GET /api/v0.1/hansard/entries/250196/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 250196,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/250196/?format=api",
"text_counter": 371,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Kituyi",
"speaker_title": "The Minister for Trade and Industry",
"speaker": {
"id": 293,
"legal_name": "Mukhisa Kituyi",
"slug": "mukhisa-kituyi"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, sikusema tunakuja hapa Bungeni kutukanana. Nilisema tuna mazoea, tukija hapa kujadiliana, wakati mwingi tunatukanana. Nimesema mazoea yetu mabaya yatarejea tukirudi hapa Bungeni. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna mambo kama ya CDF ambayo yametajwa hapa. Ni muhimu Wabunge wawe na muda baada ya kongomano la IPU kujadiliana pamoja faraghani ili wasuluhishe maswala nyeti ambayo sio vizuri tuyajadili hapa. Kila mhe. Mbunge anaelewa ninayoyasema. Kwa hivyo, hakuna maana kuharakisha kufunguliwa kwa Bunge kabla ya sisi kujadiliana faraghani ili tuweze kutekeleza kazi yetu ipasavyo. Sioni sababu ya sisi kujaribu kugeuza Hoja hii mwafaka. Desturi ya Bunge hili ni kwamba huwa tunaenda likizo kwa muda wa wiki tatu au nne kabla ya Waziri wa Fedha kuwasilisha Bajeti hapa. Wakati huu tunataka tufunge mapema ili turudi mapema. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo mengi, naomba kupinga Hoja ya kurekebisha Hoja ya Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni."
}