GET /api/v0.1/hansard/entries/250192/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 250192,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/250192/?format=api",
"text_counter": 367,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Kituyi",
"speaker_title": "The Minister for Trade and Industry",
"speaker": {
"id": 293,
"legal_name": "Mukhisa Kituyi",
"slug": "mukhisa-kituyi"
},
"content": " Nilikuwa nasema kwamba katika desturi za kidemokrasia, watu huwasiliana na kusema sababu za kubadilisha Hoja. Nimemsikiliza Bw. Sirma akileta mambo juu ya Mswada wa CDF. Moja ya sababu zilizowasilishwa na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni ni kwamba tunahitaji kwenda likizo, ili wafanyikazi wa Bunge na sisi waheshimiwa Wabunge tujihusishe na mkutano wa IPU. Ingawa waheshimiwa Wabunge watahudhuria mkutano huu kwa muda wa wiki mbili tu, ukweli ni kwamba wafanyikazi wa Bunge ambao watakuwa wakisaidia katika mkutano huu watahitaji muda fulani wa kupumzika kabla ya May 4, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 975 kurejea hapa Bungeni kwa shughuli za Bajeti. Hatufai kurudi mapema kwa sababu sisi huja hapa kuongea, kujadiliana na kutukanana. Tunafaa kuwafikiria wafanyikazi wa Bunge hili ambao wanahitaji kupumzika kwa muda fulani ili waweze kuendeleza kazi zao katika Bunge hili."
}