GET /api/v0.1/hansard/entries/246567/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 246567,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/246567/?format=api",
"text_counter": 202,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Commucations",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Naomba nichangie Hotuba ya Bajeti ya mwaka huu. Ilikuwa ni Bajeti yenye mema na maovu. Kwa kiwango fulani, ilimuinua maskini, lakini kwingineko ikamuangusha. Kabla sijazungumza juu ya upungufu wa Bajeti hii, ningependa kwanza kabisa kuipongeza Serikali kwa kutotilia maanani pesa za wafadhili wa kigeni katika Bajeti ya mwaka huu. Kama Serikali hii ingefanya hivyo, basi ingelikosea sana kwa sababu hakuna pesa zinazotolewa na wafadhili bila masharti. Masharti hayo yametufanya kuwategemea wageni sana kiasi kwamba mabalozi wa kigeni wakipiga chafya, nchi nzima inapata homa. Balozi akisema neno fulani na Rais aseme lake, magazeti yetu yatayaangazia maoni ya balozi kwa sababu ya pesa zao. Hata tatizo la mamluki limeletwa na ugonjwa wetu wa kuabudu pesa na wageni. Mgeni akisema ana pesa, tutamfuata hadi jehanamu. Ninampongeza Waziri wa Fedha kwa kutozingatia pesa za wafadhili katika Bajeti yake. Kwa kuzipa kisogo pesa hizo anastahili pongezi zetu. Natumai ya kwamba Serikali itafuata nyayo hizo ili tuweze kujikomboa kutokana na minyororo ya wageni na wafadhili. Bw. Naibu Spika wa Muda, nashukuru Serikali kwa kuondoa ushuru na kodi zinazotozwa bidhaa kama unga wa ngano na taulo zinazotumiwa na akina mama wakati wa hedhi. Hiyo ni hatua nzuri ambayo inastahili kuungwa mkono. Lakini kuondoa kodi hakutoshi ikiwa bei ya bidhaa hizo haitapunguzwa. Bajeti ya mwaka jana ilipendekeza ushuru huo kuondolewa, lakini bei haikupungua kwa sababu Serikali iliwaachia wafanyabiashara wateremshe bei. Wao walipuuza pendekezo la Bw. Waziri na bei ikabakia kama ilivyokuwa hapo awali. Waliamua kuchukua kiasi kilichopunguzwa wakakiweka mifukoni mwao kama faida, nayo bei ikabaki ndoto mpaka leo. Kwa hivyo, ninatumaini ya kwamba mhe. Kimunya atakuwa amejifunza jambo kutokana na mapungufu yaliyomtangulia Bw. Mwiraria. Kama tulitaka hii Bajeti isaidie maskini, haingekosa kupandisha kiwango cha mshahara wa chini kwa wafanyakazi wetu. Ule mshahara wa chini tunaolipa wafanyakazi wetu bado ni kidogo sana na unastahili kuinuliwa. Pia, ni muhimu tuhakikishe tumeongeza nafasi za kazi ili maskini waone kwamba wanashughulikiwa na Serikali yao. Bajeti nzuri ni ile ambayo inasaidia maskini. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo lingine ambalo Bajeti ingezungumzia ni kuthibiti bei; kurudisha ule uthibiti wa bei ambao tulikuwa nao zamani. Lakini Waziri hakufanya hivyo na kwa hivyo, kwa kiwango kikubwa, Bajeti hii inabaki ni ya matajiri. Ni hao peke yao ndio wanaweza kushindana na bei hizi. Wale wadogo kule chini hawazimudu bei ambazo zinapanda karibu kila siku. Kwa bahati mbaya, utapata wafanyabiashara wameachiwa uhuru mwingi sana wa kuamua ni lini wapandishe bei, na kwa kiasi gani, na hakuna wakati bei zinaanguka; zinakuwa ni kupanda, kupanda, mpaka sasa zinakaribia kilele cha mlima Kilimanjaro au mlima Kenya. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo lingine ambalo ningetaka kugusia ni kwamba Wilaya ya Nakuru imepewa pesa kidogo sana za barabara. Ninashindwa kwa nini Nakuru inaendelea kubaguliwa. Sisi ndio tuna wapigakura wengi sana kuliko wilaya zingine zote. Wilaya hii imenyimwa hata Waziri ingawa wapigakura wa Nakuru ndio walikuwa mstari wa mbele katika kuchagua hii Serikali. Wakati kazi zinatolewa serikalini, wilaya ya Nakuru---"
}