GET /api/v0.1/hansard/entries/254157/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 254157,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/254157/?format=api",
"text_counter": 174,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. A.C. Mohamed",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Livestock and Fisheries Development",
"speaker": {
"id": 3,
"legal_name": "Abu Mohamed Chiaba",
"slug": "abu-chiaba"
},
"content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa dakika mbili. Nataka kumpongeza Rais kwa Hotuba aliyoisoma hapa. Imejaa mambo ya busara. Alisema viongozi wote waungane pamoja, ili kuleta maendeleo makubwa katika nchi hii. Mwaka uliopita, tulizungumza mambo ya siasa tupu, ilhali wajibu wetu ulikuwa kupitisha sheria zinazoletwa Bungeni. Badala ya kupitisha Miswada 27, tulipitisha saba peke yake. Kiuchumi, Serikali imefanya vizuri. Serikali imeboresha hali ya uchumi wa taifa hili. Uchumi unaendelea kuimarika kutoka sufuri hadi asilimia 5. Ningependa kueleza shida ya maji katika eneo langu la Bunge. Tuna shida sana. Tunaomba Wizara inayohusika kuchukua hatua kurekebesha hali hiyo. Jambo lingine linahusu utafiti wa mafuta katika sehemu ya Lamu. Wakati sasa umefika kwa Serikali kuwajulisha Wakenya wote na watu wa Lamu kinachofanyika huko, ili wasiwachwe nyuma katika uvumbuzi huo. Kwa hayo machache, naunga mkono Hotuba ya Rais."
}