GET /api/v0.1/hansard/entries/255061/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 255061,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/255061/?format=api",
    "text_counter": 212,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Twaha",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 145,
        "legal_name": "Yasin Fahim Twaha",
        "slug": "yasin-twaha"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili nichangie Hoja iliyo mbele yetu, ambayo yahusu usajili wa shukrani za Nyumba hii kwa Hotuba ya Rais. Hotuba ya Rais ilikuwa nzuri. Iligusia mambo mengi kuhusu sekta nyingi za maendeleo, ambazo zaweza kubandilisha maisha ya Wanakenya. Alipokuwa akiisoma Hotuba yake, waandishi wa habari waliwapiga Wabunge picha wakiwa wamelala. Katika Bunge la Tanzania, jambo hilo limechunguzwa na kujulikana kwamba Wabunge hawalali katika Chumba. Wanachofanya ni kutafakari Hoja. Kwa hivyo, ningependa kuwaambia Wabunge wenzangu, na Wakenya kwa jumla, kwamba Wabunge huwa wakitafakari Hoja wanapofunga macho wakiwa katika Chumba. Rais alizumgumzia mambo mengi, lakini la muhimu lilikuwa swala la ukame ambao umetukabili na ukosefu wa chakula katika sehemu fulani za nchi yetu. Katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni huko Lamu, kulikuwa na mkutano kuhusu malisho ambao ulihusisha watu wa Lamu na Ijara. Huko kuna ukame mwingi na baadhi ya wakulima wa Ijara wamehamisha mifugo yao na kuipeleka huko Lamu. Kwa hivyo, kulikuwa na mvurutano kati ya watu wa Ijara na wale wa lamu kuhusu malipo. Ningependa kushukuru Serikali, hasa Wakuu wa Wilaya na Tarafa ya Lamu, kwa kuingilia jambo hilo na kulisuluhisha, kwa sababu lingeleta ugomvi. Ningependa kuwaomba wenzangu katika wakati huu mgumu, kustahimiliana na kukaribishana. Mfugaji akija kwako kuomba nyasi kidogo ili awalishe mifugo wake, mkaribishe kwa sababu si kupenda kwake kwamba ukame umeikumba sehemu yake. Siku nyingine, ukame waweza kuwa pande yako na wewe pia utake kusaidiwa. Wakenya wote ni ndugu na ni lazima tuishi pamoja na tusaidiane katika maendeleo. Jambo lingine mhe. Rais aligusia kuhusu watu wa Lamu ni Mswada kuhusu ukuzaji wa pamba, ambao utaletwa Bungeni. Sitaki kuongea juu ya Mswada huo, lakini kama watu wa Lamu kile tunachotaka zaidi ni pesa. Kubadilisha jina la bodi na kuwa halmashauri hakutawasaidia wakulima. Juzi tulisikia kuwa Kshs250 milioni zilitolewa ili kufufua sekta ya pamba katika Mkoa wa Nyanza. Sijasikia kama sekta ya pamba katika Mkoa wa Pwani imepata pesa zozote. Wilaya ya Lamu inazalisha kilogramu milioni 10 za pamba kila mwaka, na tunastahili kusaidiwa vile March 29, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 169 wakulima wa Nyanza walisaidiwa. Mhe. Rais pia aligusia katika Hotuba yake mpango wa kupunguza umaskini. Katika Wilaya wa Lamu tunataka kumaliza umaskini. Kuna mradi wa makao, lakini wakulima wameshindwa kulipa ada za mashamba yao. Mpaka leo, wana madeni. Tumependekeza kwa Serikali kutumia pesa zetu za CDF kuwalipia hawa wakulima ada za mashamba yao ili wapate hati ya umilikaji ardhi, na waweze kumiliki mashamba yao. Hiyo itawawezesha kuwa na msingi wa maendeleo. Inasikitisha kwamba Serikali haijatujibu kufuatia ombi letu hilo. Ningependa Serikali itilie maanani jambo hilo ili kumaliza umaskini. Deni tunalodaiwa ni Kshs24 milioni na tuna pesa za kulipia, lakini Serikali inatuchelewesha. Tunaomba tukubaliwe tuwalipie hawa maskini ada za mashamba ili wapate mikopo kutoka benki na kufanya biashara. Pia vijana wataweza kupata kazi. Bw. Naibu Spika wa muda, Hotuba ya Rais iligusia mambo mengi lakini nadhani alisahau kuzungumza juu ya shida ya wananchi kutokana na wanyama wa pori. Wakulima wetu wanasumbuliwa sana na wanyama wa pori, na hatupati ulinzi kutoka kwa Serikali. Wakati watu wanapoumizwa na wanyama hakuna fidia yoyote wanayolipwa. Hapa Bungeni tulipitisha Hoja iliyoletwa na mhe. Kiunjuri katika Bunge. Tuliipitisha Hoja hiyo, lakini Serikali ilishindwa kuleta Mswada Bungeni. Tuliupitisha Mswada wa mhe. G.G. Kariuki, lakini bado wananchi wanateswa na wanyama pori. Ningependa kumwomba Waziri Dzoro au msaidizi wake, Bw. Ndile, kwamba kama wanataka wanyama wa kupeleka Thailand wawachukue kutoka Lamu kwa vile hatupati watalii wa kuona wanyama pori. Kile tunachopata ni masumbuko kutoka kwa wanyama hao. Ningependa kuishukuru Serikali kwa kutoa kandarasi ya kujenga jetty inayotumiwa kuingia kisiwani Lamu. Wananchi wanafurahia jambo hilo na tunaishukuru Serikali. Watu wanasema kuwa uchumi wa nchi hii umeimarika kwa asilimia tano, lakini faida yake haionekani. Ninependa kulipinga wazo lao kwa maana katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni nilipewa Kshs24 milioni mwaka jana na mwaka huu tulipata Kshs29.5 milioni, na hili ni ongezeko. Kwa hivyo kusema uchumi haujaimarika kwa asilimia tano si kweli. Ni vizuri tutoe makosa panapofaa, lakini ukweli ulipo pia usemwe. Kwa hayo machache, naomba kuiunga mkono Hoja hii."
}