GET /api/v0.1/hansard/entries/246566/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 246566,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/246566/?format=api",
    "text_counter": 201,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kombe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 250,
        "legal_name": "Harrison Garama Kombe",
        "slug": "harrison-kombe"
    },
    "content": "Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kuwa kunitetea. Nilisema kwamba ingefaa Serikali igharimie pia elimu ya malezi. Hii ni kusema walimu wa nasari walipwe na Serikali ili kuwapunguzia gharama wazazi ndipo waweze kufurahia matunda ya Uhuru. Wakati huu imekuwa ghali mno kumsomesha mtoto katika shule ya malezi, kwa sababu karo yake 1462 PARLIAMENTARY DEBATES June 20, 2006 imefikia kiwango ambapo mzazi analipa Kshs300 kwa mwezi. Hii ina maana kuwa karo ya muhula ni Kshs900 na ya mwaka ni Kshs2,700. Katika mashambani kupata pesa kama hizi ni shida, kwa sababu hali ya uchumi imedidimia zaidi. Ninegependa kuongea juu ya elimu ya ufundi, hasa katika vyuo vya ufundi vijijini. Ni miaka mingi tangu shule hizi za, ufundi zilizobuniwa. Tangu zibuniwe, walimu wake wamenyanyaswa sana. Ni jambo la aibu kutamka pesa wanazolipwa. Wakati fulani nilimwuuliza Waziri anayehusika Swali kuhusu walimu hawa na akalieleza Bunge hili kwamba waalimu wa vyuo hivi hulipwa Kshs2,000 kwa mwezi, ingawa wana familia na watoto katika shule za sekondari na hata vyuo vya wastani. Hili ni jambo la kusikitisha sana. Ni muhimu waalimu hao kufikiriwa na kulipwa hata kama ni Kshs6000. Kiasi kama hiki kitawasaidia. Serikali inasisitiza sana elimu ya kiujuzi kwa vijana, lakini utaona kuwa si wengi wanaoweza kuhudhuria vyuo hivi kwa sababu kiwango cha karo kinachotozwa. Ningependekeza kuwa Wizara inayohusika na maswala ya vijana na ile inayosimamia elimu ya ufundi zishirikiane ili Serikali igharamie elimu katika vyuo vya ufundi. Zikifanya hivyo, vyuo hivyo vitaweza kutoa mafunzo bila malipo kwa wanafunzi. Wengi wa wanafunzi katika vyuo hivi huwa wamemaliza darasa la nane na kidato cha nne, ila tu huwa hawajafanya mitihani yao vizuri. Ikiwa tutafanya hivyo, itakuwa rahisi kwetu kutenga hela ambazo zitawafaidi vijana katika mipango yao ya kujitegemea. Kwa mfano, itakuwa rahisi kwa vijana kuunda makampuni kama yale ya ujenzi na kutumika katika miradi inayofadhiliwa na Hazina ya Maendeleo ya Mawakilisho (CDF). Sisi Wabunge tutaweza kuwapa kazi vijana wetu ambao watakuwa wametoka katika vyuo hivyo vya ufundi na ambao watakuwa wametengeneza makampuni yanayofadhiliwa na hazina ya vijana. Ikiwa Serikali itatilia maanani mambo haya, tutaweza kubuni nafasi nyingi za kazi kuliko zile laki tano tulizoahidiwa. Ninaamini tunaweza kubuni pengine kazi milioni moja kila mwaka kwa sababu vijana ambao watakuwa wameanzisha makampuni yao watawaajiri wenzao wengine. Katika upande wa kilimo, ningependa kutangaza hapa kwamba sisi watu wa Pwani tumechoka kutegemea chakula cha msaada kinachotoka kwa Serikali. Inafaa Serikali ibuni mipango kabambe ambayo itawasaidia watu wa Pwani ili waweze kuyanyunyizia maji mashamba yao. Hili likifanyika, watu wa Mkoa wa Pwani wataweza kukuza mazao na kujitegemea, badala ya kufadhiliwa na misaada wakati wote. Aidha, si Mkoa wa Pwani peke yake; hata sehemu za Ukambani ziko na shida. Ikiwa mipango ya kunyunyizia mashamba maji ingekuwepo, watu katika eneo la Ukambani wangeepuka maafa yanayotokana na kupelekewa mahindi ambayo yana vimelea hatari vya aflatoxin. Wanapokula mahindi hayo, watu wengi hupoteza maisha yao. Mahindi hayo huwa yamekaa zaidi ya miaka mitano katika maghala na huwa yameoza na kugeuka kuwa sumu hatari. Bw. Naibu Spika wa Muda, hivi ninavyozungumza, katika mawakilisho yangu, kuna lokesheni nne ambazo zina uwezo mkubwa wa kukuza mazao ikiwa tu Serikali ingeweza kuzifikiria na kuzipatia vifaa vya kisasa vya kunyunyizia mashamba maji. Nina hakika kwamba ikiwa Serikali italizingatia swala hili, basi Wilaya ya Malindi haitategemea tena misaada kutoka kwa Serikali. Hivyo basi, ningependa kuhimiza zaidi kwamba wakulima wa lokesheni za Bungale, Garashi, Dagamura, Chakama, Merikebuni, Jilore katika Wilaya ya Malindi waweze kutiliwa maanani ili wapewe vifaa vya kisasa vya kunyunyuzia mashamba maji. Kuhusu Hazina ya Maendeleo Katika Mawakilisho, kuna ile sheria iliyowekwa eti hakuna eneo Bunge ambalo litaruhusiwa kutumia fedha za CDF kununua matingatinga. Hicho kipengee ni kizuizi kwetu kwa sababu kinatufanya sisi kuwa waombaji wa chakula kutoka kwa Serikali. Ikiwa tutaruhusiwa kununua matingatinga, ninalihakikishia Bunge hili kwamba watu wa Magarini hawataomba chakula tena kwa sababu watatumia matingatinga hayo kulima. Aidha, itatuwia rahisi kutumia pesa za CDF kununua mashine ya kupiga maji na kuyanyunyiza shambani. Ni ombi langu kuwa turekebishe kipengee hicho katika sheria ya CDF ili tuwe na sheria June 20, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 1463 itakayotuwezesha kunufaisha watu wetu. Kwa mfano, tuwe na kipengee ambacho kitatuturuhusu kuwafaidi vijana moja kwa moja. Aidha, makundi ya akina mama yaweze kufadhiliwa na fedha za CDF. Kiwango kinachotengwa kwa ajili ya kugharamia elimu, yaani basari ya CDF, ni duni na hakiwezi kufaidi wanafunzi wote. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache ningependa kuunga mkono."
}