GET /api/v0.1/hansard/entries/247427/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 247427,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/247427/?format=api",
    "text_counter": 285,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Awori",
    "speaker_title": "The Vice-President and Minister for Home Affairs",
    "speaker": {
        "id": 290,
        "legal_name": "Moody Arthur Awori",
        "slug": "moody-awori"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, nasimama hapa vile vile kuunga mkono Mswada huu kwa sababu ni wa maana sana. 1290 PARLIAMENTARY DEBATES June 13, 2006 Nimefurahi sana kwa kuwa nazungumza kama mwenzangu aliyeuwasilisha Mswada huu. Kusema kweli ni lazima tuupitishe Mswada huu kwa sababu ya mambo mengi. Jambo la kwanza, tunataka usaidizi kutoka kwa wadhamini ambao wanatoka upande wa Ulaya na walitaka sana tuunganishe mambo mawili ili tuweze kuendeleza mipango ya makavazi katika nchi hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, Mswada huu utatusaidia ili tuweze kuhifadhi vitu vingi sana hasa upande wa mkoa wa Pwani kama vile Mhe. Balala alivyosema. Kusema kweli, ukiangalia historia ya nchi hii, majengo mengi sana ya kihistoria yako upande wa Pwani na tunataka tuwe na sheria ya kutosha ambayo itakataza, kwa mfano watu wa Lamu ambao ni walafi na wenye haja ya pesa tu kuharibu majengo ambayo yalijengwa miaka mingi iliyopita. Ningependekeza kwamba ye yote ambaye ana mali huko ambayo ni ya umma ichukuliwe kwa sababu hatuwezi kupoteza hii mali ambayo itasaidia vizazi vijavyo. Wahenga walisema: \"Yule ambaye hana mila ni mtumwa\" na hili ni jambo ambalo tunataka tulifikirie na tulikumbuke. Bw. Naibu Spika wa Muda, vile vile katika nchi hii tuko na watu wengi sana ambao walichangia ujenzi wa taifa hili kutoka miaka mingi iliyopita na tunataka sasa tuweze kuwa vile vile na pesa ambazo zitaweza kutusaidia tuone kwamba wale mashujaa waliokuweko, vitabu vyao na vitu vingine viweze kuwekwa katika makavazi katika sehemu hii. Hii itatuwezesha kuwa kama taifa moja ambalo linatoka mahali pamoja. Kwa hayo machache, naunga mkono Mswada huu."
}