GET /api/v0.1/hansard/entries/248619/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 248619,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/248619/?format=api",
    "text_counter": 132,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Broadcasting",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika. Ninaomba kutoa mchango wangu kwa Hoja hii inayopendekeza tutafute namna nyingine ya kuimarisha vita dhidi ya ufisadi katika nchi hii. Ningependa kusema kwamba mpaka sasa, vita dhidi ya ufisadi vimekwama. Ninasema hivyo kwa sababu, ukiangalia hali ilivyo, utaona kwamba hakuna chochote kinachoendelea. Kwa kweli, ni kama tumepoteza vita dhidi ya ufisadi. Serikali, mahakama na Bunge, pamoja na wananchi, wamepoteza vita dhidi ya ufisadi. Kwa hivyo, tunakubali kwa moyo mkunjufu msaada wowote ambao tutapata kutusaidia katika vita hivi. Bw. Naibu Spika, ufisadi ni \"ukoma\" mbaya kuliko ule ugonjwa wa ukoma, kama tunavyoujua. Wafisadi ni wagonjwa wa ukoma. Katika Biblia, tunaambiwa kwamba, katika enzi za kale, wagonjwa wa ukoma walitengwa kutoka wa jamaa zao. Hawakuruhusiwa kuishi na jamii. Lakini ukiangalia katika nchi hii, utaona kwamba wafisadi wanakubalika sana. Ningependa 1036 PARLIAMENTARY DEBATES May 31, 2006 kuwaomba wale wanaohusika na shughuli ya kuunda Kamati mpya za Bunge wasiwateue watu waliohusika na ufisadi, ama wale waliotajwa kwenye kashfa za ufisadi, kuwa wanachama wa kamati hizo. Nchi za kigeni zimeanza kupiga marufuku Wakenya ambao wamehusishwa na visa vya ufisadi wasitembelee nchi zao. Serikali za nchi hizo zinapiga marufuku watuhumiwa wa ufisadi wasizitembelee nchi zao kwa sababu wanaogopa kwamba wakienda huko watawaambukiza watu wao ukoma wa ufisadi. Lakini katika nchi hii, wafisadi wanatembea huru kama ambao hawana dosari. Kwa sababu tumeweza kufikia kiwango hicho, ni wazi kwamba tumepoteza vita dhidi ya ufisadi. Ni kana kwamba Wakenya hawaogopi kuambukizwa ufisadi. Hatuwanyanyapai wafisadi hao. Hatuwatengi, hatuwabagui ama kuwaogopa. Badala yake, tunakula na kunywa pamoja nao. Tunalala nao na kuzaa nao. Tunazaa ufisadi zaidi. Katika nchi hii, wafisadi hugombea viti vya uwakilishi Bungeni. Hawana aibu. Utaona kwamba mtu ametajwa katika hujuma ya ufisadi, lakini bado anagombea kiti cha uwakilishi Bungeni. Wengine wanagombea kiti cha Urais. Ukiona mtu aliyetajwa kwenye kashfa ya ufisadi anathubutu kugombea kiti cha Urais na hakuna mtu wa kumkemea, ni thibitisho kwamba nchi yenyewe imeungua. Katika nchi hii, wafisadi wanagombea uongozi wa vyama vya kisiasa. Pia wanaenda Ikulu ya Rais. Tunashindwa kufahamu wafisadi hao wanaenda Ikulu ya Rais kufanya nini. Ikulu ni pahali patakatifu; sio pango la walanguzi. Inawezekanaje mtu aliyehusishwa na ufisadi kumtembelea Rais katika Ikulu? Anaenda huko kufanya nini? Tuko na kasoro kubwa!"
}