HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 251650,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/251650/?format=api",
"text_counter": 198,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 253,
"legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
"slug": "mwandawiro-mghanga"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza nataka kumpongeza Bw. Kimeto kwa kuwasilisha Hoja hii muhimu sana. Hoja hii ina lengo la kutafuta sera halisi za kukabiliana na swala la kutatua usafiri katika nchi hii. Sera ni mipango halisi. Katika karne hii ya 21, ni muhimu kuwa na sera halisi ambazo zinaonekana wazi kitaifa na kimataifa. Inafaa ijulikane kwa kila Mkenya kuwa Serikali hii inalenga kufanya nini kutatua swala la usafiri katika nchi hii. Tukiangalia matatizo ambayo tuko nayo ya usafiri, ni wazi kabisa kuna umuhimu wa sera. Ukiangalia msongamano wa magari katika miji, hasa Mji wa Nairobi, inakuonyesha wazi kabisa kwamba kuna haja ya kuwa na sera ya kukabiliana na shida hii. Bw. Naibu Spika, ni aibu kuona bado tunapoteza wakati mwingi katika usafiri. Katika hii karne hatuwezi kufikia kiwango cha maendelea tunachotaka. Ukiangalia huduma za usafiri kutoka Mombasa hadi Voi utaona kuna msongamano wa magari ufikapo Mariakani. Malori yanayoenda sehemu nyingine za bara la Afrika kama Uganda, Rwanda, Burundi, Congo Demorcratic Republic na Sudan husabibisha msongamano mkubwa wa magari. Katika hali kama hiyo madereva na wafanya biashara huumia. Pia uchumi utaangamia kwa sababu ya kutokuwa na sera halisi ya usafiri. Utaona kwamba barabara ya Voi-Taveta inayotuunganisha na nchi za Tanzania na Afrika Kusini imekaa kwa miaka mingi bila kukarabatiwa. Hii ni kuonyesha kwamba hatuna sera ya kutengeneza barabara zetu zinazotuunganisha na majarani zetu. Ukifika upande wa Tanzania utaona aibu kubwa, kwa sababu Watanzania wamejenga barabara zao mpaka sehemu ya Taveta, iliyo mpakani. Lakini ukiingia sehemu zetu utaona hakuna barabara. Ukichunguza haya yote utaona kuwa ajali za barabarani zinatokea kwa sababu hatuna Sera maalum ya usafiri. Juzi tulipoteza ndugu zetu Wabunge kwa sababu ya kutokuwa na sera halisi za usafiri. Inasemekana kuwa rubani wa ndege hiyo na ndege yenyewe hawakuwa katika hali sawa. Watu wengi walikufa katika ajali hiyo. Tulipata hasara kubwa kwa sababu ya kutokuwa na sera za usafiri wa hewani. Hata katika maziwa yetu kuna shida nyingi. Ukiangalia usafiri katika Ziwa Victoria utaona watu wengi wanaangamia. Kuna ajali nyingi katika Ziwa Victoria. Pia katika Ziwa Turkana tunasikia kuna ajali nyingi. Katika Bahari Hindi ajali vile vile zipo kila siku. Hiyo inatuonyesha kuna haja kubwa sana ya kuwa na sera za usafiri. Nimesisitiza kwamba katika hii karne ya 21, ikiwa tunataka maendeleo, ni lazima tuwe na sera za usafiri na kuzitekeleza. Ni lazima tuhakikishe kuwa tuna njia bora zaidi za usafiri na mawasiliano katika nchi hii ili tukabiliane na matatizo ya karne hii. Upande wa barabara, ni muhimu tutekeleza sera za usafiri kwa makini na kwa mpango halisi. Hata wakati tunapojadili Bajeti ni lazima tuangalie sera za usafiri. Ukitoka Nairobi hadi Mombasa utaona karibu masaa matatu yanaisha kabla hujatoka mjini kwa sababu ya msongamano wa magari. Kama tungejenga barabara pana kutoka Nairobi hadi Machakos hiyo ingepunguza msongamano wa magari. Pia hii ingechangia uchumi kuimarika. Masaa mengi hutumiwa na wasafiri kutoka mjini Mombasa hadi Mariakani kwa sababu ya msongamano wa magari, na hali sehemu hiyo ina barabara ya kimataifa. Bandari ya Kilindini ni msingi wa uchumi wa nchi za Afrika Mashariki. Kama kungekuwa na sera nzuri, barabara kama hizo zingepanuliwa maradufu. Kuhusu usafiri wa reli, tukisema tuzibinafsishe huduma za reli utaona hatuendelezi hiyo sekta. Katika hii karne maendeleo yanaweza kuimarika tu ikiwa kuna usafiri sawa wa reli. Ikiwa kuna usafiri sawa wa reli mizigo mizito, ambayo huharibu barabara zetu, itasafirishwa kwa kutumia reli. April 26, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 683 Vile vile, kuna haja ya kubuni sera za usafiri wa hewani. Ni muhimu kuendeleza viwanja vyote vya ndege humu nchini. Tukivikarabati viwanja vyote vya ndege hata vile vidogo vidogo, ajali za dharura zikitokea ndege zitaweza kutua na kusafirisha wagonjwa hadi miji mikubwa yenye huduma za matibabu. Kwa hivyo, sera za usafiri wa hewani ni muhimu katika kuunganisha miji yetu na sehemu za mashambani. Ningependa kusema kuwa tukiwa na sera madhubuti za usafiri, basi wakati tunapojadili Bajeti tutajua pesa zitakazohitajika kwa utekelezaji wa miradi. Tunaweza kusema, kwa mfano, mwaka huu tunatenga zaidi ya asilimia 80 ya pesa zetu kutengeneza barabara za Nairobi peke yake, halafu sehemu nyingine zingojee mpaka wakati mwingine. Kama tungekuwa na sera za namna hiyo tungeweza kujenga barabara zetu. Lakini utaona kuwa sera za usafiri ni holela holela na tunagawa pesa kidogo kidogo kutumika kote nchini, na hivyo hatufanyi chochote cha maana. Kuna haja ya kuwa na sera za kutengeneza barabara za sehemu fulani au wilaya fulani, na zile za Sehemu nyingine zingojee mpaka pesa zake zitakapopatikana. Ni muhimu kufikiria hali halisi, na kufanya mipango madhubuti ya kuleta maendeleo kwa kutumia njia bora za kisayansi. Tukitazama nchi yetu, tunaweza kuona ni sehemu gani tunakoweza kuanzia. Tukiendelea na sera za kiholela holela, ambapo tunaigawia kila sehemu pesa kidogo, hatutaweza kupata maendeleo. Tukiendelea hivyo, tutangojea miaka mingi kabla ya kupata maendeleo. Vile vile, tukiwa na sera halisi za usafiri jeshi letu litaweza kutusaidia katika ujenzi wa barabara. Bwa. Naibu Spika, sera za usafiri ni muhimu zihusishe Wizara za Uchukuzi, Barabara na ya Mipango. Ni Wizara ya Mipango inayofaa kuingilia sana mambo ya sera. Ni lazima ituonyeshe iwapo tuna mipango halisi, ni barabara zipi tunaweza kuzitengeneza. Hili Bunge lina Wabunge ambao wamesoma. Ni lazima elimu yetu ifanye kazi. Hatuwezi kufanya mambo vile yalivyofanywa zamani na watu ambao hawakusoma. Sisi tumesoma na haifai tutekeleze miradi ya maendeleo kiholela holela. Mhe. Kimeto aliileta Hoja hii hapa akijua kuna Wabunge ambao wamesoma, na wanatarajiwa na Wakenya kubuni sera ambazo zitaleta maendeleo katika nchi yetu. Si lazima tuvutane katika mambo ya maendeleo, tukisema ni lazima tufanye maendeleo Wundanyi au Mugirango Kusini. Ni lazima tufikirie taifa kwa jumla. Ni lazima pia tuzihusishe serikali za mitaa katika ujenzi wa miji. Mji wa Nairobi una msongamano mbaya wa magari kwa sababu mpango wa barabara zake ni mbaya."
}