GET /api/v0.1/hansard/entries/253298/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 253298,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/253298/?format=api",
"text_counter": 278,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Machage",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Health",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ni yule anayeathirika na hali ya kutokuwa na usalama ambaye anafahamu uchungu. Sio Mkoa wa Magharibi au Kaskasini Mashariki tu ambapo watu wameathirika na hali ya kutokuwa na usalama. Hivi majuzi, tumeona gharama ya kutokuwa na usalama. Kenya imelipa gharama kubwa. Wazalendo walipokuwa wakienda huko, walipoteza maisha yao. Lakini ni lazima viongozi wakae na kufikiria habari walizonazo. Ni kwa nini kuna vita vya kikabila katika sehemu fulani? Katika sehemu yangu, Wakuria na Wamaasai wameishi pamoja kwa miaka mingi. Hata watu wa Mkoa wa Kaskazini Mashariki wameishi pamoja kwa miaka mingi. Lakini kila wakati, vita hutokea. Viongozi humu Bungeni hukaa, huongea na kuafikiana. Wanakubalina juu ya mambo yatakayotekelezwa na Serikali. Siku moja, mimi nikiwa ndani ya Serikali, nilitoa wosia wangu kwa Serikali kwamba kuna ukosefu wa usalama katika eneo langu la Bunge. Niliuliza Serikali itekeleze mambo fulani. Lakini haya mambo huangukia masikio yaliofunikwa. Kuna sababu gani kwa sehemu fulani nchini kuwa na wakuu wa wilaya ambao wamefanya kazi kwa miaka zaidi ya minne katika sehemu yenye vita? Kuna sababu gani wakati kuna ukosefu wa usalama, maafisa wanaopelekwa huko wanatoka kwa makabila hayo hayo? Tunawaambia kwamba wakati unapopendekeza njia za kuleta usalama, lazima wanaohusika waondolewe katika sehemu hizo, ikiwa wao ndio wanaangalia usalama. Naomba kwamba wanaohusika katika sehemu yangu na TransMara waondolewe, hata kama ni askari Wakuria au Wamaasai, walete maafisa kutoka sehemu zingine ili kudumisha usalama. Bw. Naibu Spika wa Muda, wakuu wa wilaya ambao wamekaa hapo kwa siku ambazo zimepita waondolewe. Hata kama amekaa miezi mitatu lakini kuja kwake ndio ikawa chanzo cha mapigano ya wananchi, hafai. Inafaa aondolewe kwa sababu labda yeye ndiye anasababisha 592 PARLIAMENTARY DEBATES April 19, 2006 mapigano haya. Wanapopigana hao watu hupewa mali. Ng'ombe wanavyoibiwa, kuna ng'ombe mmoja amewekewa. Wakati mwingine lazima historia pia iangaliwe; yaani juu ya mambo ya shamba na ardhi. Watu wanalalamika kwamba hii ni sehemu yao tangu siku za awali, na tafadhali waachwe wafuge mifugo wao na sio kufunika masikio na kuangalia kando wakati watu wanalalamika. Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo. Usipowasikiliza hawa kama wameshalima chakula chao halafu wengine wanakuja kulisha mifugo yao kwa hiki chakula na wakati wa kuvuna hawana chakula, wanaanza kukodolea Serikali macho kuwapa chakula cha ziada; basi mtu kama huyo ana uchungu wa kutoka na kwenda kupigana kwa sababu lazima alishe watoto wake. Mambo kama haya lazima yaangaliwe kwa undani. Ni kwa nini watu wanapigana? Bw. Naibu Spika wa Muda, inafaa Tume ya Ndung'u iangalie mambo ya mashamba kwa sababu kuna wengine wamenyanyaswa na kunyang'anywa mashamba. Watapeleka mifugo wapi? Lazima wachunge mifugo yao. Ni kweli gharama tunayotumia kwa askari wa ulinzi wa nchi hii ni kubwa sana na isiyostahili. Hao watu wapewe kazi ya kufanya. Kama hakuna vita, basi wajiunge na wengine wenzao waangalie na kulinda usalama wa nchi. Kama kuna jambo la vita basi wapelekwe huko kwa wingi na watunze walioathirika kusudi usalama urudi. Tukifanya hivi, basi tutapiga hatua mstari wa mbele. Maendeleo ni lazima yatekelezwe kila mahali nchini kwa sababu ukimnyang'anya mtoto kisu lazima umpe kijiti cha kuchezea. Kama hutaki afanye kazi ya ukulima wa ng'ombe ama kukimbiza ng'ombe kama yeye ni mwizi wa ng'ombe, basi mpe kilimo. Sehemu hizi zinatosha na zinafaa kwa kilimo fulani fulani, hata hizi sehemu za mipakani kama huko kwetu. Peleka kilimo huko kama mazao ya majani chai, weka viwanda, peleka umeme, lima barabara. Kukiwa na vita, Serikali itakimbia na kufika huko kwa muda mfupi. Peleka simu na mawasiliano yao yatakuwa sawa na ya karibu. Peleka simu za mkono kusudi kama mtu ana shida anaweza kupiga simu na kwa muda mfupi Serikali imefika huko. Magari ambayo yanapelekwa huko yawe mazuri na sio magari yanayochechemea kila wakati. Bw. Naibu Spika wa Muda, naunga Hoja hii."
}