GET /api/v0.1/hansard/entries/255004/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 255004,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/255004/?format=api",
"text_counter": 155,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba niongezewe dakika mbili ambazo zimepotea. Serikali hii imeufanyia Upinzani ufadhili wa hali ya juu kwa sababu imewaleta Serikalini hata kama hawana idhini ya kuwemo Serikalini. Shida iliyoko ni kwamba ukiwapa wapinzani shubiri, wanataka pima! Ukiwapa tabasamu, wanataka busu. Wanataka yote kwa pupa! Ndiyo sababu ni rahisi sana watakosa yote. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kuzungumzia suala la ukabila. Rais angeongea zaidi kuhusu swala hilo. Ukabila ni adui mkubwa sana kwa nchi hii. Kama ningekuwa na uwezo, ningependa Wabunge waitazame filamu iitwayo \"Hotel Rwanda.\" Hiyo filamu inaonyesha hasara ambayo inaweza kupatikana katika nchi kutokana na itikadi za ukabila. Wengine wanachochea ukabila kana kwamba hawaelewi hasara zake. Wengi hapa wameisifu serikali ya Tanzania kwa kusimamisha ukabila. Lakini tumesahau kwamba wamefanya hivyo kwa sababu wamegombeza siasa za ukabila na uundaji wa vyama vya kikabila. Tunastahili kuiga mfano huo. Bw. Naibu Spika wa Muda, nchi hii ingeunda sheria ya kugombeza matamshi na siasa za kikabila! Mtu akipatikana akitoa matamshi ya kuchochea ukabila, anashtakiwa na jinai ya kueneza itikadi mbovu. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuhusu ufisaidi, tunashukuru kwamba watu 150 wamefikishwa mahakamani kwa makosa hayo. Lakini wananchi wanataka \"damu\" zaidi. Wangetaka kuona watu wengi wakifikishwa mahakamani kwa kosa hilo. Ufisadi haumo mijini peke yake. Ukienda mashambani, visa vya ufisadi ni vingi! Lazima ufisadi huo upigwe vita pia. Ningependa kuomba Utawala wa Mikoa uwache kuunga mkono ufisadi huko mashambani. Katika eneo langu la uwakilishi Bungeni, maafisa wa Utawala wa Mikoa wanaunga mkono ufisadi. Wale wanaopiga filimbi kuhusu ufisadi wasiwe wanafutwa kazi. Wale waliopoteza kazi zao wanastahili kurudishiwa kazi hizo. Kuna wale walipoteza kazi zao wakati walifichua sakata ya Goldenberg. Kuna wafanyakazi walipoteza kazi zao huko Grand Regency kwa sababu walifichua ufisadi. Hakuna haja kungoja sheria iwepo, ili warudishwe kazini. Bw. Naibu Spika wa Muda, lazima tuwe na vigezo sawa vya kuwahukumu wafisadi. Hatuwezi kila wakati kuuliza anayehusika na ufisadi awache kazi. Lakini watu wengine, hata wakifunguliwa mashtaka, tunang'ang'ania waendelee kuwepo kazini. Ikiwa tunasema Mawaziri waache kazi, hatuwezi kusimama hapa na kusema Gavana wa Benki Kuu ya Kenya aendelee kuwa ofisini, ingawa amefunguliwa mashtaka ya ufisadi. Bw. Naibu Spika wa Muda, tuliambiwa ya kwamba wahusika katika sakata ya Anglo Leasing, ingawa walirudisha pesa, ni lazima wafunguliwe mashtaka ya kushiriki katika ufisadi. Kabla ya Anglo Leasing kujulikana, kulikuweko na Waziri aliyekuwa wa barabara na ujenzi ambaye alilipiwa safari na kampuni ambayo Wizara yake ilikuwa imeipatia kandarasi ya kutengeneza barabara ya kwenda Mombasa. Waziri huyo pamoja na maafisa wake na bibi yake walilipiwa safari ya kwenda ulaya. Huyo Waziri alisimama hapa baadaye na akakiri---"
}