GET /api/v0.1/hansard/entries/250433/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 250433,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/250433/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, asante kwa kunipa fursa hii ili nichangie Hoja hii. Ninaiunga mkono nia ya Hoja kikamilifu. Nia ya Hoja hii ni kujaribu kuhakikisha ya kwamba wananchi wetu wamefaidika kutokana na sekta ya kawi. Ikiwa bei ya mafuta ya taa imekaribia bei ya diseli, basi watu wengi wanaotumia mafuta taa wanaumia sana. Watu wengi hutumia mafuta taa sana katika matumizi ya kila siku. Hata hivyo, ni wenye magari ambao wanafaidika kutokana na bei ya juu ya mafuta. Hii ni kwa sababu bei ya diseli na petroli ni karibu sawa na ile ya mafuta ya taa. Nia ya kuona kwamba ushuru umepunguzwe ili wananchi wetu wafaidike ni ya busara sana. Hofu kubwa ni katika utekelezaji wa Hoja hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, watu wengi wameanza kuzungumza kuhusu madhara ya soko huru. Soko huru ni mpango ambao sisi tunauthamini kama vipofu bila kuelewa ni nini tunafanya. Sisi tunataka ubinafsishaji wa mashirika yetu uendelee. Hata hivyo, tunaendelea kuyapiga vita mashirika yetu kila siku, hasa Shirika la Petroli la Kitaifa. Hii ni kwa sababu Benki ya Dunia imetuagiza kubinafsisha mashirika yetu. Mojawapo ya suluhisho kubwa ni kuimarisha Shirika la Petroli la Kitaifa. Kama taifa, uchumi wetu utaendelea kukua iwapo tutayaimarisha mashirika yetu. Tunahitaji sekta ya ubinafsishaji lakini sekta hii haiwezi kunawiri bila sekta ya umma. Tatizo kubwa ni kwamba Serikali imeshindwa kusimamia mashirika ya kitaifa yanayouza petroli na mafuta ya taa kila pahali. Sisi Wabunge tukiunga mkono ubinafsishaji wa mashirika hapa nchini, tunafikiri hilo ni suluhisho. Hatuwezi kupata suluhisho hilo. Hata nchi hii ikipata mafuta katika Wilaya ya Lamu, wananchi wetu hawatafaidika kwa sababu ya sera ya ubinafsisaji. Mfano mzuri ni nchi ya Nigeria. Mpaka sasa nchi ya Nigeria ina mafuta mengi lakini wananchi wake hawafaidiki kwa sababu wanafuata sera ya kibepari. Nchi hiyo inanyonywa na mashirika ya kimataifa. Wananchi wake wana shida kabisa ya mafuta. Nchi ambayo inajali maslahi ya maskini na watu wake, inafaa kuimarisha sekta za umma katika kusimamia ushuru. Mfano ni nchi ya Venezuela. Wakati Bw. Chavez aliteuliwa kama Rais wa nchi hiyo, Serikali ya Venezuela ilianza mara moja kusimamia mafuta yake. Wananchi wa Venezuela wameanza kufaidika kutoka kwa mafuta yao na hata kuzifaidi nchi zingine za Latin America kama Cuba. Serikali ya Bolivia nayo inasimamia gesi. Bila kusimamia rasilmali kuu za kitaifa, hatuwezi kuendelea. Tukipata mafuta Lamu ama pahali pengine katika Mkoa wa Pwani, hii italeta vita zaidi ikiwa tutaendelea na sera za ubinafsishaji. Bw. Naibu Spika wa Muda, ikiwa tutapitisha Hoja hii ni lazima tuwe na mikakati kamili ya kuhakikisha ya kwamba kodi itakayopunguzwa itawasaidia watu wetu ambao hawajiwezi kiuchumi. Tunajua kwamba Bajeti ya mwaka jana ilipendekeza bei ya bidhaa fulani zipunguzwe ili wananchi wetu wafaidike. Hata hivyo, bei ya bidhaa hizo haijapunguzwa. Tukiendelea hivi, hata tukipunguza kodi tutaendelea kuwafaidi mabepari wanaomiliki makampuni ya kimataifa. Ni lazima tufikirie mikakati na sera zetu za kiuchumi. Ni lazima tuimarishe sekta za Serikali na za ubinafsisaji. Tusitumie uimarishaji wa uchumi kiholela ili kuangusha sera za Serikali. Tukifanya hivyo, Serikali itakuwa ikilalamika na tutakuwa tumeivunja nguvu. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninakubalina na Bw. Ochilo-Ayacko kwamba moja ya suluhuhisho ni kuimarisha Shirika la Petroli la Kitaifa ili liwe linaendelea kununua petroli kutoka Iran na nchi zingine, pia liweze kushindana na sekta zingine za kibinafsi. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, naunga Hoja hii mkono."
}