GET /api/v0.1/hansard/entries/251538/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 251538,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/251538/?format=api",
"text_counter": 86,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, ni ajabu kuwa Waziri Msaidizi alijua kuwa katika mwaka wa 2004 kungekuwa na upepo mkali ambao ungebomoa madarasa matatu katika shule hiyo. Hata hivyo, hawakutenga pesa za kutosha kuyajenga upya madarasa hayo. Madarasa matatu yalibomolewa lakini wao walitenga Kshs18,000. Nimemuuliza kama pesa hizo zitatosha, lakini hakunijibu. Ingawa kuna pesa za dharura katika kitita cha CDF, tulitumia pesa hizo kuwapelekea maji watu wetu wakati wa kiangazi. Wizara ina sera gani maalum ya kutekeleza dharura kama hii hapa nchini? Waziri Msaidizi amesema kuwa wananchi waliyajenga upya madarasa hayo. Ukweli ni kwamba madarasa hayo hayajajengwa mpaka leo. Kwa nini analipotosha Bunge hili?"
}