaua wadudu na kadhalika. Pia hakuzungumzia wazi ni mikakati gani Serikali itatumia kuinua bei ya mazao na mifugo. Tungefurahi sana kusikia ni vipi tutaweza kuanzisha kiwanda ambacho kitaleta mashindano baina ya wanununuzi wa mazao hayo. Wakati huu katika eneo la Pwani, kuna kampuni moja tu ya kununua pamba. Kampuni hiyo ina fursa ya 1648 PARLIAMENTARY DEBATES June 28, 2006 kuweka bei vile inataka. Ikiwa kuna viwanda viwili ama vitatu, kutakuwa na mashindano ya ununuzi wa mazao, ili kuhakikisha mapato ya wakulima yataongezeka na hali yao ya kimaisha itaimarika. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, naunga Hoja hii mkono."
}