GET /api/v0.1/hansard/entries/249311/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 249311,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/249311/?format=api",
"text_counter": 38,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wario",
"speaker_title": "The Assistant Minister, Ministry of State for Special Programmes",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": ", walikutwa katika hali ya kutojiweza. Sio nchi, wizara au halimashauri ambayo ina uwezo wa kutatua matatizo ya jangwa la kiasili. Hata hivyo, juhudi za Shirika la Msalaba Mwekundu ni nzuri. Wameg'ang'ana mara nyingi kunapotokea kwa dharura gharika ya kiasili. Mara nyingi wamefika mahali hapo na kusaidia Wakenya. Wanastahili kupongezwa. Bw. Naibu Spika, juzi kumetokea mafuriko. Wakati huo, maswala yanayohusiana na September 19, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 4015 jangwa yalikuwa katika Wizara yetu. Tulikimbia kwenda kuokoa maisha ya watu. Tulipofika mahali ambapo mzee fulani aliyekuwa na mbuzi - alituambia: \"Iwapo nyinyi mmekuja na helikopta na hamtambeba mbuzi wangu, mniache nife hapa.\" Haya ni maswala mazito kuliko vile tunavyoyachukulia wakati huu. Ni heri kuwepo na rasilmali na itengwe, ili kila Wizara iwe na mipango maalumu ya kushughulikia gharika. Lakini tukisema kwamba kutakuwa na halimashauri moja, hata iwe na ndege au pesa, sioni kama hiyo itakuwa suluhisho kwa sababu nchi nzima, kila Wizara katika Serikali inafaa iwe na kitengo cha kushughulikia jangwa la kiasili. Kwa hayo machache, ninasema asante."
}