GET /api/v0.1/hansard/entries/254998/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 254998,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/254998/?format=api",
    "text_counter": 149,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "[The Assistant Minister for Information and Communications]",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ahsante sana kwa kunipa fursa hii kusema machache kuhusu Hotuba ya Rais. Ningetaka kuanza na swala la mazungumzo. Hakuna mtu ambaye anaweza kupinga mazungumzo baina ya Serikali na Upinzani. Lakini, ni muhimu kuelewa kwamba mazungumzo yanayosemwa siyo mazungumzo. Naamini ya kwamba wanapodai mazungumzo, wanachotaka wapinzani ni utawala na mamlaka. Hali hiyo haifai kwa sababu tulifanya uchaguzi na wapinzani wakapewa kazi ya kupinga. Waliochaguliwa kuunda Serikali walipewa kazi ya kutawala. Sasa Upinzani hauwezi kudai kutawala. Ni lazima waendelee na kazi yao ya kupinga na sisi tuendelee na kazi yetu ya kutawala. Ni muhimu sana wapinzani waelewe maana ya Upinzani, ili waweze kuboresha maisha ya wananchi. Sio kubomoa Serikali, nchi na maendeleo. Upinzani hauna idhini ya wananchi ya kutawala. Wasiseme: \"Kama hatutawali, hakuna atakayetawala!\" Hata Kiongozi wa Upinzani aliposema kwamba Serikali ya umoja wa taifa haina uhalali wa Kikatiba, hakumaanisha hivyo. Kama angemaanisha hivyo, angeenda kortini kushtaki uhalali wa Serikali hii ya umoja wa taifa. Lakini hawajafanya hivyo! Hiyo inaonyesha hawaamini madai wanayoyasema hapa. Bw. Naibu Spika wa Muda, isitoshe, Serikali hii imekuwa---"
}