GET /api/v0.1/hansard/entries/255319/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 255319,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/255319/?format=api",
    "text_counter": 227,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 246,
        "legal_name": "Joseph Matano Khamisi",
        "slug": "joseph-khamisi"
    },
    "content": "na Anglo Leasing - na ambazo zimetajwa hapa mara nyingi, ningependa kurudia na kusema kwamba kuna umuhimu kwa Serikali kutekeleza Ripoti ya Akiwumi. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni zaidi ya miaka mitano sasa tangu michafuko ya kule Likoni ilipotokoea. Na tangu wakati huo, hali ya maisha katika sehemu ile haijarejea jinsi ilivyokuwa kabla ya mashambulizi hayo. Tunajua wazi kwamba ripoti ilitengenezwa na baadhi ya watu waliotajwa wako katika Serikali hii kama Mawaziri. Sielewi kwa nini Rais anaweza kuteua watu wanaojulikana wazi na ambao wametajwa katika ripoti za Serikali, kuwa ni watu ambao wanachochea hali ya kutokuweko na amani. Bw. Naibu Spika wa Muda, nikizungumzia kuhusu elimu, ninashukuru Serikali kwa kutekeleza elimu ya bure. Lakini kwa sababu ya kufurika kwa wanafunzi katika shule za msingi, kimefika wakati ambapo kuna umuhimu wa kuendeleza elimu ya bure katika shule za upili. Haina maana yoyote kuelimisha watoto wengi, maelfu na maelfu, ambao baada ya miaka minane hawana tena la kufanya. Hakuna polytechnic ambapo wanaweza kuchukuliwa na hakuna mipango yoyote ambayo inafanywa na Serikali kuweza kuwatumia vijana hawa kwa njia bora za maendeleo ya nchi hii. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba elimu ya shule za upili itolewe bure halafu tuangalie ni watoto wangapi ambao wataweza kufaidika katika mambo ya elimu na waweze kupata nafasi ya kuendelea na kuingia katika vyuo vikuu. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kuzungumzia juu ya taarifa ambayo imetolewa na Waziri wa Habari kuhusu kuajiri Wazungu kutekeleza mauzo ya nchi hii katika nchi za ng'ambo. Ninaona kwamba hatua hii ni haribifu, inaturudisha nyuma na itaendeleza ufisadi katika Serikali. Ninasema hivi kwa sababu niliwahi kufanya kazi kama ofisa wa habari katika ubalozi wetu katika nchi za ng'ambo. Ninajua kwamba wako maofisa ambao wana ujuzi na nafasi bora za mafunzo za kuweza kutekeleza kazi. Na watafanya hiyo kazi kwa sababu wanaifanyia nchi yao. Watakuwa na moyo na bidii, badala ya kutoa pesa nyingi kuandika Wazungu ambao hawana maslahi ya nchi hii katika akili zao. Kinachotakikana ni kwa Serikali kutoa vifaa vya kutosha kwa maofisa wetu wa kibalozi walio ng'ambo, kuwapa marupurupu yanayofaa kulingana na marupurupu yanayotolewa na nchi nyingine ili kuwapa uwezo wa kuuza nchi hii katika nchi za ng'ambo. Lakini ikiwa tutaanza kutajirisha Wazungu ambao, kusema kweli, hawahusiani na nchi hii, tutakuwa tunafanya makosa makubwa. Kwa hivyo, ninamwomba Waziri wa Habari afikirie tena shauri hilo ili tupate kufunza maofisa bora katika nchi hii na kuwapeleka nje wapate kufanya kazi hiyo. Kuhusu mambo ya kazi, ningependa kusema kwamba unyanyasaji katika mashamba yetu makubwa unaendelea. Katika mashamba ya kahawa, majani chai, mikonge, na mengine, wafanyakazi wanaishi maisha mabovu. Wanadhulumiwa kikazi, wakiwa wagonjwa hawashughulikiwi na kampuni hizo, na wanapata malipo duni. Hii ni aibu kubwa. Hii inaonekana kama utumwa mamboleo ambao unatokea katika mashamba yetu. Mimi ningemwomba Waziri ambaye amekuja hapa mwaka baada ya mwaka akituahidi kwamba atarekebisha sheria, za wanfanyi kazi kuwezesha mambo haya yaweze kurekebishwa afanye hivyo bila kukawia. Mpaka leo, Waziri yule angali anapiga usingizi. Tunataka tumuamshe na tumwambie kwamba wakati wa kuangalia masilahi ya wananchi wa Kenya umefika. Nimefurahishwa na hatua ya Serikali ya kutangaza kwamba itafufua kiwanda cha Kenya 216 PARLIAMENTARY DEBATES March 29, 2006 Meat Commission (KMC) hapa Nairobi. Nafikiri hili ni jambo nzuri. Wananchi wamekuwa wakingojea hatua hii kwa sababu wafugaji wamekuwa wakipata shida kubwa sana ya ukosefu wa soko la nyama na mifugo yao. Hata hivyo, ningependa pia kuikumbusha Serikali kwamba kiwanda cha KMC kilichoko Mombasa bado kimefungwa. Ingekuwa bora kwa Serikali wakati inafikiria kukifungua kiwanda cha Nairobi, pia ifikirie kukifungua kiwanda cha Mombasa ili wafugaji wapate soko. Naikumbusha tena Serikali kwamba tunazo kampuni ambazo zilifungwa wakati wa utawala uliopita na mpaka leo hazijafunguliwa. Moja ya kampuni hizo ni Kiwanda cha Korosho cha Kilifi. Ahadi za Serikali za kukifungua kiwanda hiki zimekuwa ni tupu. Ningependa Serikali ianze kufanya kazi na kutekeleza ahadi zake ilizotoa wakati wa uchaguzi ili kampuni hii ya Kilifi na kampuni za sukari na maziwa kule Kwale na Mariakani zipate kufunguliwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, nilimsikiliza kwa makini mhe. Mathaai akijaribu kuwatetea wanyama-mwitu na misitu badala ya kuwatetea binadamu. Kuna msitu wa Arabuko Sokoke katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni. Msitu huu umejaa ndovu ambao wanawasumbua na kuwahangaisha watu wangu. Ningependekeza msitu huo ukatwe nusu ili wananchi wapate kuitumia ardhi hiyo badala ya kuwepo maskwota kila mahali. Kwa jumla, Hotuba ya Rais ilikuwa ni mchanganyiko wa mambo pocho pocho. Lakini natumai kwamba pengine kuongoza vyema na kutimiza ahadi zake. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, naunga mkono."
}