GET /api/v0.1/hansard/entries/249313/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 249313,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/249313/?format=api",
    "text_counter": 40,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, asante sana. Nafikiri kuwepo kwa mamlaka ya kupambana na majangwa ambayo yanatokana na hali ya kimaumbile ni muhimu sana. Katika dunia ya leo hamuwezi kukaa tu halafu mfikirie eti, mtatatua mambo yote na hulka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ametupa akili na tunaishi duniani. Binadamu ana uwezo wa kujipanga hata ingawa majangwa ya kiasili ni magumu sana. Kwa mfano, hivi sasa, kuna jiwe kubwa sana ambalo limeanguka katika mji wa Peru na kuleta mambo mengine mapya kabisa. Mambo ya hulka ambazo zinatoka mbinguni zinaanguka hapa duniani. Lakini binadamu lazima awe na uwezo wa kujipanga kwa majangwa. Miaka nenda, miaka rudi, tumeona watu wakiuliwa kule Budalangi kwa mafuriko ya maji. Ikiwa tutajitayarisha kwa mambo hayo na kuwa na mamlaka halisi, tutaendelea kujipanga nayo. Tunajua kwamba magonjwa kama UKIMWI ni majangwa ambayo tukijitayarisha na kukabiliana nayo vizuri, kulingana na maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia ambayo binadamu ameweza kuwa nayo, tunaweza kupambana nayo na kujitayarisha kupambana na majangwa mengine. Lakini mambo hayo hayawezi kutokea kwa bahati tu. Hatuwezi kungojea majangwa yaje halafu tushtukie kama ilivyotokea wakati tulipigwa bomu hapa na maharamia wa kimataifa. Tulishtuka kwa sababu ilitokea kwa ghafla na hatukujua tutafanya nini. Bw. Naibu Spika, lazima tuwe na mpango halisi. Na mimi ninaona ya kwamba, ili kupambana na majangwa, ni muhimu kupitisha hapa Bungeni Mswada na sheria kama hiyo, ili tuunde taasisi maalum ambayo itajifundisha kutoka pahali pengine duniani ambapo kumetokea majangwa, ili endapo jangwa litatokea, tuwe tayari. Tukiwa tayari, hata kama majangwa ni magumu sana--- Kwa sababu mengine hayawezi kuzuiliwa kisayansi au kiteknolojia. Tumeona majangwa kule Marekani na Japan ambapo kuna teknolojia ya hali ya juu, lakini wameshindwa kukabiliana nayo. Lakini, haidhuru, tutakuwa tayari zaidi na hatutakuwa tunaamka kama watu ambao hatuishi dunia ya leo ambapo sayansi na teknolojia iko juu. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}