GET /api/v0.1/hansard/entries/251042/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 251042,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/251042/?format=api",
    "text_counter": 251,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. M.Y. Haji",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 26,
        "legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
        "slug": "yusuf-haji"
    },
    "content": "Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi niuchangie huu mjadala. Huu mjadala ni muhimu sana, na hili ni jambo ambalo ni lazima tulijadili kwa makini. Mambo ambayo yametokea katika miaka michache iliyopita ni mazito. Hata ingawa sisi ni wanyama, mwenyezi Mungu ametupa akili ya kuweza kutofautisha mazuri kutoka mabaya. Ni jambo la kusikitisha sana kuona watu wakifanya mapenzi na watoto wa umri wa miezi mitatu au May 2, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 835 sita; hii ni kinyume na hata tabia ya wanyama. Hata mnyama hawezi kutamani mtoto mchanga hivyo kimapenzi. Kwa hakika mambo yanayofanyika wakati huu ni kinyume na maadili ya mwafrika na ya dini zote. Katika dini ya kiislamu, mtu ambaye ameowa akifanya mapenzi na mwanamke mwingine kwa nguvu anapigwa mawe hadi kufa. Ni vigumu katika dini ya kiislamu kutoa ushahidi wa mtu anayefanya mapenzi kwa nguvu. Ni lazima kuwe na mashahidi wanne. Kwa kawaida watu wanaofanya maovu kama haya hawayafanyi mbele ya watu. Huwa wanayafanya kisiri siri. Kwa ujumla, ninapendekeza watu kama hawa waadhibiwe vikali. Ingekuwa vizuri tuwe na adhabu tofauti kwa wanaowanajisi watoto na wanaowanajisi watu wazima. Mtu anayemnajisi mtoto wa miezi sita au mwaka mmoja hafai kuishi katika dunia hii. Kama Mswada huu ungeweka adhabu ya mtu kama huyo kuawa, ingekuwa vizuri zaidi. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna mambo kadhaa ambayo Mswada huu ungeshughulikia. Mswada huu hauzungumzii usenge na ushoga. Haya ni makosa ya kimapenzi. Ninasikitika kuona kwamba Mswada huu unataka mtu anayemnajisi mwanaume mwingine apewe kifungo cha miaka 21, na anayemnajisi mwanamke afungwe maisha. Huu si uadilifu hata kidogo. Ningependa kufanywe mabadiliko ili yeyote anayemnajisi mwanaume au mwanamke afungwe maisha. Pia kuna mambo ya ushawishi wa akina dada. Watu wameacha desturi na mila zetu. Mkuu wa Sheria aliongea juu ya mwanamke Mkisii wa miaka 90. Alisema mwanamke huyo alisema zamani walikuwa wakitembea uchi na hawakushikwa na wanaume. Sasa ni lazima tujiulize kwa nini wakati huu mambo kama haya yanafanyika katika jamii. Mambo haya yanafanyika kwa sababu ya tabia yetu mbaya ya kuiga mila za watu wengine. Wanawake wetu hujirembesha, huvaa nguo fupi na kufanya mambo mengine ambayo huwafanya wanaume wapoteze akili. Hii ndio sababu Kalasinga mmoja alisema: \"Kama kitu inasimama akili potea\". Kwa hivyo, ni lazima wanawake wakome kuwashawishi wanaume. Siku hizi sisi hukaa na wanawake bega kwa bega katika magari ya abiria. Katika hali kama hiyo ni rahisi sana kwa mtu kumsukuma mwanamke au kuyagusa matako yake kidogo, jambo ambalo Mswada huu unasema litakuwa kosa la kimapenzi. Ni lazima tuambiane ukweli. Wanaume wana marafiki wanawake, na wanawake pia wana wanaume marafiki. Kwa kawaida kama una bibi na umemweka mwanamke mwingine, huyu wa pili anaweza kukuhadaa kama hufanyi kama anavyotaka. Anaweza kusema umemlazimisha kufanya mapenzi, na kulingana na Mswada huu hilo litakuwa kosa la kimapenzi. Ni lazima tufikirie kuhusu mambo kama hayo. Ni lazima tufanye mambo ambayo yanahitajika kufanywa. Ni lazima tujihadhari na mambo ambayo yanaweza kuleta ubaya katika nchi hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni kinyume cha mila zetu za Kiafrika na maadili ya dini hasa Islamu kusema kuwa ni lazima msichana afikishe miaka 18 ili aolewe. Msichana anapobalehe, tunaamini kuwa yeye ni mwanamke na kwa hivyo anaweza kuolewa. Katika sehemu ambazo wasichana hawajasoma, wakiwekwa hadi miaka 18, wanaweza kujiingiza katika usherati na UKIMWI utaongezeka. Ikiwa wanaweza kuolewa mapema, ni sawa. Kulikuwa na mwanaume mmoja aliyeowa msichana mdogo. Alikuwa amebalehe lakini mwanaume alimwona kuwa ni mdogo. Alipomwoa, alikuwa akilala kitandani mwake na yule mwanamke lakini hamgusi. Mama yake yule msichana alimwuliza kama walikuwa wamefanya mapenzi na mume wake. Yule msichana alimwambia mama yake kuwa hawakuwa wamefanya mapenzi na mume wake. Mama yake alimwuliza walilokuwa wakifanya naye akamwabia kuwa walikuwa wakilala tu. Mama yake alimwambia achukue mavi kidogo amwekee mumewe kwa mto halafu mumewe atamwuliza ni nini alichomwekea kinachonuka. Alimwambia amweleze mumewe kuwa ni mavi kidogo. Ikiwa mumewe angalimwuliza kama kuna mavi kidogo, angalimwuliza ikiwa kuna mwanamke mdogo. Kwa hivyo, yule msichana akamwekea mumewe yale mavi. Alipokuwa akilala akapatwa na harufu mbaya. Alimwuliza msichana yule ni kitu gani kilichonuka kwenye mto. Yule msichana alimwambia kuwa ni mavi kidogo. Mwanaume yule alimwuliza ikiwa kuna mavi kidogo kwa kuwa makubwa au madogo yote yananuka! Naye msichana alimwambia kuwa hata kwa mwanamke, hamna mdogo kwani anaweza kazi zote. Kwa hivyo kusema kuwa ni 836 PARLIAMENTARY DEBATES May 2, 2006 lazima wanawake wangojee hadi wafike miaka 18 si haki. Nimepinga jambo hilo lakini ninakubaliana na yale mambo mengine yote."
}