GET /api/v0.1/hansard/entries/248631/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 248631,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/248631/?format=api",
"text_counter": 144,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Ndolo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 222,
"legal_name": "Reuben Owino Nyanjiga Ndolo",
"slug": "reuben-ndolo"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii niunge mkono Hoja hii. Hii ni kwa sababu swala la ufisadi limekita mizizi katika nchi yetu. Hoja hii imewasilishwa wakati unaofa. Waziri wa Haki na Maswala ya Kisheria alisema jana kuwa ufisadi ni swala nyeti katika nchi yetu. Pia Serikali ilisisitiza kwamba ni lazima kuwe na tume maalum ya kushughulikia maswala ya kuchunguza na kupeleka kortini mashtaka ya ufisadi. Ni jambo la kushangaza sana ikiwa Serikali wakati huu inageuka na kusema kwamba kamati ambayo tunataka kubuni hapa leo itakuwa inakariri kazi ya Kamati zingine za Bunge na tume tofauti zilizoundwa kushughulikia ufisadi nchini. Ikiwa Serikali inataka kubuniwa kwa tume ya kuchunguza ufisadi, kwa nini leo inapinga Hoja hii na kusema kamati hii itakariri kazi ya kamati zingine? Bunge hili ndilo kitovu cha kutunga sheria katika nchi yetu. Kwa hivyo, inafaa mambo ya ufisadi yachunguzwe vilivyo na Bunge hili. Bw. Naibu Spika wa Muda, vita dhidi ya ufisadi vinahitaji sisi sote kushiriki. Si Bunge tu, wala Serikali pekee, bali wananchi wote kwa jumla, kupitia kwa Wabunge wao. Ni lazima sote 1042 PARLIAMENTARY DEBATES May 31, 2006 tutilie maanani jambo hili. Jambo la kustaajabisha ni kwamba watu ambao wanachunguza ufisadi nchini hawalipwi vizuri. Lakini watu wanaohusika na visa vya ufisadi wana pesa nyingi zaidi. Je, inawezekanaje mtu ambaye anapata mshahara wa chini kuchunguza visa vya ufisadi? Je, mtu huyo atachunguza ufisadi bila kuhongwa? Uchunguzi utafanyika vipi? Kwa hivyo, ningependa kuunga mkono kabisa Hoja hii na kusema kwamba ni lazima kamati hii ibuniwe ili tuone kwamba wafisadi wote wamechunguzwa na kuchukuliwa hatua madhubuti. Hii ndio sababu wanapinga Hoja hii kwa sababu sisi tunawajua wafisadi wote. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni kweli tuna Kamati za PIC na PAC. Lakini ni wafisadi wangapi ambao wametajwa katika ripoti hizo wamefikishwa kortini? Hakuna hata mmoja ambaye amefikishwa kortini. Wenye kufikishwa kortini ni wale ambao wameiba kuku na pesa za thamani ya chini. Hao ndio tunaoambiwa ni wafisadi. Wafisadi wanaohusika kwa kuiba pesa nyingi wanashirikiana na viongozi kuona kuwa swala la ufisadi halitashughulikiwa kikamilifu na Serikali hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninamuunga mkono Waziri wa Haki na Maswala ya Kisheria kwa kazi yake nzuri. Itakuwa ni aibu sana ikiwa yeye atapinga Hoja hii. Hoja hii itamsaidia kupambana na visa vya ufisadi nchini. Ikiwa Waziri ataungana na watu ambao wanataka kuona ufisadi ukiendelea, basi itakuwa ni hatari sana. Tutarudi nyuma kimaendeleo na hatutaweza kuwapeleka kortini wafisadi. Bw. Naibu Spika wa Muda, siwezi kusema kwamba hakuna wafisadi katika Bunge hili. Waziri amesema ufisadi umekita mizizi katika nyanja zote za nchi. Ni kweli vita dhidi ya ufisadi ni vigumu sana. Kwa hivyo, ni lazima Bunge hili lijishughulishe na swala hili la ufisadi kikamilifu. Hii ni kwa sababu swala hili limekita mizizi katika Bunge na Serikali yetu. Wakati Serikali ilibuni tume ya KACC inayoshughulikia maswala ya ufisadi, nilienda kortini kupinga uteuzi wa Jaji Ringera. Hii ni kwa sababu yeye alikuwa ameshtakiwa kuhusika na visa ya ufisadi. Nilisema hastahili kusimamia tume ya kupambana na ufisadi nchini. Tukiendelea kufanya kazi kwa njia hii, hatutaweza kufaulu dhidi ya ufisadi. Ningependa kumuomba Waziri arudi nyuma afikirie juu ya swala hili na aunge mkono kubuniwa kwa kamati hii. Kuna watu wanaodhani kwamba watakaoteuliwa watajifaidi wenyewe. Hiyo si kweli. Ninaunga mkono mhe. Mbunge ambaye aliwasilisha Hoja hii kwa sababu ana roho nzuri ya kusaidia nchi hii katika mambo ya ufisadi. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaiunga mkono Hoja hii kwa dhati. Ningemwomba Waziri atusaidie na aunge Hoja hii mkono ili kamati hii ibuniwe ili imalize ufisadi hapa nchi."
}