GET /api/v0.1/hansard/entries/246561/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 246561,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/246561/?format=api",
"text_counter": 196,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kuwa kunipa nafasi kutoa mchango wangu kwa mjadala huu kuhusu Bajeti. Bw. Naibu Spika wa Muda, mengi yamezungumzwa kuhusu mambo ya elimu. Hata hivyo, ningependa kuongeza kwamba elimu ya msingi ambayo tunasema ni ya bure hapa nchini si ya bure. Hii ni kwa sababu Serikali inaigharimia. Kwa hivyo, tukisema elimu ya msingi ni ya bure bado hatuuambii ulimwengu ukweli. Ninegependa kupendekeza kuwa elimu ya msingi igharamiwe na Serikali. Pia ningeiomba Serikali kuunyosha mkono wake na kugharamia elimu ya malezi. Inafaa walimu wa shule za malezi walipwe na Serikali badala ya kulipwa na wazazi."
}