GET /api/v0.1/hansard/entries/245722/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 245722,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/245722/?format=api",
    "text_counter": 233,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kingi",
    "speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
    "speaker": {
        "id": 27,
        "legal_name": "Amason Jeffah Kingi",
        "slug": "amason-kingi"
    },
    "content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuuchangia Mswada huu. Ningependa kuanza nikiwaunga mkono Wabunge wenzangu waliosema kwamba Bajeti hii imezingatia maadili ya Wakenya na kujaribu, kwa hali ngumu kidogo, kuhakikisha kwamba kila Mkenya, popote alipo, amefikiwa na Bajeti hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, Mbunge mwenzangu aliyetangulia kuzungumzia Mswada huu, Bw. Ojaamong, aligusia swala la ajira. Ameiomba Serikali iwaajiri kazi watu kutoka sehemu yake ya uwakilishi Bungeni. Ningependa kumuhakikishia Bw. Ojaamong kwamba Serikali imeshafanya hivyo, inazidi kufanya hivyo, na itaendelea kufanya hivyo. Katika sehemu yake ya uwakilishi Bungeni, kuna manaibu wa machifu, machifu na walimu ambao wanahudumu katika Serikali. Ndio maana nimesema kwamba tumeshawaajiri, na tutazidi kuwaajiri wakaazi wa Teso kama tunavyowaajiri Wakenya wengine mahali popote walipo. Kuhusu swala la kuongezwa kwa idadi ya maeneo ya uwakilishi Bungeni, sote tumepewa nafasi ya kutoa maoni yetu kwa tume ya Uchaguzi Nchini (ECK), ambayo inazunguka kote nchini kuchukua maoni ya wananchi juu ya jambo hili. Ninaamini kwamba Bw. Ojaamong atapata nafasi ya kutoa maoni yake kwa tume hiyo. Kama atajitetea vizuri mbele ya tume hiyo, sielewi ni kwa nini ana wasiwasi kiasi cha kuja Bungeni na kumwomba Waziri wa Haki na Maswala ya Katiba aende kumtetea, kana kwamba yeye mwenyewe hawezi kujitetea. June 28, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 1707 Bw. Naibu Spika wa Muda, Bajeti hii imezipa nafasi sekta nyingi za nchi hii. Tukianzia sekta ya elimu, tunafahamu kwamba elimu huleta maendeleo na msingi wa maisha ya leo. Kwa hivyo, kwamba sekta ya elimu imeangaziwa vilivyo na kupewa kipa umbele katika Bajeti hii, ni jambo la kupongezwa. Sasa, kinachosalia ni wasimamizi katika sekta hii kuhakikisha kwamba pesa hizo zimesimamiwa vizuri ili ziweze kufanya shughuli ambayo imenuiwa. Walimu wamelalamika sana kuhusu mishahara yao. Hivi majuzi, walitishia kugoma kwa sababu ya marupurupu yao yaliyozungumziwa tangu mwaka wa 1996, na ambayo hayajalipwa kikamilifu. Marupurupu hayo yalileta maneno mengi. Kwa hivyo, ninamwomba Waziri wa Elimu aanzishe mazungumzo na walimu, na iwapo kuna uwezekano wa kuwalipa walimu hao marupurupu ya nyongeza za mishahara yao yaliyosalia, asisite kufanya hivyo. Akifanya hivyo, Waziri atawapatia walimu motisha ya kuweza kufanya kazi kwa bidii zaidi. Bw. Naibu Spika wa Muda, hapa Bungeni, mara kwa mara, tumekuwa tukijibu Maswali kuhusu majengo ya shule yaliyoharibiwa aidha na upepo mkali au mvua nyingi. Inaonekana hakuna mwongozo maalum wa kuziwezesha shule zinazoathiriwa na majanga kama haya kufaidika. Kwa hivyo, ninamwomba Waziri katika Afisi ya Rais wa Mipango Maalum kuhakikisha kwamba mambo haya yamefikiriwa ili majengo ya shule yanapobomoka kufuatia majanga haya, yarekebishwe mara moja ili watoto wasitaabike. Mimi nahusika na mambo ya utawala wa mikoa. Katika Bajeti yetu, tulipatiwa kiwango cha pesa ambacho hatukukitarajia. Mambo mengi katika taifa letu hutegemea utawala mzuri. Usalama huwezesha elimu kuendelea vyema na pia huwezesha watu kufanya kazi vizuri. Tunatarajia kwamba katika Bajeti ijayo, mambo ya usalama yatapewa uzito kama vile elimu inavyopewa uzito. Tulitarajia kupata pesa za kutosha ili tuajiri askari wengi ambao wangetapakaa kila mahali na kuhakikisha kwamba usalama unaimarishwa. Tulitarajia kupata pesa za kutosha ili tuwaajiri maofisa wa usalama katika kila tarafa kwa sababu mara nyingi, watu hutaka tupeleke maofisa katika kila tarafa, lakini kwa sababu ya upungufu wa pesa, hatuwezi kuwaajiri. Tunataka pesa zaidi ili tuhakikishe kwamba tutafungua kituo cha polisi katika kila lokesheni, aidha cha kawaida au kile cha utawala, ili tuhakikishe kwamba wananchi wanaishi maisha mema. Kwa hivyo, ingawaje Bajeti hii imekuwa nzuri, kuna sehemu za muhimu ambazo tunaona zimetubana sana. Tunatoa mwito kwamba sehemu za muhimu kama hizo ziangaziwe vilivyo. Tatizo kubwa lililopo katika mkoa wa Pwani ni lile la ardhi. Nashukuru kwamba Waziri wa Fedha ametenga kiwango cha Kshs400 milioni ambacho nadhani lengo lake ni kushughulikia maslahi ya ardhi ya maskwota na sehemu ambazo hazijagawanywa, ili wananchi wapewe vyeti vya kumiliki ardhi. Pesa hizo, Kshs400 million, hazitoshi, lakini ni pesa ambazo zinaweza kuanzisha kazi na ionekane. Tuna imani kwamba Waziri wa Ardhi, atakapokuwa akitumia pesa hizo katika kufanya kazi yake, ataangazia Mkoa wa Pwani ambapo kuna matatizo sugu ya ardhi, kwa sababu kuna maskwota na watu wengi wasio na makao. Kwa hivyo, tunaomba pesa hizo zitumiwe vizuri ili ziwapatie makao wananchi wa Mkoa wa Pwani kwa sababu wamepata matatizo kwa muda mrefu. Ningetaka kuzungumzia mambo ya uvuvi, ambayo ni uchumi kabambe kwa watu wa Pwani na pia wananchi wanaokaa katika sehemu za Ziwa Victoria. Bajeti yetu imetenga pesa kidogo na tunaamini zitakapoanza kutumiwa, zitatumiwa vyema na kuwapatia wavuvi vifaa bora ambavyo watatumia kuvua samaki na kuziuza ili wapate pesa za kuwawezesha kufanya shughuli zao. Katika Mkoa wa Pwani, wavuvi wengi hawana vifaa vinavyohitajika kufanyia uvuvi. Wageni ndio wanafanya shughuli hiyo kwa sababu wao ndio walio na vifaa vya kisasa. Nadhani si lengo la Serikali au nchi yetu kuimarisha uvuvi kwa wageni na si kwa Wakenya. Nataka kushukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kufungua kiwanda cha Kenya Meat Commission (KMC), kilichofunguliwa majuzi. Hiyo ni ishara bora hata kwa wale ambao viwanda vyao vilikuwa vimefungwa, kwamba sasa vitafunguliwa. Napongeza mipango iliyopo ya 1708 PARLIAMENTARY DEBATES June 28, 2006 kuhakikisha kwamba kiwanda cha Mombasa kimefikiriwa na hivi karibuni kitafanya kazi. Katika moyo huo, tungeomba viwanda vingine, kama vile vya Mariakani Milling Scheme na Ramisi Sugar Factory, vifikiriwe ili vifunguliwe na wananchi wapate kazi za kutengeneza vifaa ambavyo vinaweza kupatia nchi yetu pesa za kuimarisha uchumi. Nataka kumpongeza Waziri kwa kuangazia mambo ya vijana na kumuuliza Waziri anayehusika na mambo hayo kwamba anapopanga miradi, ahakikishe kwamba itagusa vijana wote popote walipo katika taifa hili kwa usawa. Kwa hayo mengi, naunga mkono."
}