GET /api/v0.1/hansard/entries/246569/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 246569,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/246569/?format=api",
"text_counter": 204,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Lakini Waziri Msaidizi hana chochote! Tunataka Waziri mwenyewe kwa sababu tunatosha. Wakati kazi zinatolewa, ni vigumu Wilaya ya Nakuru kupewa chochote. Hatuwezi kusema tumepewa hata 1464 PARLIAMENTARY DEBATES June 20, 2006 balozi mmoja au katibu mkuu, au mkurugenzi katika kampuni yoyote ya umma. Hatupewi! Tunauliza, kama hii Serikali haipatii wakaaji wa Nakuru chochote, ni Serikali gani ambayo itakuja itupe? Rais mstaafu Moi alitunyima. Serikali hii nayo inatunyima; tunatakiwa tungojee Serikali gani ndio ije kukumbuka watu wa Nakuru? Hili ni swala ngumu ambalo ni lazima lifikiriwe. Bw. Naibu Spika wa Muda, Bajeti hii pia imesahau ya kwamba kuna wakaazi wengi sana wa Mkoa wa Bonde la Ufa ambao walifukuzwa kutoka kwa mashamba yao, wakachomewa manyumba. Ukiangalia pesa ambazo wametengewa za kuwasaidia kupata mashamba na makao tena, hazitoshi hata kidogo; ni Kshs400 milioni peke yake. Tunashindwa hizo pesa zitanunua mashamba mangapi. Kuna maelfu na maelfu ya watu katika Mkoa wa Bonde la Ufa ambao walifukuzwa kwa mashamba yao. Serikali hii iliapa ya kwamba itawasaidia kuwarudisha kwa mashamba yao. Sasa Serikali hii inasoma Bajeti yake ya mwisho na haijafanya kitu chochote. Watu hawa watakuja kupatiwa mashamba na nani? Hili ni kosa ambalo haliwezi kusameheka kwa sababu ni kosa kubwa! Tunaongea kuhusu watu ambao wamekuwa wakimbizi katika nchi yao, na naona kuwa Waziri Msaidizi, Bw. Kenneth, hasikizi ninavyosema. Hawa ndio wangetoa pesa za kusaidia watu hawa. Watu hawa wasiposaidiwa na Serikali hii, mwaka ujao ukifika tutawaambia watupigie kura ili tukirudi Bunge tuweze kuwatafutia mashamba? Hivyo ndivyo tutakwenda kuwaambia? Nasikia kuwa wale ambao wamepangiwa kupewa mashamba kwanza ni wale ambao wanajua vita; wakaazi wa Likia. Inasemekana kuwa hawa ndio watakuwa wa kwanza kupewa mashamba. Sasa nauliza hivi: Hadi wakazi wengine wa Bonde la Ufa watoe fujo, waandamane, wapigane na Serikali ndio Serikali ione haja ya kuwapa mashamba? Hili ni kosa kubwa ambalo linahitaji kushughulikiwa na Serikali kwa sababu kama haikushughulikia jambo hili, nani mwingine atalishughulikia? Bw. Naibu Spika wa Muda, nilisikia kwamba kuna ujumbe uliotoka Norway na pesa kusaidia watu hawa kwa kuwatafutia mashamba. Walipoingia katika Ofisi ya Rais, waliambiwa kuwa Kenya hakuna watu wasiokuwa na makao. Hili ni swala ambalo haliwezi kuchezewa tena! Lazima lishughulikiwe au sivyo, tunafanya kazi ya bure tu."
}