GET /api/v0.1/hansard/entries/252987/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 252987,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/252987/?format=api",
"text_counter": 223,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamunyinyi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 291,
"legal_name": "Athanas Misiko Wafula Wamunyinyi",
"slug": "athanas-wamunyinyi"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa hii nafasi ili niweze kuchangia Hoja hii. Kwanza ningependa kuchukua dakika mbili kumuuliza Waziri wakati anapojibu atueleze kinaganaga kilichozuia ujenzi wa kiwanda cha sukari cha Busia. Pia ningependa atueleze kilichotendeka kuhusiana na upanuzi wa kiwanda cha sukari cha Nzoia. Kuna vifaa vinavyohitajika kufanya upanuzi huko Nzoia katika kiwango cha asilimia 30. Miaka mitano imepita na upanuzi huu haujafanywa. Ikiwa Serikali haina haja na wakulima wa miwa upande wa Busia, Bungoma na Mkoa wa Magharibi kwa jumla, anafaa atueleze leo. Tunataka Waziri atueleze mipango madhubuti Wizara yake iliyonayo kuhusiana na secta ya ukuzaji wa miwa katika nchi yote. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninazungumza hivi kwa sababu eneo ninalowakilisha liko Nzoia. Mimi ni mkulima na ninawakilisha wakulima. Wakulima wameumia. Waziri anafaa atueleze mambo haya leo. Tunataka tuambiwe kama kiwanda cha Busia hakitajengwa ili tusahau jambo hilo. Kila wakati tunaambiwa kwamba kiwanda cha Busia kitajengwa na kile cha Nzoia kitapanuliwa, lakini mambo haya hayajafanywa ingawa wakulima wanatozwa ushuru. Nikiyafikiria haya mambo ninaweza kukasirika, ingawaje sipendi kukasirika. Kwa hivyo, nataka Waziri azungumzie juu ya mambo haya. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}