GET /api/v0.1/hansard/entries/255013/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 255013,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/255013/?format=api",
"text_counter": 164,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. H. M. Mohammed",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 394,
"legal_name": "Hussein Maalim Mohamed",
"slug": "hussein-mohamed"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninafurahi kwamba tumerudi kwa Bunge. Mwaka uliopita ulikuwa mgumu sana kwa sababu kulikuwa na mambo ambayo si ya kawaida. Tulikuwa tukishindania matunda mawili; chungwa na ndizi. Hiyo vita ilikuwa ngumu sana. Sijaona vita mbaya kama hiyo maishani mwangu, tangu nilipokuwa kwa siasa. Bw. Naibu Spika wa Muda, watu wakishindana, mmoja hushindwa na mwingine anashinda. Na yule anashindwa anapanguza vumbi na kuendelea na kazi. Lakini jambo ambalo linanishangaza ni kwamba wale wameshinda ndio wako na hasira. Badala ya kufurahi, wako na hasira nyingi sana. Labda ni kwa sababu watu wengine wamekosa kuwa mawaziri. Nataka kuwaambia hawa kwamba kukosa kuwa Waziri si hoja. Mimi nilikuwa Waziri miaka mingi sana na wakati huu nimekosa hiyo nafasi. Lakini ninakaa hapa bila hasira. Ningependa kuwaambia wenzangu ambao wamekosa kazi ya Uwaziri wawache hasira na waendeshe kazi zao pole pole. Bw. Naibu Spika wa Muda, ufisadi ni kitu kibaya sana kwa nchi. Umeangusha mataifa mengi katika dunia na hasa katika bara la Afrika. Miaka kumi na tano iliyopita, nilikuwa hapa nikichangia Hoja kama hii ya Hotuba ya Rais na wakati huo nilikuwa Waziri katika Afisi ya Rais. Nilisema ufisadi umezidi katika nchi hii. Nilisema kuwa watu wamekuwa maskini, wameshindwa kulipa karo, wameshindwa kununua vyakula na nguo kwa sababu ya ufisadi. Niliongeza kusema kwamba ufisadi umefika asilimia 45 katika nchi yetu. Nilipomaliza kuzungumza nilienda kula chakula cha mchana. Kurudi ofisini, nilipata barua ya uhamisho kutoka Afisi ya Rais hadi orofa ya tatu ya Reinsurance Plaza. Wakati Serikali hii mpya ilipochukuwa mamlaka, nilifikiria ufisadi utasimama. Serikali hii imechaguliwa kwa sababu ilitoa ahadi kwamba itamaliza ufisadi. Lakini inaonekana ufisadi katika nchi hii bado unanawiri na unaendelea. Wananchi wa Kenya wanataka ufisadi ukomeshwe. Wananchi hawana haja sana kurudi kwa mambo yaliyofanyika hapo nyuma. Kurudi nyuma sana, kutaleta balaa. Ninafuraha Waziri wa Haki na Mambo ya Katiba yuko hapa. Ningependa kumueleza akomeshe ufisadi. Afunge brake na wale watu ambao wako katika hili gari la ufisadi wateremke na gari liende bila hao watu. Ningependa kuzungumza juu ya ardhi. Nafikiri nimeona Serikali nne tangu nikiwa mchanga. Tumewahi kuwa na serikali ya mkoloni, ya Hayati Mzee Jomo Kenyatta, ya Rais Mstaafu Bw. Moi na hii ya sasa inayoongozwa na Rais Kibaki. Serikali ya mkoloni iliwapa watu mashamba makubwa na mpaka sasa hati za mashamba hayo zinatambuliwa kisheria. Hayati Mzee Kenyatta, kwa mfano, aliwapa watu wake mashamba makubwa. Hati hizo zinatambuliwa hadi sasa chini ya sheria zetu. Rais Mstaafu, Bw. Moi, alifanya vivyo hivyo. Hata mimi nilipata sehemu ndogo ya ardhi. Inajulikana wazi kwamba mimi sina shamba kubwa. Hata kama ningepewa shamba kubwa singalikubali kwa sababu sijui kulima. Nafikiri Serikali ya Rais Kibaki haijawapa watu mashamba yoyote hapa nchini. Naipongeza Serikali hii kwa sababu haijahusika katika ufisadi wa mashamba. Lengo langu la kurejelea historia hiyo ni kuhimiza Serikali hii isifuatilie mambo yaliotendeka miaka ya zamani. Tuendelee kwa utaratibu. March 29, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 155 Waziri wa Haki na Mambo ya Katiba anafanya kazi nzuri. Wakati alipokuwa katika Wizara ya Maji alifanya kazi nzuri. Ningemuhimiza aendelee vivyo hivyo na asifanye mambo kwa hasira. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kuzungumza juu ya idara ya polisi. Polisi wanawasumbua watu wangu. Kutoka Liboi hadi Nairobi kuna zaidi ya vizuizi 100 vya polisi barabarani. Polisi hawa wanasimamisha magari na kuwashukisha watu. Kisha wanawapokonya wasafiri kila kitu. Nasikia kwamba hata wanaingiza mikono yao ndani ya nguo za akina mama. Sielewi kile wanachokitafuta. Kuna kizuizi kimoja katika daraja la Garissa. Vizuizi vingine viko Madogo, Bangali na Ukase. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, ningewasihi polisi wawache kuwasumbua wananchi."
}