GET /api/v0.1/hansard/entries/248621/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 248621,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/248621/?format=api",
    "text_counter": 134,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika, nimeongea kuhusu watu ambao wamehusishwa na ufisadi. Sikumtaja mtu yeyote. Kama mhe. Ndolo hawajui, mwenye macho haambiwi \"tazama\". Uoga wangu mkubwa ni kuwa Rais anawaruhusu watu ambao wamehusishwa na ufisadi kumtembelea katika Ikulu. Watamuweka dosari. Ni lazima Rais siku moja asimame hadharani aseme: \"Ikulu ni pahari patakatifu. Siyo pango la walanguzi. Sitaki kuona mhalifu yeyote akikaribia hapa\". Watu ambao wametajwa katika ripoti za kamati ambazo zinachunguza ufisadi na waliopendekezwa kutoshikilia nyadhifa za umma, wanaendela kufanya hivyo. Hapa kuna kasoro kubwa. Wafisadi wamejaa Serikalini; kwa mfano, wako katika polisi na katika utawala wa mikoa. Bw. Naibu Spika, katika mashambani, ufisadi umejaa tele. Uchumi wetu, siasa na utawala zimetekwa nyara na ufisadi. Kila pahali, ufisadi unatawala. Huduma zinacheleweshwa kwa sababu ni lazima watu watoe hongo ili wapate huduma hizo. Hata makanisani, ufisadi umejaa. Ufisadi unaripotiwa kwa Kenya Anti-Corruption Commission (KACC) lakini hakuna hatua ambayo inachukuliwa. Walanguzi wanaendelea na ufisadi na huku tunapigana na ufisadi. Ni kama tunaogopa kuwafunga watu ambao wamehusika na ufisadi. Serikali ya NARC iko karibu kumaliza kipindi chake, lakini sijui itasema nini kama haitakuwa imewahukumu watu ambao wamehusishwa na ufisadi? Waliokulia sahani ya ufisadi na waliofaidika kutokana na ufisadi sasa ndio mabingwa wakubwa wa kupigana na ufisadi. Wanazunguka kote nchini wakisema vile ufisadi ulivyo mbaya. Tukifikia kiwango ambacho watu ambao wamehusika na ufisadi wanajifanya mabingwa wa kupigana na ufisadi, hiyo ni ishara kwamba tumevipoteza vita dhidi ya ufisadi. Bw. Naibu wa Spika, watu wengi wanafikiria kwamba kupigana na ufisadi ni kile Waswahili wanakiita \"lele mama\". Ni maoni yangu kwamba kama vita vya wenyewe kwa wenyewe havijatangazwa katika nchi hii, hatupigani na ufisadi wo wote. Vita vya kuondoa ufisadi sio mchezo. Ni vita ambavyo vitatingiza nchi hii. Kama nchi hii bado haijatingizika, vita vya kuondoa ufisadi bado havijaanza. Sijui ni nani atavianzisha vita hivi. Ufisadi umeshinda katika nchi hii. Kilele cha ushindi huu ni namna ambavyo wananchi wanavyotambua wafisadi kama mashujaa wao. Ukihudhuria mkutano wa hadhara, uwe wa siasa au May 31, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 1037 mazishi, utaona kwamba watu ambao wamehusishwa na ufisadi wakisimama, wanapigiwa makofi kwa deremo. Wafisadi wamekuwa ndio mashujaa wa raia. Kila siku tunasema kuwa tunapigana na ufisadi lakini wafisadi wamekuwa mashujaa wa wananchi. Tutapigana vipi na ufisadi kama wananchi wanashangilia wafisadi? Kuna kitu ambacho kimeenda kombo. Wananchi hawawezi kuwatambua wafisadi kama mashujaa kama hatujapoteza vita vya kuondoa ufisadi. Tumepoteza vita vya kuondoa ufisadi na wananchi wanawafuata wafisadi ili wawapatie watakachowapatia. Bw. Naibu Spika, tumo katika hali baya. Ni lazima tushinde vita hivi kama nchi hii itaweza kupigana na umaskini na kujikomboa kwa kila hali. Ufisadi hauadhiri tu maendeleo. Unaadhiri pia siasa. Ni lazima tukumbali kwamba ufisadi umepiga hatua kadhaa mbele ya wale ambao wanapigana nao. Ni lazima tukumbali kuunda Kamati hii ili iongezee nguvu katika vita vya kumaliza ufisadi katika nchi hii."
}