HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 245917,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/245917/?format=api",
"text_counter": 173,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kajembe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 163,
"legal_name": "Ramadhan Seif Kajembe",
"slug": "ramadhan-kajembe"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Naomba kushiriki katika mazungumzo ya Bajeti ya mwaka huu. Bw. Naibu Spika, sehemu kubwa ya Bajeti hii ni nzuri. Ile sehemu ndogo iliyobakia ndio itakayowaumiza Wakenya. Waziri alipendekeza kuondolewa kwa kodi ya leseni ya kutumia barabara na kuongezwa kwa kodi ya petroli kwa Kshs3.20 kwa kila lita. Ukilinganisha ushuru ambao ulikuwa ukikusanywa kupitia kodi ya leseni ya kutumia barabara na ule ushuru utakaokusanywa kupitia kodi mpya ya petroli, utaona kwamba Serikali itakusanya pesa nyingi zaidi katika mwaka huu. Lakini gharama za uchukuzi katika sekta ya umma na uchukuzi wa mizigo zitaongezeka. Mwananchi wa kawaida ataathirika kutokana na kuongezeka kwa nauli katika magari ya abiria. Mishahara wanayolipwa wafanyikazi katika sekta za umma na kibanafsi nchini humu bado iko chini sana. Kuongezeka kwa gharama za uchukuzi hali misharaha bado ni kidogo kunamuumiza mwananchi wa kawaida. Hali hiyo inaondoa umaarufu wa Serikali miongoni mwa wananchi. Huu si wakati wa kumwongezea mwananchi gharama za maisha. Ukilinganisha matumizi miongoni mwa jamii na mishahara wanayolipwa wafanyikazi katika sehemu za mijini na mashambani, utaona kwamba mishahara bado ni kidogo sana. Serikali imetwambia kwamba uchumi wa nchi hii umekua kwa asilimia 5.6. Iwapo ni kweli kwamba uchumi umekua kwa kiasi hicho, inafaa Serikali iongeze mishahara ya wafanyikazi wote wa umma nchini, wakiwemo walimu. Bw. Naibu Spika, ningependa kuipongeza Serikali kwa kuanzisha mpango wa elimu ya bure. Ingawaje inasemekana kwamba watoto wanapata elimu ya bure, ukweli ni kwamba watoto hawapati elimu ya bure, kwa sababu pesa za umma zinatumika kugharamia mpango huo. Uchumi unapokua, pesa huongezeka. Kama kweli uchumi wa Kenya unaongezeka kwa kasi kama inavyodai Serikali, basi kuna haja Serikali kufikiria kuanzisha mpango wa elimu ya bure katika kiwango cha sekondari. Kufanya hivyo kutampunguzia mwananchi mzigo wa kuwaelimisha watoto. Kuhusu sekta ya uchukuzi, kila mwaka, kiasi kikubwa cha pesa hutumika katika urekebishaji wa barabara, haswa barabara ambazo hazijawekwa lami; lakini, barabara hizo huharibika wakati wa msimu wa mvua. Kwa hivyo, kila mwaka, pesa ambazo hutumika kwa shughuli hiyo hupotea bure. Hivyo ni kumaanisha kwamba pesa hazipo. Ni lazima kuwe na mpango mwingine, ikiwezekana, ili kila barabara katika nchi hii itengenezwe kwa njia inayoweza kudumu, badala ya kupoteza pesa kiholela. Kunapokuwa na shida, watu huanza kurekebisha mambo nyumbani kwao. Bandari ya Mombasa inakusanya pesa nyingi sana kama ushuru. Hata hivyo, pesa hizo zinazokusanywa hazisaidii wakaaji wa Mombasa, bali tu pesa zinazotolewa katika mradi wa CDF. Kuna kandarasi ya kutengeneza barabara inayotoka Miritini kwenda mpaka Maji ya Chumvi, ambayo imetangazwa. Tumelia na kutoka machozi ya damu kwa sababu barabara hiyo imekuwa mbaya. Barabara hiyo ndio inayosaidia uchumi wetu, kwa sababu magari yanayotoka Kilindini huleta mizigo na magari yanayoenda Kilindini pia hutumia barabara hiyo. Baada ya sisi kulia machozi ya damu, kandarasi ya kutengeneza barabara hiyo ilitolewa. Kulingana na utengenezaji wa barabara na pesa zilizotengwa na Serikali kwa kazi hiyo katika Mkoa wa Pwani, ni barabara hiyo tu ambayo 1626 PARLIAMENTARY DEBATES June 27, 2006 Serikali imeamua kutengeneza katika Mkoa wa wilaya saba. Kuna barabara mbovu katika sehemu za Mombasa. Afadhali kama kungekuwa na mpango maalum wa kugawa fedha za kutengeneza barabara, lakini sasa, sehemu wanapotoka Mawaziri na Wabunge wenye nguvu katika Serikali ndio hupata pesa nyingi, na sehemu zinazoongozwa na watu ambao wako katika Serikali. Nafikiri tuna haki ya kugawiwa pesa za kutengeneza barabara na pia za kuendesha miradi mingine ya maendeleo. Bw. Naibu Spika, ni jambo la aibu, fedheha na uzembe kuwa na mahali kama Mkoa wa Kaskazini Mashariki ambapo watu wanaota lakini hawajaona barabara za lami. Watu katika sehemu hiyo wamekuwa wakiota tangu mwaka wa 1963 tulipopata Uhuru. Ni lazima Serikali ieneze maendeleo ya barabara, mashule na maendeleo mengine. Hakuna sheria inayosema wilaya fulani inafaa kufaidika zaidi, na nyingine iumie zaidi. Tunataka maendeleo na barabara zitengenezwe kwa usawa. Wakati Serikali hii ilipochukua hatamu, tuliambiwa kwamba kiwanda cha sukari huko Ramisi kitafunguliwa. Tuliambiwa pia kiwanda cha korosho kitafunguliwa. Sasa tuko karibu kwenda katika uchaguzi na kiwanda cha sukari bado kimekwama. Kile cha korosho pia kimekwama."
}