GET /api/v0.1/hansard/entries/246328/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 246328,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/246328/?format=api",
    "text_counter": 141,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Moroto",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Health",
    "speaker": {
        "id": 318,
        "legal_name": "Samuel Chumel Moroto",
        "slug": "samuel-moroto"
    },
    "content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili nichangie Hoja hii kuhusu Hotuba ya Bajeti ya mwaka huu. Kuna wimbo unaosema: \"Ombea adui yako aishi maisha marefu ili aone baraka ambazo unazopewa na Mwenyezi Mungu\". Waziri wa Fedha aliposoma Bajeti ya mwaka huu aliwapa Wakenya wengi matumaini ya maisha yao ya sasa na siku za usoni. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa miaka mingi, jamii ya wafugaji haijashughulikiwa na Serikali yetu. Sisi kama Wakenya tulijitahidi sana kupigania Uhuru wa nchi hii na hatimaye tukaupata. Lakini tulipoanza safari ya kuendeleza shughuli za nchi hii, baadhi ya viongozi walituzuia kupata maendeleo. Tumeomba sana Serikali isaidie jamii ya wafugaji na inaonekana kwamba Mwenyezi Mungu kwa wakati huu anayasikiliza maombi yetu. Bw. Naibu Spika Wa Muda, jamii yetu imegawanyika katika vikundi kadha wa kadha kimaendeleo. Kuna kikundi cha juu, kati na chini. Ombi letu kubwa kwa Serikali hii ni kuhakikisha ya kwamba pesa ambazo zimetengewa sehemu kavu za nchi hii zinatatumiwa kikamilifu. Tukitumia pesa hizo vilivyo, watu wetu watafaidika sana. Bw. Naibu Spika wa Muda, mzozo uliotekea katika Kaskazini mwa Bonde la Ufa kati ya wafugaji ulisababishwa na upungufu wa mahitaji ya kimsingi ya wakaazi hao na mifugo wao. Mara nyingi, wakaazi wa West Pokot na Turkana huhama hadi Uganda na mifugo wao kutafuta maji na lishe bora. Ingawa Uganda imekuwa na matatizo kadhaa lakini watu wetu bado wanakimbilia huko kutafuta usaidizi. Huu ndio mwanzo na ndio maana ninasimama hapa kumpongeza Waziri kwa kufikiria wafugaji katika Bajeti yake. Jambo lingine ambalo ningependa liangaliwe ni elimu. Ingawa Wizara ya Elimu imetengewa fedha nyingi katika Bajeti hii, watu wetu katika Kaskazini Mashariki na Kaskazini mwa Bonde la Ufa wanazidi kuhama na mali yao. Watoto wao hubaki wakihangaika kusoma. Kwa hivyo, tungependa shule za mabweni zianzishwe katika sehemu hizo ili tupate kufurahia matunda ya nchi hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, kulikuwa na ukame mkali ambao uliangamiza mifugo wengi. Huo ndio utajiri wetu katika sehemu hizo. Ningependa kuuliza Wizara ya Elimu ijaribu kupunguza karo za shule, hasa katika sehemu kame ili kuwahimiza wazazi kuwatuma watoto wao shuleni. Pia 1500 PARLIAMENTARY DEBATES June 21, 2006 ningeomba Serikali igharamie karo za shule kama vile wanavyogharamia chakula cha msaada ili watoto wetu wasikose kusoma na wapate haki yao. Ningependa kuwashukuru sana wadhamini mbali mbali kama makanisa na mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO). Mashirika hayo yametusaidia sana katika kupambana na ukosefu wa chakula na mahitaji mengine. Vile vile, yamechangia sana kuleta maendeleo katika maeneo hayo na kuwapa watu wetu moyo wa kuendelea kuishi. Bw. Naibu Spika wa Muda, pia ningependa kumpongeza Waziri wa Mifugo na Usitawi wa Samaki kwa kuanzisha rasmi kiwanda cha Kenya Meat Commission (KMC). Wakati Waziri alisema kuwa KMC itaanza kufanya kazi, tuliichukulia kama ndoto ama hadithi za kawaida ambazo unasema na kusahau. Lakini tuliona jana walipokuwa wakijaribu kuonyesha mifugo wakichinjwa, tulilala fo fo fo bila wasiwasi wowote kwa sababu tunaona kuwa maisha yanaanza kuturudia. Ningependa kumuuliza Waziri, ninajua kuna kituo kimoja kule Lokichoggio, afungue kituo kingine katikati ya Turkwel na Kainuk ili tuwasaidie wafugaji wa Turkana na West Pokot. Anaweza pia kufungua vituo vingine kule Kaskazini Mashariki. Hatuna rasilimali nyingine kama mahindi ambayo yanakuzwa katika sehemu zingine za Kenya. Rasilimali yetu ni mifugo na ndio maana ninafurahi kuona vile Serikali inavyoshughulikia maslahi yetu. Tunajua kuwa maombi ya mnyonge yanaweza kujibiwa. Kwa hivyo, ni jukumu letu kuwaunga mkono na kuwapa moyo ili waendelee kuishi. Bw. Naibu Spika wa Muda, ingawa tunaipongeza Serikali, ni vizuri kuikosoa mahali ambapo imefanya vibaya. Kwa mfano, hali ya usalama katika nchi yetu imedhoofika. Hivi majuzi kulitokea hali ya taharuki juu ya wale ndugu wawili wa Kiarmenia. Hatujui walivyokuja hapa nchini na walifanya kazi gani. Hata hatukujua walivyofurushwa kutoka humu nchini. Bw. Naibu Spika wa Muda, mnamo tarehe 15 mwezi huu kuna jambo, ambalo hatujui lilipangwa na nani, lililotokea kule Chepsoina, Trans Nzoia. Jamii ya wafugaji walivamiwa na askari wa jeshi na polisi wakiandamana na askari kutoka nchi jirani ya Uganda. Askari hao walikusanya ng'ombe zaidi ya 500 ya wafugaji na kuwapelekea watu wa Uganda. Waliwaambia watu wa Uganda ni ng'ombe wao waliokuwa wamepotea. Sijui walitumia sheria gani kuchukua hatua kama hiyo. Ni watu kama hao ambao wanaweza kuitia dosari Serikali ambayo watu wanaifurahia. Utaona kwamba mtu anaamka na kuchukua hatua fulani bila idhini ya Serikali. Wakati mwingine watu wanasema Raisi anajua kuhusu hatua hii au ile. Lakini ninafikiri ni wazimu wa mtu fulani, ambaye anaamka na kusema anaweza kufanya jambo lolote. Kwa hivyo, ningependa kuungana na Wakenya wengine waliolaani vitendo vya watu ambao wanahujumu sera za Serikali kutoka ndani. Bw. Naibu Spika wa Muda, pia ningependa kuishukuru Serikali kwa kubuni hazina ya CDF. Miradi ya CDF imeanzishwa katika kila kona ya nchi. Pia kuna hazina ya Local Authorities Transfer Fund (LATF) ambayo inawasaidia wananchi. Pia ninaungana na wenzangu waliogusia hazina ya vijana. Ili hazina hii itumike vizuri ni lazima itumie mipangilio ya CDF. Hii ni kwa sababu katika kila sehemu ya uwakilishi Bungeni vijana wake wajulikana vizuri. Hatua hii pia itawezesha usawa katika ugawaji wa mali katika nchi hii."
}