GET /api/v0.1/hansard/entries/255317/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 255317,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/255317/?format=api",
    "text_counter": 225,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 246,
        "legal_name": "Joseph Matano Khamisi",
        "slug": "joseph-khamisi"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Waswahili walisema: \"Mvumilivu hula mbivu!\" Nimevumilia tangu jana na sasa, nashukuru kupata nafasi hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, wakati Rais alitoa Hotuba yake, alizungumzia kuhusu Katiba. Alisema kwamba ameteua kamati itakayoshughulikia maswala ya Katiba. Nafikiri kwamba Rais hakupewa ushauri bora katika jambo hilo. Wakati tulipiga kura ya maoni na sisi upande wa chungwa tukashinda, ilitumainiwa kwamba tutarejelea kielelezo cha Bomas kilochotokana na maoni ya wananchi, taarifa na ripoti mbali mbali. Ingekuwa kazi rahisi kwa Bunge hili kushikilia usukani wa kusukuma jitihada hizo. Lakini kwa kutoa kazi hii kwa kamati au jopo kutoka nje--- Namheshimu sana Bw. Bethwell Kiplagat kwa sababu alikuwa Katibu Mkuu wangu katika Wizara ya Mambo ya Nje. Lakini naona kwamba hali hiyo ni hali ya kupotosha wananchi wa Kenya. Ningeomba kwamba jitihada hizo zirudishwe mikononi mwa wananchi wenyewe, badala ya kuwekwa chini ya mikono mwa jopoo lenye watu ambao hawakuwako tangu mwanzo, katika harakati za kutengeneza Katiba mpya. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa pia kutilia mkazo swala la ardhi ambalo sikulisikia likitajwa katika Hotuba ya Rais. Swala hilo ni nyeti sana katika nchi hii. Linafanya wananchi wetu March 29, 2006 PARLIAMENTARY DEBATES 215 kutaabika, kufukuzwa na kuchomewa manyumba na Serikali ambayo haitilii maslahi ya wananchi maanani. Ikiwa Serikali hii haiwezi kushughulikia swala la ardhi wakati huu, naona hatari zitakazokuja siku zijazo! Zinaweza kuadhiri utawala na shughuli za maendeleo katika nchi hii. Tumeona mambo hayo yakiadhirika katika nchi za Zimbabwe. Tumeona msukosuko kule Brazil na katika nchi zingine ambazo zimepuuza maswala ya ardhi. Tukizungumzia ripoti mbalimbali ambazo zimetengenezwa na Serikali - kama vile"
}