GET /api/v0.1/hansard/entries/253285/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 253285,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/253285/?format=api",
"text_counter": 265,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 253,
"legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
"slug": "mwandawiro-mghanga"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili nichangie huu mjadala nyeti kuhusu usalama. Huu ni mjadala nyeti sana kwa sababu tumewapoteza ndugu zetu tuliokaa nao hapa. Nataka kupendekeza kwamba watu ambao wako upande huo, hasa Mawaziri ambao wanaandika Bajeti na kuleta hapa, wana jukumu kubwa zaidi la kuangalia hayo maneno. Hatuwezi kuwa tunalalamika kila wakati katika Bunge hili. Wengine lazima waonyeshe njia kwa sababu wamepewa mamlaka ya kuwa huko. Tunajua kwamba vyombo vya usalama ni lazima vifanye kazi kwa umoja. Vinapaswa kuzingatia nidhamu zote zinazohusika. Hivi ninavyozungumza, katika Kikosi cha Polisi, inajulikana kwamba Kamishina wa Polisi na Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi hawazungumzi! Hawafanyi kazi pamoja. kuna chuki nyingi kati yao. Tunataka Bw. Waziri atueleze Serikali inafanya nini ili kusuluhisha mzozo huo. Hatuwezi kuongozwa na siasa hasa katika vyombo nyeti kama hivyo vya usalama wa kitaifa. Bw. Naibu Spika wa Muda, nakubaliana na yote yaliosemwa na wenzangu kwamba, wakati wa Bajeti, tuangalie hali halisi ya nchi yetu. Hatuwezi kugawanya kila kitu kwa usawa na kupata maendeleo. Ni lazima tuangalie sehemu zingine ambazo ni muhimu sana katika kuharakisha maendeleo. Hiyo ni miundo-misingi ya kitaifa. Vile vile, ni lazima tuangalie sehemu ambazo zimewachwa pembeni kwa muda mrefu. Wakati tunapofanya Bajeti, kwa mfano ya maji, lazima tuseme: \"Mwaka huu kwa Bajeti ya maji, tunaenda sehemu fulani!\" Nakubali tuanze na zile sehemu kame kama Mkoa wa Kasikazini Mashariki ambao una mahitaji mengi. Hata wakati tunaangalia Bajeti ya barabara, hatuwezi kujenga barabara kila mahali. Lazima tuseme kwamba tutaanza na Nairobi na tuitengeneze yote. Wengine tunaweza kungoja. Sehemu kama Mkoa wa Kasikazini Mashariki na sehemu zote ambazo zimewachwa pembeni, ni lazima tuwe na sera makusudi za kuhakikisha kwamba kila wakati, tunatenga pesa za kutumiwa katika sehemu hizo. Bw. Naibu Spika wa Muda, kama vile wengine wamesema, ningependa kuona kuwepo kwa wanajeshi zaidi katika Mkoa wa Kaskazini Mashariki. Maafisa wa polisi, Jeshi la Nchi Kavu na Jeshi la Hewani wanapaswa kupelekwa kwa wingi katika mkoa huo. Tunasikitika kwamba swala la usalama linazidi kuzorota kila wakati. Kuwepo kwao huko kusiwe ni kuchukua silaha tu na kulinda wananchi. Wajiunge na wananchi kujenga mabwawa, kupanda misitu na shughuli zote za kimaendeleo katika sehemu hiyo. Hilo ni jambo ambalo linaweza kufanywa makusudi. Tusingojee hadi mwaka ujao. Hata maswala mengine kama ya kutokujua kusoma na kuandika yanaweza suluhishwa kimapinduzi. Tunaweza kupeleka watu ambao wamesoma katika Mkoa wa Kasikazini Mashariki. Katika muda wa miezi sita, watakuwa wamejua kusoma na kuandika. Nchi zingine zimefanya hivyo badala ya kulimatia na kungojea tu. Nakubali kwamba Bajeti ikija, tuiangalie makusudi kabisa na tutenge pesa za kutumiwa katika sehemu hiyo. Tusijaribu kung'ang'ania pesa hizo ili zipelekwe kwa kila mtu. Ni lazima tuangalie mahali ambapo kuna mahitaji zaidi kama vile barabara, ili tufanye maendeleo. Kwa hayo machache, nashukuru!"
}